Njia Sita Salama Za Kuanzisha Uzazi Peke Yako

Njia Sita Salama Za Kuanzisha Uzazi Peke Yako

There are healthy activities you can engage in to induce labour when the delivery date has come and passed.

Umewafahamisha wapendwa wako juu ya tarehe ya kujifungua. Ila, siku imeshafika na kupita na bado hauhisi kama yule mdogo wako, anajitayarisha kusema jambo kwa ulimwengu.  Iwapo una msukumo wa kumshika mtoto mikononi mwako, ama umechoka kuwa mjamzito, kuna mbinu rahisi unazoweza kutumia kuanzisha uzazi ulio salama.

Ingawaje, hutaki kuanzisha uzazi kama mtoto hayuko  tayari kutoka. Hata katika wiki za mwisho mtoto huendelea kukua. Kwa hivyo hata ukijihisi hauna starehe unafaa kungoja hadi wiki ya 39 ama ya 40 imetimia kabla ya kuanzisha uzazi. Lakini siku ya kujifungua huwa si wazi. Wakati mwingine siku yako yakujifungua  inaweza kuwa  imebadilika kwa wiki chache. Kwa hivyo iwapo utaanza kuanzisha uzazi kabla wiki ya 39 au ya 40 haijakamilika unaweza kujifungua  mtoto kabla ya wakati.

Isitoshe, mwili wako unafaa  kuwa tayari kwa mbinu zinazoweza kusababisha wewe kuwa na kubana  na kuanzisha uzazi. Ikiwa mwili wako hautakuwa tayari unaweza kuwa unajaribu bure.

Jinsi ya kuanzisha uzazi ulio salama wewe binafsi.

When to induce labour

So if you are sure you're around 40 weeks in, here are eight ways to hasten things up.

  • Chechemua chuchu zako

Wakati chuchu zinachechemuliwa, tezi za pituitari hutoa homoni oxytocin. Hii homoni ambayo husababisha maziwa kutoka  pia inaweza kusababisha kubana ambako huanzisha uzazi iwapo chuchu zitachechemuliwa  kwa kati ya saa moja hadi masaa matatu kila siku. Oxytocin ni njia mwafaka ya kuanziasha uzazi.

Kulingana na utafiti, asilimia 40 ya wale ambao walichechemua chuchu zao kwa kati ya saa moja hadi masaa matatu kila siku walijifungua watoto kati ya siku tatu ilihali asilimia 6 tu ya kundi la walio jidhibiti ndio walijifungua. Wanawake 719 waliokuwa katika wiki yao ya 37 ndio walishiriki kwenye Utafiti.

Walakini, hata kwa manufaa yote ya kuchechemua chuchu, wataalam  wengi hawazingatii mbinu hii ya kuanziasha uzazi. Hii ni kwa sababu kuna hatari ya kuchechemua  chuchu kupita kiasi. Na iwapo hii itatendeka, kubana kwaweza kuwa kwa nguvu hadi kupunguza mipigo ya moyo ya kijusi.

  • Kunywa mafuta ya mbarika au ya evening primrose.

Virutubisho kama vile mafuta ya mbarika, cohosh bluu na nyeusi, evening primrose vinaweza kusaidia kuanzisha uzazi kwa kusaidia mlango wa tumbo la uzazi kuwa mwembamba na kupanuka. Hatua hii huuandaa kwa uchungu wa kuzaa. Tembe za mafuta ya primrose zinaweza kumezwa ama kuingizwa ndani ya uke.

Lakini lazima uwe mwangalifu kwa vile kunaweza kuwa na athari au matatizo. Mafuta ya mbarika mara nyingi hutumika kuharisha na mambo yanaweza kwenda njia yoyote ile. Inaweza fanya kazi kuharakisha kuwasili kwa mtoto wako ama kusababisha maumivu ya tumbo.

Kwa bahati mbaya, jopo la majaji bado lashughulikia mbinu hii. Hakuna masomo tosha ya kueleza jinsi inavyofanya kazi

kuanzisha uzazi ulio salama

  • Fanya mapenzi

Uliza wanawake wengine na watakwambia kuwa kufanya mapenzi vizuri ilikuwa msukumo tosha kwa mtoto kutoka na kupatana na mama yake . Msisimko wakati wa mapenzi kwa mwanamke unaweza sababisha kubana kwa tumbo la uzazi na mbegu za mwanamume huwa na mafuta ambayo hulainisha mlango wa tumbo la uzazi. Hujulikana kama prostaglandins.  Kwa hivyo iwapo unatumia hii mbinu, kaa umelala chini na kiuno chako katika mwinuko ambao utasaidia mbegu zile kukaa katika mlango wa tumbo la uzazi. Kufanya mapenzi ni miongoni mwa mbinu za kuanzisha uzazi ulio salama.

  • Tembea

 

Njia za kuanzisha uzazi

Kutembea ni mojawapo ya desturi inayojulikana zaidi kati ya wanawake ya kuanzisha uzazi. Ni jambo la kawaida nchini Nigeria kumsikia mwanamke akimwambia mwenzake atembea ili kuanzisha uzazi. Kutembea tu kunaweza kusaidia kumvuta mtoto chini hadi nyonga ya nne. Kuzungushwa kwa viuno na mvuto wa graviti ndio husababisha hili. Alafu mkazo unaotokea kwa sababu ya jinsi mtoto alivyokaa katika mlango wa tumbo la uzazi inaanzisha uchungu wa kuzaa. Lakini hata kama kutembea haku taanzisha uzazi kama ulivyo tarajia, juhudi zako si bure. Zoezi hilo hukuandaa kwa wakati kujifungua kutawadia.

  • Kula chakula chenye vikolezo

Hakuna somo au ushahidi wa kusisitiza hili, lakini watu wengine huamini kuwa chakula chenye vikolezo kina uwezo wa kuanzisha uzazi. Ofe nsala(white soup) ndio pendekezo la wanawake wengi waliokomaa  kwa wale wadogo nchini Nigeria. Fikira nyuma ya hii ni kuwa chakula chenye vikolezo husababisha tumbo la mtoto kubana kwa kufanyiza matumbo kazi.

  • Jipumzishe

Kama utakuwa mwenye wasiwasi, ukijaribu sana kuanzisha uzazi kuna uwezekano haitafanya kazi. Kwa hivyo, sitawisha mazingira ya mapumziko ambapo unaweza tulia bila wasiwasi.  Fanya kitu cha kufurahisha ambacho kitakusaidia upumzike.  Nenda kuona sinema, kupodolewa ama upate aiskrimu yako uipendayo na kadhalika. Mambo haya yote yatachangia katika kuanzisha uzazi ulio salama.

 

 

Read also: Healthy Foods That Induce Labour Naturally

Written by

Risper Nyakio