Mwezi wa Disemba umewadia ambapo wengine wetu wanapenda kusafiri sana mahali tofauti. Lakini wakati unapo usafiri wa barabarani una fahamika kwa ajali na kukwazwa kimawazo, hakuna njia kwa nini haupaswi kuifurahia safari yako ijayo. Hapa kuna baadhi ya vidokezo vya kukusaidia kubaki na afya unapo safiri barabarani.
Lakini, mtu atawezaje kutimiza hili hasa wakati ambapo kuna uwezekano wa ajali za barabarani, maafisa wanao itisha pesa nyingi na uwezekano wa gari lililo kando yenu na kelele nyingi ama wageni msio juana.
Kumbuka kuwa 'afya ni mali' na wakati wa safari ya barabarani, kuwa makini na afya yako ni muhimu kama kuwatembelea jamii wako wakati wa likizo hizi.
Katika hatua tano, hapa kuna baadhi ya mapendekezo ya kukusaidia kubaki na afya unapo safiri barabarani.
- Tayarisha chakula na vitamu tamu vyako

Huku kuna maanisha kuwa hakuna mama pima ama kununua kwa wauza barabarani. Unataka kuhakikisha kuwa wakati wote wa safari hii, unakula chakula chenye afya na kilicho salama kwa sababu itakuwa ajali mbaya kuanza kuumwa na tumbo wakati wa safari hii; ama safari yoyote ile.
Kuhakikisha kuwa unacho kula wakati wa safari ni salama, weka baadhi ya vitamu tamu, na uweke chakula kwenye kifaa cha kuhifadhi chakula baridi.
Sio vibaya kununua matunda ama njugu kutoka kwa wauza barabarani, ili kumbuka kuyaosha vyema kabla ya kula.
Pia, unaweza beba vitamu tamu ambavyo vina dumu kwa muda na vinaweza baki freshi hadi kwa masaa sita.

Utakuwa mahali palipo fungwa kwa masaa mengi. Ni kawaida kupata joto jingi, kuumwa na kichwa ama kukwazwa kimawazo.
Maji peke yake hayata kata kiu chako lakini pia yatasaidia kupunguza maumivu ya kichwa.
Kumbuka kuwa makini na kiwango cha maji unacho kunywa ikiwa una kibofu kidogo. Hautaki kuwa msafiri mbaya anaye msihi dereva asimamishe gari mara kwa mara aende haja ndogo.
- Nyoosha mwili wako mnapo simama
Kuwa mahali pamoja kuna chokesha bila shaka na huenda mifupa yako ikaganda.
Hakikisha kunyoosha mikono yako, miguu, mabega, mgongo na miguu mnapo simama. Kwa njia hii, una uanzia tena mfumo wako wa kuzungusha damu mwilini. Ni kidokezo muhimu cha kubaki na afya unapo safiri barabarani.
- Epuka vyoo vya uma visivyo takaswa
Usiwe na pupa ya kwenda choo chochote kilicho karibu nawe. Watu wameugua maambukizi hatari baada ya kutumia choo katika hali sawa.
Badala yake, angalia njia mbadala kama vile kutumia kiwanja wazi (ambacho huwenda kikawa salama zaidi kuliko choo cha uma).

Kuenda safarini sio jisababu ya kufanya seli za ubongo wako zife. Soma kitabu, ama makala kwenye simu ama hata gazetti, anzisha mjadala wa ushupavu, pumzika ama hata uangalie video kwenye mtandao.
Chochote unacho fanya, epuka kufanya ubongo wako ubaki bila kufanya chochote.
Soma Pia: Sababu 7 Za Kuwa Hamasisha Wanawake Kwenye Jamii