Mwanamme anapotoa idadi ndogo ya manii kuliko ilivyo kawaida, huenda akawa na matatizo ya uzalishaji. Kuna mambo kadhaa yanayoathiri uwezo wa uzalishaji wa mwanamme. Tuna angazia jinsi ya kuboresha afya ya manii katika wanaume.
Idadi na ubora wa manii

Wanaume wanavyozidi kuzeeka, ndivyo idadi na ubora wa manii yao unavyozidi kupunguka. Kuna sababu nyingi zinazomfanya mwanamme kuwa na manii yasiyo na ubora. Kama vile kupunguka kwa testosterone kadri mwanamme anavyozidi kuzeeka. Mishipa inayosafirisha manii inapoziba, inafanya iwe vigumu kwa mwanamme kumwaga katika kitendo cha ndoa.
Sababu zinazoathiri ubora wa manii ni kama vile magonjwa ya kingono kama vile kisonono, matibabu hasa yanayolenga prostate gland, shinikizo la damu la juu, kusombwa na mawazo na kisukari.
Uzalishaji katika wanaume unahusiana na afya ya manii na unyevunyevu wa semina. Maji ya semina huwa na manii na virutubisho vingine vinavyo athiri ubora wa manii na uwezo wa kuzalisha mtoto. Uwezo wa kusonga katika manii ni ishara chanya ya uzalishaji.
Tatizo la kutoshaliza katika wanaume husababishwa na mambo kama; utoaji wa idadi ndogo ya manii, manii kushindwa na mwendo, maumbile duni ya manii, mishipa inayosafirisha manii kuziba, magonjwa, uzee kuingia na kadhalika. Wanaume wanapozidi kuzeeka, idadi na ubora wa manii wanayotoa hupunguka, hasa wanapofika umri wa miaka 40.
Jinsi ya kuongeza idadi ya manii

Mfumo wa maisha ambayo mwanamme anaishi unachangia pakubwa katika afya yake ya kijumla na ubora wa manii.
Lishe, ni muhimu kwa mwanamme kuhakikisha kuwa chakula anachokiongeza mwilini. Na kuhakikisha kuwa wakati wote chakula chake kinaongeza virutubisho mwilini. Vyakula kama, maharagwe, samaki, mayai, nyama na viazi.
Mazoezi, yanasaidia katika kuzibua mishipa ambayo huenda ikawa imeziba na kusaidia katika usafirishaji wa manii mwilini.
Kupunguza utumiaji wa vileo. Vileo vina athiri idadi na manii yanayotolewa mwilini. Hasa kwa wanandoa wanaojaribu kutunga mimba, ni vyema kukoma kutumia vileo ili kuboresha manii yanayo tolewa mwilini.
Ni vyema wanaume kujitenga na hali za anga zilizo na joto ya kupindukia kwani zinapunguza ubora wa manii yao.
Kwa wanandoa walio katika harakati zao za kutunga mimba, ni vyema kuwasiliana na mtaalum wa afya na kufanyiwa vipimo kudhibitisha iwapo wana matatizo yoyote na kupata maarifa jinsi ya kuboresha afya ya manii.
Soma Pia: Vidokezo Vya Kukusaidia Kujua Ikiwa Manii Yana Afya Kwa Kuangalia