Jinsi Ya Kuanzisha Tendo La Ndoa Na Mumeo Ili Kuibua Cheche Katika Ndoa Yenu

Jinsi Ya Kuanzisha Tendo La Ndoa Na Mumeo Ili Kuibua Cheche Katika Ndoa Yenu

Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa ndoa yako, kwa hivyo una hitaji kuchukua jukumu hili na kuanzisha tendo la ndoa na mumeo.

Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa ndoa yako, kwa hivyo una hitaji kuchukua jukumu hili na kuanzisha tendo la ndoa na mumeo. Mwanamme hahitajiki kufanya kazi yote wasaa wote. Jambo rahisi kama kumwonyesha hamu ya tendo hilo kwanza kunaweza leta cheche chumbani mwenu.

Kwa nini unapaswa kuweka haya chini na kujua jinsi ya kuanzisha tendo la ndoa na mumeo?

Kuna sababu nyingi kwa nini unapaswa kuchukua usukani chumbani chenu cha kulala.

  1. Kuna weza fufua maisha yenu ya kingono

Wanandoa katika ndoa zisizo na ngono wanaweza tatua hali hiyo ikiwa wote wawili wata tia juhudi katika kufufua cheche hizo. Maisha yenu ya ngono sio jukumu la mtu mmoja, kumaanisha kuwa nyote mtahitajika kufanya kazi kurejelea mlipo kuwa awali.

2. Ni njia nzuri ya kurejesha kujiamini

Juhudi unazo tia katika kuanzisha ngono zinakusaidia kuwa shupavu zaidi kuliko ulivyo dhania. Fikiria kuhusu vitu vyote vizuri utakavyo nufaika navyo unapo mfanya mumeo pia awe na hamu la tendo hilo.

3. Utakuwa na hamu ya kujaribu mambo mapya kitandani

Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa ndoa kuanzisha tendo la ndoa na mumeo.

Unapo anza kuwa na ujasiri wa kuanzisha tendo la ndoa, utapata ujasiri zaidi wa kujaribu mambo mapya kitandani pamoja na mumeo. Usiwe na hofu, jaribu mambo yote unayo yatamani.

4. Mumeo ataona kuwa unamtamani

Sio wanawake peke yao wanao taka kuhisi kuwa wanapendwa. Mumeo atapendezwa na juhudi zako za kufanya tendo la ndoa chumbani. Kwa hivyo usione haya kumjuza kuwa unamtamani na unampenda.

Jinsia ya kuanzisha tendo la ndoa na mumeo

Fikiria kuhusu ngono sana

Ikiwa unataka kufanikiwa, lazima uwe kwa mazingira sawa ili juhudi zako zifuzu. Katika wakati huo, panga vitu ambavyo ungependa kufanya na mumeo chumbani.

Usione aibu

Tunaishi katika jamii ambayo ina amini kuwa mwanamme peke yake ndiye anaye paswa kuanzisha tendo la ndoa. Lakini la, wanawake pia wana hisia kama wanaume. Kwa hivyo weka fikira hizo mbali na umfikie bwanako.

Kuanzisha ngono bila woga

Jinsi Ya Kuanzisha Tendo La Ndoa Na Mumeo Ili Kuibua Cheche Katika Ndoa Yenu

Kuanzisha ngono hakumaanishi kuwa ugeuke upande ambao mumeo ana lala. La, kuna maana kuwa umfikie, umpapase, kwa njia sawa anavyo kufikia na kukupapasa anapo taka kukutia katika hali ya kutamani tendo hilo. Usione haya kumshika, ni mumeo.

Tendo la ndoa ni kitendo kizuri kwa wanandoa. Na sio jukumu la bwana peke yake kuanzisha wakati wote. Mwanamke anapo anza, ana boresha utangamano wao na kufanya uhusiano wao kuwa bora zaidi. Kwa hivyo, chukua jukumu leo na utumie vidokezo tulivyo angazia.

Chanzo: VeryWellMind.Com

Soma piaMakosa 5 Ya Kingono Ambayo Wanaume Hufanya!

Written by

Risper Nyakio