Chakula Cha Mimba: Je, Ni Salama Kula Kitunguu Saumu Ukiwa Na Mimba?

Chakula Cha Mimba: Je, Ni Salama Kula Kitunguu Saumu Ukiwa Na Mimba?

Kitunguu saumu ni chakula kikuu kinacho sifika kufuatia faida zake za kiafya. Ila ukila saumu ukiwa na mimba, hapa kuna vitu unavyo paswa kuangazia.

Wakati ambapo huenda baadhi ya vyakula vikawa salama kula kwa ujumla, huenda zikawa hatari kwa wanawake wakiwa na mimba. Kitunguu saumu kinasifika kwa kuwa chakula kizuri na chenye faida nyingi kwa afya yetu na kulinda dhidi ya maradhi tofauti. Tuna angazia athari za kitunguu saumu kwa mama aliye na mimba.

Kitunguu saumu ni salama kwako na mtoto wako unapokuwa na mimba?

Kwa miaka mingi, kitunguu saumu kimejulikana duniani kote kwa faida zake za kiafya. Kina wingi wa organosulfur, ambayo ina kipa ladha na harufu na pia faida zake za afya. Faida hizi za kiafya huathiri wanawake walio na mimba, ila swali ni iwapo saumu ni salama. Jibu kwa swali hili sio dhahiri kwa wanawake walio na mimba.

kitunguu saumu na mimba

Kwa miaka mingi iliyopita, hakuna masomo yaliyo dhihirisha kuwa kitunguu saumu sio salama kwa mama mwenye mimba, na wala hawakupata kuwa ni salama. Hata kama baadhi ya watafiti wanawakubalisha wanawake wenye mimba kula saumu, ila katika miezi ya kwanza ya mimba. Hii ni kwa sababu wanaweza faidika na baadhi ya faida za kiafya za kitunguu saumu kwani mimba bado haijakua na hakuna hatari kwa mtoto. Na hata katika kipindi hicho, lazima wakule katika viwango vidogo. Halafu katika trimesta ya pili na tatu, hawa shauriwi kula saumu kwa sababu ya athari zake. Katika hatua hii, athari hasi za kitunguu saumu huwa kupunguza shinikizo la damu na kufanya damu iwe nyembamba. Iwapo ungetaka kula saumu ukiwa na mimba, ongea na daktari wako. Ata kushauri iwapo ni sawa kula kitunguu saumu ama la, na ikiwa lazima ule, atakushauri kiwango unacho faa kula.

Faida za kula kitunguu saumu unapokuwa na mimba

Hapa chini kuna faida za kiafya za kitunguu saumu unapokuwa na mimba.

  • Kupunguza athari za kupata shinikizo la juu la damu

Kitunguu saumu kina sifika kwa kutibu na kulinda dhidi ya matatizo ya moyo. Wanawake wenye mimba wanaweza faidika kwani shinikizo la juu la damu ni tatizo la kawaida ukiwa na mimba. Shinikizo la damu ni hali moja inayo athiri mmoja kati ya wanawake kumi walio wajawazito. Kitunguu saumu hupunguza nafasi za mwanamke mwenye mimba kupata shinikizo la juu la damu.

kitunguu saumu na mimba

  • Kuongeza uzito wa mtoto

Uzito wa chini ni mojawapo ya matatizo ya mimba na kitunguu saumu chaweza kukusaidia kukabiliana na changamoto hii. Kulingana na masomo, kitunguu saumu huongeza uzito wa watoto wanaokuwa katika hatari ya kuzaliwa wakiwa na uzito wa chini. Wakati ambapo kina punguza nafasi za matatizo ya kuzaliwa, kitunguu saumu huboresha ukuaji wa seli zilizoko kwenye placenta.

  • Kupunguza cholesterol

Kitunguu saumu ni chanzo cha allicin, inayo kuwa bora katika kupunguza viwango vya cholesterol na kuhakikisha kuwa havipiti viwango. Kwa ujumla, kitunguu saumu kinapo katwa hupunguza hatari za matatizo mengine ambayo huenda yaka ibuka kufuatia maradhi ya moyo.

  • Kulinda dhidi ya saratani

Aina fulani za saratani huenda zika epukwa kwa kula kitunguu saumu, hasa saratani ya colon, hata kama utahitajika kula saumu mara nyingi, ambayo sio nzuri kwa wanawake walio na mimba. Somo lililo fanyika Uchina lina egemeza wajibu wa kitunguu saumu katika kulinda dhidi ya saratani. Kulingana na NCI ( US National Cancer Institute), kula kitunguu saumu na kitunguu cha kawaida hupunguza hatari za saratani ya tumbo.

  • Kulinda dhidi ya homa na maambukizi

Mwanamke anapokuwa na mimba, lazima ahakikishe kuwa ana afya kuepuka kuchukua matibabu. Hii ni kwa sababu baadhi ya matibabu yana athiri mwili wako na wa mtoto wako. Kula saumu husaidia kukumbana na homa, kuchemua na maambukizi mengine kwa kuhakikisha kuwa mfumo wako wa afya una afya kadri iwezekanavyo.

  • Kulinda dhidi ya maambukizi ya ngozi

Mwanamke anapokuwa na mimba, kuna mabadiliko mengi yanayo fanyika kwenye ngozi yake na kitunguu saumu chaweza saidia kulinda dhidi ya tatizo hili. Kitunguu saumu kina vitu ambavyo ni muhimu katika kulinda dhidi ya maambukizi ya ngozi.

Athari za kula kitunguu saumu unapokuwa mjamzito

kitunguu saumu na mimba

Hata na faida za kiafya, kitunguu saumu huenda kikawa na athari hasi, hata kwa wanawake wenye mimba. Hizi ni baadhi ya athari hasi ya kula kitunguu saumu unapokuwa na mimba.

  • Kitunguu saumu kinaweza sababisha kutokwa na damu katika utaratibu wa upasuaji kwa sababu ya uwezo wake wa kufanya damu iwe nyembamba.
  • Ulaji mwingi wa kitunguu saumu huenda ukasababisha shinikizo la damu kupunguka. Hii ni nzuri kwa wanawake walio na mimba wenye shinikizo la juu la damu, ila plae tu ambapo shinikizo la damu halipunguki sana. Hili linapo tendeka, huenda mwanamke akashtuka na kuzirai.
  • Huenda kitunguu saumu ikapunguza uwezo wa kutumia iodine mwilini, inaweza sababisha hali ambapo thyroid gland haitoi homoni tosha.
  • Kitunguu saumu kinaweza kuwa na athari hasi kinapo chukuliwa na aina fulani za matibabu ili kupunguza viwango vya sukari ya damu.

Kabla ya kuchukua saumu, ni vyema kuwasiliana na daktari wako. Kitunguu saumu huenda kikawa salama kwa wanawake mjamzito kinapo kuliwa kwa viwango vidogo, ila haupaswi kupuuza kuongea na daktari wako kuhusu jambo hili.  Ata kushauri kiwango ambacho ni salama kwako na kwa mtoto ambaye hajazaliwa.

Soma pia: Garlic benefits for men: Why should you really consume it?

Web MD

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio