Ulifahamu Kuwa Kitunguu Saumu Kinaongeza Viwango Vyako Vya Manii?

Ulifahamu Kuwa Kitunguu Saumu Kinaongeza Viwango Vyako Vya Manii?

Kitunguu saumu ni chakula bora katika kuongeza viwango vyako vya manii.

Lishe huchangia pakubwa katika ubora wa kiwango cha manii. Utafiti mkuu unadhibitisha kuwa asilimia 90 ya ukosefu wa uzazi kwa wanaume unasababishwa na kiwango kidogo cha manii. Habari nzuri ni kuwa, mabadiliko ya lishe inaweza changia pakubwa katika kubadilisha jambo hili. Iwapo unashangaa jinsi ya kuongeza kiwango chako cha manii kwa chakula, usitafute zaidi! Kuna vyakula vya miujiza ambavyo vinaweza kusaidia kutatua shida hii. Ulifahamu kuwa kitunguu saumu kinaongeza viwango vyako vya manii? Soma zaidi:

Jinsi Kitunguu Saumu Kinaongeza Viwango Vyako Vya Manii: Je, Kiwango Kidogo Cha Manii Ni Nini?

Kiwango chako cha manii ni idadi ama nambari ya manii iliyoko kwenye kila milimita ya unyevu wa kiume. Mwanamme anasemekana kuwa na kiwango kidogo cha manii iwapo anashindwa kutoa kiwango tosha cha manii kinacho hitajika kutunga yai la mwanamke. Hii haina maana kuwa mwanamme hawezi mpachika dada mimba.

garlic increases sperm count

Kiwango cha manii na uhai wake

Kiwango cha kawaida cha manii kina maana kuwa kuwepo kwa milioni 20 za manii kwa kila milimita ya unyevu wa kiume (semen). Kuwa na viwango vya kawaida kwa mwanamme hakumaanishi kuwa ana uzazi bora. Mwanamme anaweza kuwa na kiwango cha kawaida cha manii na bado awe na tatizo iwapo manii hayana mwendo kufikia mayai.

Uchambuzi wa manii unaangalia pande zote za manii. Saizi na mwundo wa manii. Ikiwa mwundo wake si wa kawaida ama saidiz yake ni kubwa sana, huenda yaka sababisha kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto ama kusababisha kuharibika kwa mimba.

Sababu za kiwango kidogo cha manii

Kuna sababu nyingi zinazo sababisha mwanamme kutokuwa na viwango tosha vya manii:

 • Fikira nyingi
 • Uvutaji wa sigara
 • Unywaji wa vileo
 • Testicular blockage
 • Maambukizi
 • Chromosomal defects
 • Madawa
 • Matatizo ya kumwaga manii
 • Kutokuwa na usawa wa manii
 • Ukuaji usio wa kawaida
 • Uzito mwingi
 • Joto jingi
 • Mavazi yanayo kubana sana

Athari za kiwango cha chini cha manii

Wanaume walio na kiwango cha chini cha manii wana mengi ya kuwatatiza mbali na kutokuwa na uwezo wa ulezi. Kuna watafiti wanao sema kuwa kiwango cha manii cha mwanamme ni kipimo cha ujumla cha afya yake. Kipimo kinapo kuwa chini, mwanamme anapaswa kutahadhari.

Kulingana na daktari Alberto Ferlin, kiwango cha chini cha manii huenda kikawa ni ishara ya uzito mdogo wa mifupa, matatizo ya moyo na ya mfumo wa chakula.

Jinsi ya kutibu kiwango kidogo cha manii

Kwa bahati nzuri, kuna matibabu ya kiwango kidogo cha manii. Machaguzi ya matibabu yana tegemea na chanzo cha tatizo lako.

Matibabu ya kinyumbani ya kiwango kidogo cha manii

Hii ndiyo hiari njema zaidi ya kiwango kidogo cha manii kwa hormonal imbalance. Mwili unapo toa kiwango kidogo cha homoni ama kingi zaidi, huenda ika athiri utendaji kazi wa kibiolojia.

Dawa hizi zinafanya kazi kuregesha utendaji kazi wa kawaida wa homoni na kusawasisha kila kitu. Na kufanya manii yako yawe na viwango vya juu. Ni muhimu kutibiwa na daktari aliye na vyeti atakaye zingatia maendeleo yako.

