Sio kila dalili za ujauzito ni ishara tosha kuwa mtu ana ujauzito. Hii ni kwa sababu dalili zingine huwa sawia na zile za siku za hedhi. Hivyo ili kuondoa taswishi ni bora kupima ujauzito. Kujua kipimo cha ujauzito nyumbani ni jambo la busara.
Kipimo Cha Ujauzito Nyumbani

Kwa kawaida mwili wa mwanamke hubadilika baada ya kutunga mimba. Ishara hizi ni kama vile Kukosa hedhi, jasho zaidi ya kawaida, kuwa na matiti na chuchu nyeti. Pia wanaweza kuhisi kukojoa zaidi na pia kichefuchefu. Pamoja na hizi dalili kufanya kipimo cha mimba nyumbani huondoa shauku.
Mara baada ya yai na manii kukutana, maumbile mbalimbali yanaunganika kutengeneza seli mpya. Seli hii mpya inagawanyika haraka na kila seli mpya iliyoundwa kugawanyika tena kuwa kiini-tete. Baadhi ya seli mpya ndani ya kiini-tete hukua na kufanyika plasenta ya mtoto. Hii plasenta ya mtoto huanza kutengeneza homoni inayoitwa Human Chorionic Gonadotropin (HCG).
Mara tu kiini-tete kinapojipandikiza kwenye uterasi, ndipo mtu hujulikana kuwa mjamzito. Utengenezaji wa homoni HCG huongezeka kwa wingi na hii homoni huamrisha mwili kuachisha hedhi. Kiwango cha HCG huzidi kuongezeka kadiri kiini-tete kinavyozidi kukua na plasenta yake inavyoendelea kukua.
Jinsi Ya Kufanya Kipimo Cha Mimba
Kipimo cha mimba nyumbani hulenga kutambua uwepo wa homoni (HCG) kwenye mkojo. Hii inafaa kufanyika baada ya siku sita. Huu wakati huwa tosha kwa yai kuwa limerutubishwa na kusafiri kwenye uterasi. Kufanya kipimo mapema sana kabla ya huu wakati unaweza pata majibu yasiyo sahihi. Pamoja na kuwa kipimo hiki ni rahisi na cha faragha pia ni cha haraka.
Kuna Njia Mbili za Kupima:
- Weka mkojo wako kwenye kikopo safi kisicho na mafuta ama kemikali. Kisha weka sehemu ya kupimia kwenye mkojo wako
- Shika sehemu ya kupimia ya kipimo chako kisha ukiwa unakojoa kiweke kwenye mtiririko wa mkojo ili kilowane
Baada yake subiri kwa muda mchache ili kupata majibu. Haya huonekana kwa kutokea kwa mistari miwili yenye rangi au kwa alama ya chanya(+) au hasi (-). Vipimo vya kigiditali huonyesha neno (pregnant) ujauzito au (not pregnant) hakuna ujauzito. Unaweza kununua vipimo vya ujauzito bila kuelekezwa na daktari katika maduka ya dawa au mtandaoni.

Wakati Mwafaka Wa Siku Kupima Ujauzito
Majibu sahihi kabisa huweza kupatikana asubuhi. Kipimo cha nyumbani hufanya kazi kwa kutambua homoni HCG kwenye mkojo. Mkojo wako wa asubuhi utakuwa na viwango vikubwa vya hii homoni isipokuwa kama uliamka usiku kujisaidia ama ukanywa maji mengi.
Uhakika Wa Vipimo Vya Nyumbani
Vipimo vya nyumbani vina uhakika kama utafuata maelekezo yalitolewa. Baadhi ya vipimo vina umakini wa kugundua haraka, rahisi kutumia na kutafsiri zaidi ya vingine. Umakini kugundua haraka katika kipimo ni mzuri zaidi maana unanyaka hata viwango vidogo vya HCG. Vipimo vya mimba vya kidigitali hutajwa kuwa na uhakika zaidi.
Ni vyema kusubiri baada ya siku moja baada ya Kukosa siku zako za hedhi. Kisha ufanye kipimo cha mimba nyumbani. Hivyo utaepuka majibu ya uongo. Ikiwa mzunguko wako wa hedhi haueleweki, usifanye kipimo hadi utakapopita mzunguko mrefu unaokuwa nao. Vipimo vya mimba nyumbani vimekubatiwa na wengi kwa sababu ya urahisi wa kutumia.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Fahamu Mambo Haya Kabla Ya Kushika Mimba Katika Miaka Ya 30’s