Kuna njia nyingi ambazo mama anaweza kutumia kupima hali yake ya mimba. Kukosa kupata kipindi chake cha hedhi, huenda kukamfanya awe na shaka. Kufanya kipimo cha nyumbani kunamsaidia mama kufahamu iwapo ana mimba ama la. Kwa kasi, kwa usiri wa nyumbani mwake na bila kuwajuza watu wengine.
Manufaa ya kufanya kipimo cha nyumbani

- Ni kipimo cha kasi
- Unaweza kufanyia nyumbani bila kumjuza yeyote
- Ikiwa unaishi na mtu mwingine ambaye hungetaka ajue, ni rahisi kwake kuona kipima mimba cha kisasa, ila vigumu kugundua ulipo pima mimba kiasili
- Unatumia viungo vilivyo jikoni na rahisi kupata
- Ni cha bei nafuu
- Vilitumika hapo awali na vilikuwa na matokeo sahihi
- Unapimia nyumbani bila shaka za kwenda kununua kifaa cha kupima mimba
Uhasi wa vipimo vya nyumbani
- Havija egemezwa kisayansi kuwa sahihi
- Vinakawia kuonyesha matokeo
- Usipo kuwa makini kuna nafasi ya kusoma matokeo vibaya
Unafaa kuangazia nini katika vipimo vya mimba vya kinyumbani
Vipimo vya mimba hupima kuwepo kwa kichocheo cha hCG. Kichocheo hiki hutengenezwa mwilini baada ya yai kujipandikiza kwenye kuta za uterasi. Hiki ndicho kichocheo kinacho dhibitisha ikiwa mwanamke ana ujauzito ama la.
Unapo fanya kipimo cha mimba mapema sana, nafasi kubwa ni kuwa kiwango cha hCG mwilini kitakuwa kidogo na huenda kikakosa kudhibitika. Mwanamke ana shauriwa kufanya kipimo cha mimba wiki mbili baada ya kukosa kipindi chake cha hedhi. Baada ya wakati huu, viwango vya hCG huwa vimeanza kuongezeka mwilini. Kwa hivyo ni rahisi matokeo hasi kudhibitika mwanamke anapo fanya kipimo.
Kwa hivyo ikiwa viwango vya hCG viko chini sana, kipimo cha mimba kitakuwa hasi.
Jinsi ya kuhakikisha unapata matokeo sahihi

- Tumia mkojo wa kwanza kabla ya kunywa kiamsha kinywa. Mkojo wa kwanza wa siku huwa na kiwango cha juu cha kichocheo cha hCG
- Hakikisha unatumia chupa ama kontena safi kufanya kipimo cha nyumbani cha mimba
- Tumia kiwango tosha cha mkojo. Epuka kutumia kiwango kidogo sana ama kingi zaidi
- Kuwa mvumilivu na kukipa kipimo wakati tosha kabla, angalau dakika kumi
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Je, Kupima Mimba Ni Bei Ghali Ama Rahisi?