Mbinu 5 Salama Za Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi

Mbinu 5 Salama Za Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi

Ikiwa una hisi kuwa mtoto amekawia kwa kipindi kirefu bila kufika, na siku mlio mtarajia ishafika na kupita. Ni kawaida kwa mama kuwa na shaka kuhusu mtoto kufika. Hakikisha kuwa kabla ya kujaribu mbinu yoyote ya kuanzisha uchungu wa uzazi, una wasiliana na daktari wako na uko katika wiki 39-40 za ujauzito.Tazama mbinu hizi rahisi za kuanzisha uchungu wa uzazi.

Vidokezo muhimu kwa wamama wenye mimba

kuanzisha uchungu wa uzazi

  • Tembea

Kutembea ndiyo njia maarufu zaidi inayo fahamika ya kuanzisha uchungu wa uzazi kwa wanawake. Ni maarufu kusikia mwanamke mjamzito akishauriwa kutembea ili kuanzisha kipindi chake cha uchungu wa uzazi. Kutembea kunaweza saidia kumsukuma mtoto chini kwa pelviki yako ya nne.Lakini hata kutembea kusipo anzisha uchungu wa uzazi ulivyo kusudia, juhudi zako hazikuambulia patupu. Mazoezi haya yana kutayarisha utakapo anza kujifungua.

  • Chechemua chuchu zako

Homoni ya oxytocin hutolewa mwilini chuchu zinapo chechemuliwa. Homoni hii ina weza anzisha uchungu wa uzazi inapo chechemuliwa kwa masaa 1-3 kila siku. Homoni hii ni njia kuu ya kuanza uchungu wa uzazi. Kulingana na somo moja, asilimia 40 ya walio chechemua chuchu zao kwa saa 1-3  walipata watoto wao katika kipindi cha siku tatu. Lakini, kwa mbinu zote zinazo husisha kuchechemuliwa kwa chuchu, wataalum wengi hawako makini kudhibitisha mbinu hii kuwa kamili. Hii ni kwa sababu kuna hatari ya kuchechemua chuchu zaidi. Na jambo hili linapo tendeka, huenda kubanwa kwa uchungu wa uzazi kukazidi, na kupunguza mpigo wa moyo wa fetusi.

  • Kula vyakula vyenye pilipili

Hakuna utafiti ama masomo yaliyo fanyika kuegemeza hili, lakini baadhi ya watu wana amini kuwa chakula kilicho na pilipili kina uwezo wa kumfanya mama aanze uchungu wa uzazi. Imani ni kuwa, chakula hiki kinafanya uterasi yako ianze kubana.

kuanzisha uchungu wa uzazi

  • Kufanya mapenzi

Uliza wanawake wachache na watakuambia kuwa kufanya mapenzi ndiyo mahimizo yote ambayo mtoto anahitaji ili kukuja duniani na kupatana na mamake. Mwanamke anapo fika kilele, huenda uterasi yake ikaanza kubanwa na manii ya mwanamme pia huwa na ufuta unao legeza mlango wa uke. Kwa hivyo kama hii ndiyo mbinu utakayo chagua, hakikisha kuwa umelala kwa mgongo wako ili kusaidia manii kubaki kwenye mlango wa uke.

  • Pumzika

Ikiwa una hisi kiwewe, kujaribu sana kuanzisha uchungu wa uzazi huenda kukakosa kufanikiwa. Kwa hivyo, hakikisha kuwa umepumzika na kutulia. Fanya kitu ambacho kitakufanya uhisi umetulia. Kama vile kukula kitu unacho penda ama kwenda kutazama sinema.

Soma Pia:Je, Ulifahamu? Kusukuma Katika Uchungu Wa Uzazi Kunaongeza Nafasi Za Uke Kuraruka Kwa Asilimia 700!

Written by

Risper Nyakio