Katika wikendi iliyopita, Kisiwa cha Zanzibar imekuwa ikiongoza kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter kwa sababu zote zisizofaa. Hii ni baada ya mtalii mmoja wa kike kutoka Nigeria kwa jina Zainab Oladehinde kuchukulia mtandao wa kijamii wa Twitter kuhadithia jinsi alivyodhulumiwa kingono alipokuwa katika mojawapo ya mahoteli huko Zanzibar mwaka uliopita.
Kisa cha Zainab katika Kisiwa cha Zanzibar
Picha: Picha ya kurusa ya twitter
Zainab alielezea jinsi alivyofunga safari kutoka nchi yake ya Nigeria na kuelekea Zanzibar ambapo ni mahali pa utalii panaposifika kwa sana duniani kote. Alikuwa na furaha tele kwani, angesherehekea siku ya kuzaliwa kwake na kuidhinisha kufika umri wa miaka 23 katika mahali pa utalii pa ndoto zake.
Kuamkia siku ya Jumamosi, Zainab aliandika kwenye kurasa yake ya Twitter, “Ni wakati nizungumze kuhusu shuhudio langu katika Zanzibari kama msafiri wa kipekee wa kike. Tukio hili lilifanyika mwaka mmoja uliopita katika mwezi wa Aprili 2021, ila sijaweza kulizungumzia kwani nimekuwa katika tiba ama therapy kwa mwaka mmoja kupona kutokana na kiwewe cha kisaikolojia nilichokipata.”

Zainab alieleza jinsi ambavyo mtu asiye mfahamu karibia alimbaka kwenye chumba chake cha kulala katika hoteli ya pwani ya Warere huko Zanzibari. Juhudi zake za kupata haki katika kituo cha polisi huko Nungwi hazikufua dafu.
Siku ya kuwasili kwake
Picha: pexels
Zainab aliwasili katika hoteli hii jioni. Baada ya kuzungumza na jamii na marafiki wake na kuwajuza kuwa aliwasili salama, alizima sitima kisha kulala, kwani alikuwa na uchovu mwingi. Usiku alihisi mtu akimshika na mara ya kwanza kudhani kuwa alikuwa anaota. Alipogutuka usingizini, alifahamu kuwa kulikuwa na mwanamme juu yake aliyekuwa akijaribu kumdhulumu kingono. Aliweza kutoroka alipomwambia kuwa ana virusi vya ukimwi.
Siku iliyofuatia, alienda kuripoti kwenye kituo cha polisi, alipojulishwa kuwa hawawezi kufanya chochote kwani hakubakwa.
Usemi wa hoteli
Katika chapisho ambalo hoteli ilifanya katika mwitikio wa suala hilo. Walisema kuwa ni kweli Zainab alikuwa kwa hoteli yao katika kipindi kilichosemwa. Aliripoti kuwa mfanyikazi wa usalama wa kiume aliingia kwenye chumba chake na kujaribu kulala naye. Katika juhudi zao za kumsaidia Zainab, walimpeleka kwenye kituo cha polisi kuripoti. Alikataa kuendeleza suala hilo kortini na badala yake kuitisha malipo ya kifedha ya taslimu $10,000 kwa uharibifu uliofanyika.
Kauli ya serikali ya Zanzibar
Tume ya utalii ya kisiwa cha Zanzibar ilihakikisha kuwa imefungua utafiti kudadisi zaidi kilichotokea kuhusu kisa hicho cha kujutwa. Utafiti umeanza na ripoti itafanyika, tume ilizidi kusema.
Soma Pia: Zahanati Bora Zaidi Za Uzazi Nchini Kenya