Tatizo la ashiki ya chini mara nyingi husababishwa na hali kama kuwa na mawazo mengi, kuwa na matatizo ya kiafya, umri mwingi ama matatizo katika ndoa na uhusiano. Tunaangazia njia tofauti za kuboresha ashiki.
Jinsi ya kuboresha ashiki

1.Kuboresha ubora wa uhusiano
Watu wengi hushuhudia punguko la kufanya mapenzi na wachumba wao katika kipindi kimoja katika uhusiano wao. Hasa baada ya kuwa katika uhusiano kwa kipindi kirefu. Wachumba wanaweza fanya uamuzi wa kuboresha uhusiano na urafiki wao kwa, kuzuru mahali tofauti, kwenda date nights mara kwa mara, kuwa na mazungumzo wazi na kutenga wakati hasa wa kuwa pamoja.
2. Pata usingizi tosha
Usingizi bora husaidia kuimarisha mhemko na viwango vya nishati. Kwa wanawake, kupata usingizi bora husaidia kuongeza viwango vya ashiki.
3. Kupunguza wasiwasi na mawazo mengi
Mawazo mengi huziba kufikiria na kujitayarisha kuwa na kipindi cha kufanya mapenzi na mchumba wako. Huenda wasiwasi ukasababishwa na uhusiano wa kimapenzi, kazi, kukosa pesa ama kuwa na majukumu mengi maishani. Wanaume walio na mawazo mengi huenda wakatatizika kusimamisha kibofu kwa muda wanapofanya mapenzi.
Kujaribu mambo haya kunaweza kupunguza wasiwasi. Kufanya mazoezi, kula chakula bora, kuwa na ratiba ya kulala na kuzungumza na mtaalum.
4. Kula chakula bora
Kuzingatia lishe bora na yenye afya kuna faida nyingi kwa watu wanaotatizika na ashiki ya chini. Huboresha mzunguko wa damu mwilini. Ni muhimu kuepuka vyakula vinavyopunguza ashiki. Vyakula kama protini na mboga ni bora katika kusaidia na ashiki.
5. Kufanya mazoezi

Kufanya mazoezi mara kwa mara kuna saidia kuongeza viwango vya libido mwilini. Kufanya mazoezi husaidia kwa kuongeza viwango vya ashiki. Pia yanasaidia kuwa na mwili bora wenye nguvu na kupunguza mawazo mengi.
6. Uzito wa wastani
Baadhi ya utafiti huhusisha uzito mwingi wa mwili na kuwa na ashiki ya chini. Kuwa na uzito mzuri kulingana na mwili wako husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi na viwango vya nishati.
7. Kukoma kuvuta sigara
Uvutaji wa sigara huwa na athari hasi kwa mfumo wa cardiovascular. Kuwa na moyo wenye afya ni muhimu katika kufanya mapenzi vyema. Watu wanaovuta sigara huwa na viwango vya chini vya nishati na mara nyingi huenda wakakosa hamu ya kufanya mapenzi.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Je, Kuna Madhara Hasi Ya Kufanya Mapenzi Katika Mimba Kwa Mama Mjamzito