Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Njia Za Kuanzisha Kipindi Cha Hedhi Kinapo Chelewa

3 min read
Njia Za Kuanzisha Kipindi Cha Hedhi Kinapo ChelewaNjia Za Kuanzisha Kipindi Cha Hedhi Kinapo Chelewa

Kumbuka kuwa kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi huenda kuka ashiria tatizo ulilo nalo la kiafya.

Ni salama kusema kuwa wanawake hutazamia kupata vipindi vyao vya hedhi. Na vinapo chelewa, huenda wakawa na mbinu tofauti wanazo tumia kuanzisha kipindi cha hedhi.

Kuna sababu tofauti kwa nini mwanamke huenda akafanya uamuzi wa kuanzisha kipindi chake cha hedhi. Kuna njia tofauti ambazo anaweza tumia.

Sababu za kuchelewa kwa hedhi yako

  • Mawazo mengi
  • Uzani wa juu ama chini wa mwili
  • Mbinu za kupanga uzazi zilizo na homoni
  • Ugonjwa wa PCOS
  • Kisukari
  • Mimba
  • Umri wa ugumba

Hatari za kujaribu kuanzisha kipindi chako

Huenda baadhi ya vitu vinavyo tumika kukusaidia kutimiza lengo hili vika sababisha kuharibika kwa mimba.

  • Nanasi

Nanasi lina wingi wa bromelain inayo athiri homoni inayo husika na hedhi, estrogen. Ila, kumbuka kuwa hakuna utafiti dhabiti unao egemeza imani kuwa kula nanasi kwa wingi kutasaidia kupata vipindi vya hedhi.

  • Vitamini C

Njia Za Kuanzisha Kipindi Cha Hedhi Kinapo Chelewa

Hata kama hakuna ushahidi wa kisayansi kuegemeza imani hii, kuna watu wanao amini kuwa vitamini C inasaidia kutekeleza jambo hili. Ina pandisha viwango vya homoni ya estrogen huku vya progesterone vikishuka na baadaye kusababisha kipindi cha hedhi kuanza.

Vyanzo vya vitamini C ni kama vile tembe, matunda kama berries, mbogha kama broccoli, mchicha, nyanya na hata pilipili za kijani na nyekundu. Kuwa mwangalifu wa viwango unavyo vichukua.

  • Tangawizi

kuanzisha kipindi chako cha hedhi

Tangawizi ni dawa ya kale ambayo imetumika kwa muda mrefu kusababisha kubana kwa uterasi. Inatumika kwa kuchemshwa pamoja na maji, ama kutengeneza chai.

  • Manjano

kuanzisha kipindi cha hedhi

Kiungo cha manjano kinatumika katika kutengeneza rojo ama kufanya wali uwe na rangi ya manjano. Kuna imani kuwa kiungo hiki kinafanya kazi kwa kuathiri viwango vya homoni ya estrogen na progesterone. Hakikisha kuwa una kiongeza kwenye lishe yako ikiwa ungependa kuanzisha kipindi chako.

  • Kupumzika

kuwa hamasisha wanawake

Fikira nyingi huenda zikawa chanzo cha kipindi cha hedhi kuchelewa. Tunapo hisi kukwazwa kimawazo, mwili unatoa homoni ya cortisol ambayo ina athiri utoaji wa homoni zinazo husika na hedhi. Estrogen na progesterone, na zisipo tolewa, mama hawezi pata kipindi chake cha hedhi. Ni vyema kupumzika, na kuna njia tofauti ambazo unaweza tumia kufanya hivi, kama vile:

  • Punguza kazi unazo fanya
  • Hakikisha unapata wasaa wa kuwa na familia yako
  • Fanya mazoezi
  • Fanya kazi zinazo kufurahisha

Wakati wa kwenda hospitalini

Kumbuka kuwa kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi huenda kuka ashiria tatizo ulilo nalo la kiafya. Nenda hospitalini ukigundua kuwa:

  • Una shaka kuwa una mimba
  • Umekosa hedhi kwa zaidi ya miezi miwili
  • Una vuja damu baada ya kufanya ngono
  • Vipindi vya hedhi vina koma kabla ya umri wa miaka 45

Soma Pia: Je, Kwa Nini Kipindi Changu Cha Hedhi Kimechelewa? Mambo Yanayo Sababisha

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Njia Za Kuanzisha Kipindi Cha Hedhi Kinapo Chelewa
Share:
  • Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

    Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

  • Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

    Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

  • Sababu Za Kipimo Hasi Cha Mimba Bila Kuwa Mjamzito

    Sababu Za Kipimo Hasi Cha Mimba Bila Kuwa Mjamzito

  • Damu Nyepesi Katika Hedhi Ni Chanzo Cha Kiwewe Kwa Mwanamke?

    Damu Nyepesi Katika Hedhi Ni Chanzo Cha Kiwewe Kwa Mwanamke?

  • Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

    Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

  • Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

    Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

  • Sababu Za Kipimo Hasi Cha Mimba Bila Kuwa Mjamzito

    Sababu Za Kipimo Hasi Cha Mimba Bila Kuwa Mjamzito

  • Damu Nyepesi Katika Hedhi Ni Chanzo Cha Kiwewe Kwa Mwanamke?

    Damu Nyepesi Katika Hedhi Ni Chanzo Cha Kiwewe Kwa Mwanamke?

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it