Unamfahamu Koffee? Yeye Ndiye Mwanamke Wa Kwanza Kushinda Tuzo La Grammy La Album Bora Zaidi Ya Reggae

Unamfahamu Koffee? Yeye Ndiye Mwanamke Wa Kwanza Kushinda Tuzo La Grammy La Album Bora Zaidi Ya Reggae

Koffee alitoa wimbo kuhusu mkimbiaji Usain Bolt kwa jina 'Legend' na wimbo huu ukatamba katika mtandao wa Instagram na kumpa umaarufu.

Mikayla Simpson, anaye fahamika kama Koffee kwenye tasnia ya muziki alifanya historia Jumapili. Ali shinda tuzo la Grammy la mwana muziki bora zaidi kwa album yake ya reggae na jina lake kuingia katika historia ya reggae. Dunia itaishi kumkumbuka Simpson kama mtu mchanga zaidi na mwanamke wa kwanza kushinda tuzo la Grammy la Album nzuri zaidi ya Reggae. Kulingana na eDaily, Koffee mwenye miaka 19, alishinda tuzo la EP yake ya reggae ya 'Rapture' iliyo tolewa mwaka ulio pita.

EP hiyo ilikuwa na nyimbo nyingi, ikiwemo wimbo wa 'Toast' wimbo uliokuwa wa kwanza kwenye charti za Billboard za Reggae. Na kubaki katika nambari hiyo kwa wiki 32.

Koffee ni nani? Fahamu machache kumhusu

Mwimbaji huyu alizaliwa mwaka wa 2000, na kulewa na mama yake peke yake katika mtaa wa Spanish, nje ya Kingston. Aliimba kwenye kikundi cha kanisa kama mtoto na kujifunza kucheza guitar akiwa na umri wa miaka 12.

Koffee alianza kuandika nyimbo akiwa katika miaka yake ya ujana; huku aki hamasishwa na waimbaji mashuhuri wa reggae kama Chronixx na Protoje.

Katika mwaka wa 2017, Koffee alitoa wimbo kuhusu mkimbiaji Usain Bolt kwa jina 'Legend' na wimbo huu ukatamba katika mtandao wa Instagram. Wimbo uliofuata wa "Burning" uliongoza kwenye charti nyingi za reggae huko Umarekani.

Mwaka wa 2018, akiwa na miaka 18, Simpson ali igiza pamoja na Protoje na Chronixx, kisha akaenda zuru ya U.K.

Kulingana na Allmusic.com, hali ya utambaji wa nyota ya Koffee uling'aa zaidi alipo weka saini na Columbia U.K.. Kisha akatoa nyimbo za "Toast" na "Ragamuffin" zote ambazo zilitokea kwenye EP yake ya kwanza ya Rapture mwaka wa 2019.

Alipokuwa akichukua tuzo yake, Koffee aliyasema haya

Koffee aliwa shukuru walio msaidia katika muziki na wana muziki wengine kama vile Julian Marley na Steel Pulse; "kwa juhudi zote walizo tia kwenye tasnia ya muziki wa reggae na muziki kwa kijumla. Nimesoma mengi kutoka kwao na watu wengine wazee kwenye tasnia na hiyo ndiyo sababu kwa nini niko hapa; kilicho tuleta hapa." alisema.

Na kuzidi kusema kuwa ana hamasishwa sana na marehemu Bob Marley.

Vyanzo: Guardian, All Africa Stories, Face2Face Africa

Soma Pia:Mwigizaji Nyota Maarufu Chadwick Boseman Aaga Dunia

Written by

Risper Nyakio