Njia 5 asili za kubadili rangi ya ngozi bila kutumia kemikali

Njia 5 asili za kubadili rangi ya ngozi bila kutumia kemikali

In this article, the natural ways of skin lightening are listed for those who would like to add an extra glow to their skin with safe and natural ingredients.

Krimu za mapambo zina umaarufu nchini Nigeria kwa wale wanaotazamia kubadili rangi ya ngozi zao. Ila swali kuu ni iwapo ni salama kutumia kwani krimu hizi za kubadili rangi zimetengenezwa kutumia kemikali tofauti ambazo zinadhuru ngozi. Sio jambo la kustahabisha kuwa krimu hizi zina fanya kazi ya kiholela na kuacha sehemu zingine za ngozi zikiwa nyeusi kuliko sehemu zingine za mwili zilizo ikubali kemikali hizi za kubadili rangi. Wakati mwingine, krimu hizi huenda zika sababisha chunusi zaidi kuliko vile ulivyo kusudia. Kwa bahati njema, kuna njia asili za kubadili rangi ya ngozi bila kutumia krimu zenye kemikali.

Njia 5 asili za kubadili rangi ya ngozi bila kutumia krimu za kemikali

  1. Nyanya na chakula cha oti

Nyanya husaidia kuifanya ngozi iwe nyeupe zaidi kwa Kuondoa dosari nyeusi, kuchomeka na jua na kuanika. Ili kuitumia kuifanya ngozi iwe nyeupe zaidi, chukua juisi ya nyanya na chakula cha oti, changanya kisha utandaze kwenye uso wako. Iache kwa dakika kumi na tano kisha usafishe kutumia maji yaliyo pashwa joto au maji ya vuguvugu.

  1. Chungwa na binzari manjano

kubadili rangi ya ngozi

Vitamini C inayo patikana katika machungwa ina nguvu katika kuifanya ngozi iwe nyeupe. Ina ufanisi wa juu kiasi cha kuiboresha ngozi kufuatia kulila chungwa moja kila siku. Ila kwa kulitumia kwa kubadili rangi ya ngozi, changanya vijiko viwili vidogo vya juisi ya machungwa na finyo ya poda la binzari manjano. Jipake kwenye shingo na uso wako kabla ya kulala kisha uoshe baada ya dakika kati ya 20-30.

3. Tango na asali

kubadili rangi ya ngozi

Tishu unganishi zina jukumu la kuishikilia ngozi, misuli, mishipa na tendons. Collagen ni mojawapo ya vitu vinavyo tunga misuli unganishi. Collageni huipa ngozi muundo. Tango husaidia collageni kuimarisha ngozi yako na kisha athari ya kuituliza inayo ifanya ngozi yako kung’ara.  Kata vipande vya tango kisha uchanganye na asali na ujipake usoni. Iache kwa dakika 10-15 kabla ya kuosha uso wako kutumia maji vuguvugu.

4. Juisi ya ndimu na mlozi

Hii huenda ikiwa mojawapo ya michanganyiko unayo itazamia bila kuiamini kana kwamba aliye iandaa hakujua alicho kuwa anakiongelelea. Ila mchanganyiko huu utafanya miujiza katika kuibadili rangi ya ngozi yako. Tengeneza mlozi kwa kuponda kisha changanya na idadi kidogo ya ndimu. Ndimu ina nguvu za kubadili rangi na kufanya nyeupe. Jipake usoni mwako na shingoni kisha uache kwa muda wa dakika 10-15. Baadaye osha kutumia maji ya vuguvugu.

5. Mgando na asali

kubadili rangi ya ngozi

Viungo hivi ni rahisi kupata nchini Nigeria. Mgando katika muundo wake uliokamilika unafanana na maziwa. Kwa maana mgando unatengenezwa kutumia maziwa, una nguvu za virutubisho ambazo ni muhimu kwa ngozi yako. Ina unyevu na ajenti za kufanya nyeupe kama vile asidi ya lactic ambayo ina ufanisi wa kutoa alama kwa ngozi na kuiacha ngozi yako na mwanga asili. Iwapo una asali, ongeza kiasi kwa mgando kabla kupaka kwenye uso na shingo. Itandaze kwa ngozi na uiache itulie kwa muda usio pungua dakika 15 kabla ya kuosha na maji ya vuguvugu. Njia nyingine ni kujipaka mgando na kuacha ubaki dakika 15 kabla kuosha uso.

Hitimisho

Ni muhimu kuwa makini na kuzingatia njia yoyote ile utakayo amua kuitumia. Ila ngozi yako isipo kubaliana na njia hiyo, iwache na ujaribu njia nyingine.

 

Read more: Five Reasons Your Facial Skin Isn’t As Beautiful As It Should Be

Source: Web MD

Written by

Risper Nyakio