Kisa Cha Kwanza Cha Kupona Kwa Mgonjwa wa Covid-19 Nchini Kenya

Kisa Cha Kwanza Cha Kupona Kwa Mgonjwa wa Covid-19 Nchini Kenya

Katika hotuba yake ya Jumatano tarehe 25 mwezi wa tatu mwaka wa 2020, kiongozi wa nchi alitangaza kisa cha kwanza cha kupona kwa covid-19 Kenya. Siku 12 baada ya kisa cha kwanza cha virusi hivi kushuhudiwa nchini. Kwa kweli kila wingu huwa na laini yake ya dhahabu. Hata serikali ilipotangaza kuwa idadi ya watu walio athirika ilifika 28, lakini kuna mwangaza unao anza kung’aa kwa kiza hiki kilicho ifunika dunia kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.

“Miongoni mwa haya yote, nafurahikia kutangaza kuwa kuna idadi kubwa ya watu wanao semekana kuwa na virusi hivi ambao vipimo vyao vina dhihirisha alama hasi. Kuna maana kuwa hawana virusi hivi. Cha muhimu zaidi ni uponyaji wa wagonjwa hawa. Ni dhihirisho kuwa tuna weza na tuta pigana na kukabiliana na virusi hivi,” rais Kenyatta alisema.

Kisa Cha Kwanza Cha Kupona Kwa Mgonjwa wa Covid-19 Nchini Kenya

Picha: Sonko news

Kupona Kwa Covid-19 Nchini Kenya

Rais Uhuru Kenyatta aliendelea kuwahakikishia wananchi  kuwa wagonjwa wote walikuwa wana  wana fuatiliwa kwa umakini ikiwa walikuwa kwa karantini ya kipekee ama ya kulazimishwa na serikali. Hata serikali ikifanya juhudi kuhakikisha kuwa wanaweka mikakati ipasavyo kuhakikisha kuwa wanaweka kikomo katika usambazaji wa virusi hivi vya homa ya korona.

Hotuba ya rais ilifuata siku moja baada ya waziri wa wizara ya afya Mutahi Kagwe kuhakikishia wakenya kuwa wagonjwa wote walikuwa wanaendelea vyema isipokuwa waathiriwa wawili walio kuwa wamekula chumvi. Kulingana na waziri, waathirika ni wa miaka kati ya ishirini (20) hadi miaka sitini na saba (67). Wote hawa walikuwa wametengwa kando na watu wengine ili kuhakikisha kuwa hawasambazi virusi hivi kwa watu wengine. Kulingana na sheria za Shirika La Afya Duniani (WHO), mtu anaye semeka amepona kutokana na virusi hivi anapaswa kudhihirisha vipimo viwili vilivyo hasi. Vipimo hivi vinapawa kuchukuliwa na tofauti ya masaa 24 kati yake.

kupona kwa covid-19 kenya

Hata baada ya mmoja huyu kuachiliwa kwenda nyumbani, madaktari bado hawana uhakika iwapo amepona kabisa ama atawaweka wengine kwenye hatari ya kupata virusi hivi vya homa ya korona. Ila walisisitiza kuwa wataendelea kufuatilia kisa chake kuhakikisha kuwa hako kwenye hatari ya kuwa hatadharisha wengine. Wataalum wa afya wanasema kuwa virusi hivi huenda vikabaki mwilini hadi wiki mbili baada ya kutangazwa kwa kupona kwa covid-19 nchini Kenya.

Hadi wakati huu, hakuna dawa ya virusi hivi iliyo dhibitika ila utafiti bado unaendelea kupata chanjo itakayo walinda watu dhidi ya maradhi haya. Kama virusi vingine vyovyote hamna dawa ya kuponya ila ni mfumo wa kinga wa mwili wako unao pigana na virusi hivi na kukuzuia kuugua. Iwapo mfumo wa kinga wa mwili wako uko chini, unashauriwa kula matunda mengi na vyakula vitakavyo uongeza mwili wako nguvu. Ili kusaidia kupigana na virusi vyovyote. Visa vingi vya watu wanao kufa kutokana na virusi hivi ni walio na mfumo wa kinga mwilini usio na nguvu. Watu wanao ugua magonjwa tofauti, kama vile walio na ugonjwa wa sukari, matatizo ya moyo ama walio zeeka. Hii si kusema kuwa wengine hawa athirika, ila nafasi zao ni chache kuliko wengine.

kupona covid-19 kenya

Idadi ya watu waliopona kutokana na virusi hivi katika bara la Afrika ni 183 kutoka nchi 15 tofauti Kenya ikiwa miongoni mwa nchi hizi. Ila nchi zote zilizo athirika na janga hili ni 43 katika bara la Afrika na wagonjwa 2,412. Visa vya vifo kutokana na maradhi haya sio mengi. Tunaendelea kutumainia kuwa hatutashuhudia visa zaidi na walio athirika watapona.

Chanzo: Daily nation

Soma Pia: Kafyu Nchini Kenya Kutekelezwa Kufuatia Visa Vyingi Vya Homa Ya Korona

Written by

Risper Nyakio