Kipimo cha ujauzito kwenye simu kina manufaa sana kwa mwanadada yeyote anayetaka kufahamu kama ana mimba au la.Teknolojia imesaidia sana jinsia ya kike kwani wamewezesha kipimo cha kupima mimba kwenye simu. Kuna vipimo aina nyingi ambazo kina dada hutumia kupima mimba kama vile ya zahanatini au ya kinyumbani. Kupitia njia hii mpya ya kupima mimba kwenye simu, kujua hali yako Imerahisishwa kwa kuwa mtu anapata matokeo hapo hapo na kwa haraka. Kulinganisha na vipimo vya hapo awali,kina dada walilazimika kwenda mpaka hostipitalini kupimwa,kisha baadae asubiri kwa muda mrefu ili apate matokeo.
Vipimo hivi vya simu vinafanya kazi vipi?

Kipimo hiki cha mimba hufanya kazi kama vipimo hivi vingine vya zahanatini. Kipimo hiki hupima kiwango cha homoni inayoitwa HCG, ambayo huanza kutengenezwa na mwili wa kina dada siku sita baada ya yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kujipandikiza kwenye nyuta za uterasi.
Kuna kijiti ambacho mtu hutumia kupima mkojo, katika teknolojia hii kijiti hiki huunganishwa na Bluetooth,kisha baadae matokeo hutumwa kwenye simu yako. Ili uweze kujua kama una mimba au la. Kipimo hiki huchukua muda wa dakika tatu. Unaposubiri unaweza kupata wosia kuhusu jinsi ya kulea mtoto,chakula bora ya kukula ukiwa mjamzito, njia bora mbali mbali za kuongeza kiwango cha uzazi.
Vipimo tofauti tofauti za kupima mimba

Kuna aina nyingi sana ambazo zinaweza kudhibitisha kama una mimba au la.
Kipimo cha mkojo
Kipimo hiki hususisha kuweka kijiti cha kupima mimba kwenye mkojo. Utafiti umetamatisha kwamba ni vyema kuchukua mkojo asubui ukiamka kabla ya kula kiamsha kinywa ili uweze kupata matokeo yaliyo sahihi kwa kiwango cha asilimia 99.Unapoeka mkojo katika kontena yako ,tia kijiti kile humo ndani.
Utafiti wa wataalam tofauti tofauti wa kisayannsi huhimiza kina dada kuchukua kipimo cha kipima mimba kwenye simu siku 14 baada ya siku ya yai la uzazi kurutubishwa kwenye kuta za uterasi.
Kipimo cha damu
Kiwango cha usahihi katika kipimo hiki huwa juu sana.Kipimo hiki huwa ni cha kisayansi. Kipimo hiki hupima asalimia ya homoni ya HCG katika mwili wako. Kina dada wanaweza kupima mimba wiki ya kwanza baada ya yai la uzazi kurubitishwa na kujipachika kwenye kuta za uterasi.
Dawa tofuati tofauti zinazoweza kuathiri matokeo ya kipimo cha mimba
- Promethazine
- Chlorpromazine
- Opioids
- Anticonvulsants
- Diuretics
- Dawa za kuongeza kiwango cha uzazi
- Dawa za usingizi
APP tofauti tofauti za kupima mimba kwenye simu
Kuna vipimo vingi ambavyo vinaweza kutumika kupima mimba kwenye simu. Kama vile:
- Pregnancy PRO
- Pregancy test Checker
- easyRead App
- Pregnancy APP
- Peanut
Uzuri wa APP hizi ni kuwa kuna kitufe ambacho unaweza kutumia kama unataka kutuma matokeo yako kwa mtu mwingine.Pia teknolojia hii huweza kukumbusha ingawa una miadi ya kumuona daktari wako. Kipimo cha ujauzito kwenye simu kinashauriwa sana lakini ni vyema baada ya kutumia kipimo hiki umwone daktari wako ili aweze kukuelekeza iwapo matokeo ni chanya.
Baadhi ya vipimo humshauri mtu kupima mara mbili au zaidi ili uweze kupata matokeo sahihi.i wapo utapima mara mbili kisha upate matokeo tofauti ni vyema kumuona daktari ili aweze kukupa majibu.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Nani Anapaswa Kuwa Na Mama Katika Chumba Cha Kujifungua?