Klabu maarufu ya The Alchemist Bar iliyoko Westlands Nairobi imefungwa ili upelelezi ufanyike. Hii ni baada ya klabu hii kushtakiwa kuwa na ubaguzi wa rangi. Klabu ya Alchemist yafungwa baada ya Wakenya kuanzisha mada kuwa imekuwa na ubaguzi wa rangi kwa muda sasa.
Kulingana na kauli yao rasmi, uongozi wa klabu hii walisema kuwa hatua hii ni ya muda mfupi ili kuipa serikali ya kaunti ya Nairobi chanya na muda tosha kufanya upepelezi kuhusu mashtaki kuhusu klabu ile.

Kauli yao ilisoma, “Baada ya kushauriana na serikali ya kaunti ya Nairobi, The Alchemist imekubali kufunga milango yake kwa muda huku upelelezi ukifanyika kwa siku chache zijazo.
Usiku wa Mei 20, 2022, video ilitanda kwenye mitandao ya kijamii ambapo Mkenya mmoja alionekana kufurushwa kutoka kwa laini ya wazungu. Video hiyo ilionyesha foleni mbili, moja ya wakenya na nyingine ya wazungu. Mwanamme huyo alipojaribu kujiunga na foleni ya wazungu, alifurushwa vikali na walinda lango.
Video hii imewakasirisha Wakenya ambao hawaamini kuwa ubaguzi wa rangi unatendeka kwa nchi yao. Huku Wakenya wengi wakijitokeza na kusema waliyoyapitia wakiwa kwenye klabu hii.
Gavana wa kaunti ya Nairobi Ann Kananu pia alibatilisha leseni ya klabu hii kuendelea na operesheni zake mjini wa Nairobi.
Klabu hii ilifunguliwa mwaka wa 2015, Disemba 31. Alchemist inamilikiwa na Peng Chen na mchumba wake Michelle Morgan.
Picha: The Alchemist254 Instagram
Walinda lango watafanyiwa upelelezi kudhibitisha wanachostahili kufanyiwa. Kulingana na wasimamizi wa klabu hii, muda huu ambapo wamefunga utawapatia chanya cha kuajiri na kuwapa mafunzo wafanya kazi wapya.
Wakenya wamekuwa na maoni tofauti baada ya kusikia kuwa klabu ya alchemist imefungwa. Wengi wao wakifurahi na kukashifu ubaguzi wa rangi nchini mwao.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Mavazi ya Watu Mashuhuri Kwenye L’Oreal High Tea Kenya