Upasuaji kutatua shida ya kiwango cha chini cha manii

Baadhi ya wakati, kiwango kidogo cha manii kitahitaji upasuaji. Katika kesi hi, tatizo huenda likawa kufuatia mishipa iliyo vimba na kuhitaji upasuaji.

Matibabu ya viwango vidogo vya manii

Madaktari wata kushauri kutumia dawa iwapo matatizo yako yanatokana na maambukizi. Tatizo hili litaisha  baada ya kuanza matibabu.

Lishe ya viwango vya chini vya manii: Jinsi vyakula bora kama kitunguu saumu vinaongeza wingi wa manii

Lishe ni sehemu muhimu ya maisha yenye afya. Lishe bora inaweza hakikisha kuwa hauna matatizo ya kiafya na kuyatibu unayo yapitia. Tuliku eleza hapo awali kuwa kitunguu saumu kinaongeza viwango vyako vya manii. Kuna vyakula vya kiasili unavyo paswa kuongeza kwa lishe yako iwapo ungependa kuwa na manii mengi. Kama vile:

 1. Oysters

Oysters zina wingi wa amino acids, zinazo saidia kuongeza utoaji wa testosterone kwenye waume na progesterone kwenye wake. Homoni hizi mbili ni muhimu sana katika kupata hamu ya ngono na kupata watoto.

kitunguu saumu kinaongeza viwango vyako vya manii

 

2. Mandizi

Unaweza pata mandizi pahali popote pale unapo ishi. Ndizi zina bromelain ambayo ni muhimu sana katika kupata hamu ya ngono. Iwapo ungetaka kuongeza viwango vyako vya manii, hakikisha kuwa unakula ndizi mara kwa mara.

Ulifahamu Kuwa Kitunguu Saumu Kinaongeza Viwango Vyako Vya Manii?3. Kitunguu saumu

Kitunguu saumu ni mojawapo ya matibabu ya nyumbani yanayo fahamika duniani kote. Baadhi ya watu wana apa kwamba chembe chache za kitunguu saumu zinaweza ponya maambukizi na hata matatizo ya moyo. Unaweza ongeza kiwango chako cha manii kwa kutumia kitunguu saumu. Ina viwango vya juu vya allicin- ambayo ni sulfur inayo sifika kutengeneza mamilioni ya manii. Iwapo unatumia kitunguu saumu kutatua hali ya kiwango cha chini cha manii, kumbuka kuto furahia sana na kula viwango vingi ili watu wasi nusie harufu yako ya kitunguu saumu kwa umbali. Na hivi ndivyo kitunguu saumu kinavyo ongeza kiwango chako cha manii.

kitunguu saumu kinaongeza viwango vyako vya manii4. Chokleti nyeusi

Kuongeza wingi wako wa manii huenda ikawa safari tamu. Kula chokleti nyeusi ili kupata viwango vingi vya L-Arginine HCL, ambayo ni amino acid itakayo ongeza viwango vyako vya manii.

5. Ginseng

Unaweza pata bidhaa za ginseng kweny duka la mboga na haipaswi kuwa vigumu kuipata. Ni maarifa sana sehemu za Asia, ila sasa wanasayansi siku hizi wana zisifu kila mahali. Kwa hivyo iwapo unataka kuongeza hamu yako ya ngono, ama utendaji bora wa ngono, hili ndilo jibu lako.

6. Karoti

Karoti zina kiwango cha juu cha vitamini A, inayo hitajika zaidi katika utoaji na mwendo wa manii. Ni rahisi sana kupata karoti kutoka sehemu yoyote ile unayo ishi. Unaweza pata karoti mahali popote iwapo unashangaa jinsi ya kuongeza manii kwa kutumia chakula.

kitunguu saumu kinaongeza viwango vyako vya manii7. Parachichi

Parachichi ni jibu mwafaka kwa wanaume wanao taka kuongeza kiwango cha manii yao kwa kupitia vyakula. Ina wingi wa antioxidants, na kukusaidia kupata manii zaidi.

8. Mayai

Ni jambo la kupendeza kuwa kula mayai huenda kukakusaidia kupata manii tosha ya kutunga yai. Mayai yana wingi wa protini na Vitamini E, na pamoja hizi mbili zinashirikiana kulinda manii kutokana na radicals ambazo huenda zikapunguza kiwango chake.

Soma Pia: Natural foods to help you last longer in bed

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio