Koma Kuwaambia Vijana Vitu Hivi: Kuwalea Vijana Kwa Njia Inayo Faa

Koma Kuwaambia Vijana Vitu Hivi: Kuwalea Vijana Kwa Njia Inayo Faa

Koma kuwaambia vijana wadogo vitu hivi 10. Ili wakue waki waheshimu wasichana na pia uwawezeshe kuwa wanaume bora kwa jamii.

Uwezeshaji wa wanawake #women empowerment, kupigana dhidi ya ubaguzi - dunia inabadilika. Sehemu kubwa ya mabadiliko haya ina kutegemea, wamama na jinsi mna lea vijana wenu. Ukitaka kijana wako akue akiwa sawa pande zote, mwenye heshima na mwenye ukarimu kwa kila mtu, unapaswa ku koma kuwaambia vijana vitu hivi 10!

Vitu 10 Unapaswa Kukoma Kuwaambia Vijana

stop telling your sons1. "Kua mgumu"

Watu wengi hufikiria wanaume ni wagumu na shupavu na wanawake wana hisia na mhemko. Hiyo ndiyo sababu kwa nini wewe huona wababa wengi wakiwaambia vijana wao wawe wagumu na wasilie.

Walakini, ukweli hauwezi kuwa tofauti sana. Ni kawaida kwa baadhi ya wanaume kuwa na hisia, wakati ambapo wanawake wengine ni shupavu na wagumu. Watu huzaliwa wakiwa tofauti kabisa, na hai husishwi na jinsia yao.

2. "Una tenda kama msichana"

Kuna maana gani "unafanya kama msichana?" Ukifikiria kwa makini kuhusu jambo hili, watoto wachanga wa kike na kiume huwa na tabia sawa na wanapenda kufanya vitu sawa.

Kumwambia mtoto wako wa kiume kuwa "anafanya kama msichana" ni kama tusi. Lakini hakuna kitu mbaya na kuwa msichana.

Kama mzazi, ni muhimu kuwafunza watoto wako wangali wachanga kuhusu usawa, na usiwafanye watoto wako wafikirie kuwa jinsia moja ni kuu kuliko nyingine.

3. "Unapaswa kuwa mwanamme"

Kuna maana gani 'kuwa mwanamme?' Kwa sehemu kubwa, kuna maana kuwa vijana wanapaswa kukua na kuwa kama vile imani za mwanamme wa jadi.

Lakini siku hizi, hakuna kitu kama hicho. Wanaume huja kwa shepu na saizi zote, kila mmoja ana ubinafsi na upekee wake wa kitabia. Badala yake, wafunze wanao wa kiume kujikumbatia, kujikubali na kuwa na fahari yake.

Koma Kuwaambia Vijana Vitu Hivi: Kuwalea Vijana Kwa Njia Inayo Faa

4. "Lazima uwe mkubwa na mwenye nguvu"

Tena, hii ni imani isiyo ya kweli ya mwanamme "mkubwa na mwenye nguvu". Kwa ukweli, wanaume wote sio wakubwa na wenye nguvu za mwili - inalingana na geni zake. Wazazi wana paswa kuona fahari kwa vijana wao wakati wote, sio kuwa lazimisha kuwa kama imani zilizo pitwa na wakati za jinsi mwanamme anavyo paswa kuwa.

5. "Hilo sio jambo la wavulana"

Unasikia hivi mara nyingi wakati ambapo vijana wadogo wana cheza na vidoli 'vya wasichana'. Lakini nini mbaya na wavulana wadogo kucheza na vidoli? Ama kucheza michezo ya kupika?

Vidoli ni vidoli, na watoto wanapenda kucheza. Haijalishi iwapo wanafanya vitendo na vidole ama vidoli, kinacho jalisha ni kuwa watoto wana furahia na wana soma.

Pia katika nguo na rangi, jambo hili ni sawa. Aliye sema kuwa wavulana hawa wezi valia pinki kwa sababu ni rangi ya wanawake. Kama mtoto mdogo anataka kuvalia sharti la pinki, usiwa kataze.

Koma Kuwaambia Vijana Vitu Hivi: Kuwalea Vijana Kwa Njia Inayo Faa

6. "Unataka watu wafikirie wewe ni msichana?"

Hili ni jambo lingine ambalo wazazi huambia vijana wao. Ikiwa wewe ni mojawapo wa wazazi hao, tafadhali koma kuwaambia vijana wako maneno kama hayo.

Hakuna kitu kibaya na kuwa msichana, na wazazi wanapaswa kuwa kwenye usukani wa kutupilia mbali imani hizi za kale.

Kama mzazi, unapaswa kukubali na kuelewa watoto wako sio kuwa hukumu.

7. "Wanaume hawalii"

Ni sawa kwa vijana kulia. Iwapo kijana wako anahisi huzuni, ni sawa kwake kujieleza kwa kulia. Hii ni kawaida.

Kukubali hisia za mtoto ni muhimu sana, na kulia ni mojawapo ya njia ambazo mtoto anaonyesha hisia zake. Na wazazi hawapaswi kuingilia njia ya mtoto kuonyesha hisia zake.

8. "Hii itakubadilisha kuwa mwanamme"

Kitu cha pekee kinacho wabadilisha vijana kuwa waume ni utaratibu asili wa kukua. Hakuna tabia hasa inayo wafanya vijana kubadilika kuwa waume. Kusema jambo hili kutawafanya watoto wahisi vibaya kuhusu maisha yao wasipo ishi jinsi mwanamme anavyo paswa.

9. "Vijana watakuwa vijana"

Kuwa ambia wavulana kuwa "vijana watakuwa vijana" ni kuwafunza kuwa wanaume hawapaswi kuchukua jukumu la vitendo vyao.

Iwapo mtoto anafanya kila kitu vibaya, usikubalishe ipite kwa sababu "vijana watakuwa vijana." Inakuza tamaduni kuwa wanaume wanakubalishwa kufanya wanacho taka, bila kutafuta vijisababu vyovyote.

10. "Wewe ni msichana?"

Koma kumwambia kijana wako jambo hili. Kuna fanya kukae kana kwamba kuwa msichana ni jambo mbaya, na si kweli.

Jambo hili halimpuuzi kijana wako tu, mbali wanawake wote kwa ujumla. Kumwita mtu msichana haipaswi kuwa tusi katika wakati wowote ule.

Chanzo: Psychology Today

Soma piaMambo 14 Ya Kuwachilia Ili Uwe Mzazi Mwenye Furaha

Written by

Risper Nyakio