Krimu Bora Zaidi Kwa Ngozi Nyeupe: Kutunza Ngozi Yako Na Ya Familia Yako

Krimu Bora Zaidi Kwa Ngozi Nyeupe: Kutunza Ngozi Yako Na Ya Familia Yako

Baadhi ya chapa za ngozi na uso zinazo aminika zaidi kwa utumizi kwenye ngozi nyeusi.

Ngozi ya Kiafrika bila shaka ni tofauti kutoka na zinginezo za watu kutoka bara zingine. Hii ndiyo sababu kwa nini kutumia krimu yoyote ama zilizo tengenezwa za watu weupe huenda ika athiri ngozi yako. Huku wana Afrika wengi wakiamua kukaa mbali na hydroquinone, kojic acid na kemikali zingine za kueusha ngozi, swali ni: Krimu bora kwa ngozi nyeupe ni zipi?

Cha kufurahisha ni kuwa watu wenye ngozi nyeusi wanapendelea bidhaa za shea butter na cocoa butter kama utaratibu wa ngozi zao. Sio jambo geni kuwa nyanya zetu pia walipenda shea butter ambayo kwa miaka mingi imekuwa bidhaa ya lazima kwa utunzaji wa ngozi nyeusi kwenye dunia ya hivi sasa. Kwa pamoja, tuangazie, krimu bora kwa ngozi nyeupe. Haijalishi rangi ya ngozi yako, ngozi yako ni mojawapo ya zawadi bora ambazo ulituzwa, kwa hivyo unapaswa kuichunga. Tizama orodha ya krimu zitakazo ifaa ngozi yako zaidi.

Angalia Orodha Ya Krimu Bora Kwa Ngozi Nyeupe Ambazo Wanawake Wanapenda

Dermatological E-45

best cream for dark skin tone

Hii ni mojawapo ya krimu zinazo nunuliwa zaidi Uingereza. Inaponya ngozi iliyo kauka zaidi. Wanao itengeneza wametengeza aina mbili ya chapa hizi, zote ambazo zinasaidia kuilainisha ngozi yako. Kuna krimu nene na mafuta. Mojawapo ya vitu vya kupendeza kuhusu bidhaa hii ni kuwa kila mtu kwenye familia yako anaweza kuitumia ikiwemo watoto. Haina harufu za kuongeza, na ndiyo mojawapo ya sababu kwa nini inatambulika kama krimu bora kwa ngozi nyeusi.

Nyraju

Krimu Bora Zaidi Kwa Ngozi Nyeupe: Kutunza Ngozi Yako Na Ya Familia Yako

Bidhaa hii imetengenezwa hasa kwa ngozi ya aina yako. Iwapo unatafuta krimu nzuri ya mwili ya ngozi nyeupe, unaweza pata kwimu hii kwa maduka yaliyo karibu nawe. Hasa zinazo husika na bidhaa za ngozi na mwili. Mbali na krimu, kuna matibabu ya scrubs, na kila kitu kinacho husika na ngozi.

Nivea Naturally Even

krimu bora kwa ngozi nyeupe

Krimu hii ina wingi wa vitamini E na UV filters ambazo zinasaidia kupunguza kupata madoa. Itasaidia ngozi yako kuwa na rangi sawa kote. Pia utaweza kukabiliana na kuzeeka mbio kunako sababishwa na kueuka. Chapa hii ya Nivea ina bei nafuu na inapendwa na watu wengi wenye rangi nyeusi.

Krimu bora kwa ngozi nyeupe: Aveeno Daily Moisturizing

best cream for dark skin tone

Krimu hii ina ipa ngozi unyevu na ime dhibitishwa kikliniki kuisaidia ngozi yako kwa muda wa masaa 24. Ina bidhaa asili za colloidal oats na shea butter. Ina isaidia ngozi yako iliyo kauka na mahali ambako imeharibika. Pia haina harufu kwa hivyo ni bora kwa watu ambao hawapendi krimu zenye harufu.

The Body Shop Shea Body Butter

best creams for dark skintone

Shea butter ni chanzo asili cha vitamini na antioxidants. Watu wengi wanaipenda kwa sababu ya hamu yao ya kutoa bidhaa asili za utunzaji wa ngozi. Kwa hivyo, kwa wale ambao hawawezi tumia shea butter kwenye ngozi yao, shea body butter ndiyo kitu kikuu kijacho. Na pia ni nzuri kwa kutumiwa na watoto.

Ambi Soft & Even Creamy Oil

krimu bora kwa ngozi nyeupe

Utagundua kuwa bidhaa hii imesifiwa kwa wingi kufuatia mchanganyiko wake wa kibinafsi wa vitu asili: shea butter kwa ngozi laini na mafuta ya olive kupunguza kukauka kwa ngozi. Chapa ya Johnson & Johnson inaheshimika sana duniani kote na ina kuahidi ngozi yenye afya. Sio kwako tu, ila kwa familia yako yote.

Jergens Shea Butter Deep Conditioning Moisturizer

Krimu Bora Zaidi Kwa Ngozi Nyeupe: Kutunza Ngozi Yako Na Ya Familia Yako

Utagundua kuwa imeandikwa bila fiche kwenye chupa ya krimu hii kuwa imechanganywa na African shea butter. Jergens ni chapa ambayo ni maarufu sana hasa katika nchi ya Nigeria na imetumika kwa miaka mingi kurudisha afya ya ngozi na kuifanya ing'ae. Kwa hiyo, Jergens Shea Butter ina shinda. Pia ni bora kwani familia yako yote inaweza itumia.

Palmers Cocoa Butter Formula

krimu bora kwa ngozi nyeupe

Mbali na kuwa na harufu ya kupendeza, mafuta haya yana vitamini E. Hii ndiyo sababu kwa nini watu wengi wanaipenda, na huenda ukaipenda pia. Vitamini E huilinda ngozi yako kutokana na kupoteza hewa. Watu wengi husema kuwa wameitumia tangu wakiwa wadogo. Sio jambo jipya kuwa iko kwa orodha ya krimu za ngozi nyeupe.

Mambo 3 Unapaswa Kufanya Kila Siku Kuhakikisha Ngozi Yako Ina Afya

  •  Kusafisha. Ni muhimu kuosha ngozi yako kwa kutumia maji kila siku.
  • Kunywa maji tosha. Ngozi yako ina sehemu inayo julikana kama derma ambayo ni asilimia 70 maji na epidermis ni asilimia 15. Unapaswa kunywa maji wakati wote. Mbali na kunywa maji, unaweza hakikisha kuwa ngozi yako ina unyevu tosha kwa kutumia barakoa ya unyevu.
  • Kuipa ngozi virutubisho. Ngozi yako, kama mwili wako, mara kwa mara inahitaji virutubisho na madini. Unaisaidia sana unapo ipa virutubisho.

Chanzo: Legit NG

Soma pia: 5 Simple ways to use makeup to look younger!

Written by

Risper Nyakio