Mtangazaji Wa Kipindi Cha Kids Say the Darndest Things Nigeria

Mtangazaji Wa Kipindi Cha Kids Say the Darndest Things Nigeria

Kuna programu mpya inayo julikana kama kipindi cha Kids Say the Darndest Things Nigeria

kids say the darndest things Nigeria

Chanzo cha picha: okayafrica.com

Iwapo unatafuta programu ya kuchekesha, programu hii ya Kids Say the Darndest Things Nigeria ndiyo unayo tafuta na ni njema kwa familia yote kutizama.

Programu hii ya Kids Say the Darndest Things ni mali ya CBS huko Uingereza. Kipindi hiki ni maarufu katika pande za Uitaliano, Australia na Singapore.

Mtangazaji wa kipindi hiki huwauliza watoto wanao jumuika naye maswali ambayo hawakuwa wanajua, na majibu ya watoto ambayo hawakuwa wamepanga, yana chekesha.

Nani Mtangazaji Wa Kids Say the Darndest Things Nigeria?

Huenda ukawa unashanga uliko patana na Tony Okungbowa. Sio mgeni kwa televisheni zetu. Uso wake ni maarufu kwetu na hapo awali alikuwa ana fanya kazi na kipindi cha Ellen DeGeneres kama DJ. Ellen anapenda kusakata densi kwa ngoma za hivi sasa katika kipindi chake na Tony Okungbowa alimfanya akatike katika wakati wake kama DJ wa nyumba.

Okungbowa anapenda kazi yake mpya kama mtangazaji katika kipindi cha Kids Say the Darndest Thing Nigeria. Ana amini kuwa zaidi ya kicheko na kuchekeshwa, mzazi anaweza soma mengi kutoka kwa watoto wao. Anapenda kuwa watoto wanapata ushupavu wa kuja kwenye kipindi chake.

kids say the darndest things nigeria

Tony Okungbowa. Chanzo cha picha: the3as.com

Kipindi chaKids Say the Darndest Things kilianza lini Nigeria

Kipindi cha kwanza kuonyeshwa kwenye runinga kilikuwa, June 21, 2015. Hii ilikuwa siku sawa na siku ya kusherehekea wababa duniani al maarufu kama Father’s Day na kilionyeshwa kwenye DSTV na AIT.

Ni maswali yapi yana ulizwa katika kipindi hiki?

Programu ya kipindi hiki huwa wazi: kwa hivyo mtangazaji huwa uliza watoto maswali katika sekta za siasa, michezo, mazingira, kiroho na mambo ya kijumla. Maswali haya huwa mapya na watoto hawajui kuyahusu na wana himizwa kuya jibu kwa uwazi.

Mazingara huwa ya kirafiki na yenye furaha. Wazazi hukaa karibu na umati wa watu na kucheka pamoja na wengine watoto wao wanapo sema kitu cha kuchekesha.

Kids say the darndest things Nigeria

Chanzo cha picha: Bellanaija.com

Epic moments on Kids Say the Darndest Things Nigeria

Mtangazaji: Ungekuwa rais, ungefanya nini vitofauti?
Esther, wa miaka saba: Nitafanya Nigeria iwe mahali salama kwa kuleta aina tofauti ya candy

Mtangazaji: Ungependa kuwa nini ama nani unapo kua?
Onyinye, 7: Nitaanza kama daktari wa matibabu kisha nifanye kazi kama mshonaji wa mitindo hadi nife

Mtangazaji: Una rafiki mvulana?
Nkechi, 10: La
Mtangazaji: Unge penda kuwa naye iwapo angekupa kitu unacho kitamani zaidi maishani?
Nkechi: Nitachukua zawadi, nimshukuru vyema na kisha niseme kwaheri

Mtangazaji: Je, usemi a stitch in time saves nine’ una maana gani?
Ola, 8: Ina maana kuwa unapo enda nje, una paswa kurudi nyumbani saa tatu za usiku.

Mtangazaji: Kwa hivyo, Emmanuella, je una rafiki mvulana?
Emmanuella, 10: Apana, na wewe je?

Cha Kufanya Ili Watoto Wajiunge na Kipindi cha KSDT

Iwapo ungependa watoto wako wajiunge na kipindi hiki cha watoto, utahitajika kwenda vikao vya kusajiliwa. Wanao panga kipindi hiki hutangaza tarehe za kusajili watoto kwa vipindi vijavyo. KSDT Nigeria inataka watoto wacheshi, wenye busara na walio na utu wazi.

Resources: guardian.ng 

Also ReadMust-read Nigerian children’s books for 10 years and below

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio