Hongera!Umefanya uamuzi wa kupata mtoto! Haijalishi ikiwa ni kifungua mimba ama kitinda mimba chako unachotarajia kupata. Vidokezo hivi vya jinsi ya kuboresha mfumo wa uzazi wa mwanamke kabla ya kutunga mimba vinapaswa kuzingatiwa kila mara mama anapoamua kuwa mjamzito. Ni vigumu kubaini wakati hasa ambao mwanamke atachukua kushika mimba. Lakini kwa kuzingatia vidokezo hivi, anaongeza nafasi zake za kushika mimba kwa kasi. Soma zaidi!
- Lishe ya uzalishaji

Chakula huchangia pakubwa katika afya ya kujumla na ya kizazi pia. Chagua vyakula kama mboga za majani, protini laini, na parachichi. Kula vyakula bora kunasaidia kuboresha afya jumla na kutatua matatizo kwenye mfumo wa uzazi. Chakula kinasaidia katika uzalishaji wa mayai mwilini mwa mwanamke.
Punguza unywaji wa kahawa nyingi, na vyakula vya barabarani vilivyopikwa kutumia mafuta nyingi. Badala yake, kunywa maziwa ya bururu, samaki na ndizi mbivu.
2. Koma kutumia pombe na sigara

Sigara ina nicotine iliyo na athari hasi katika mfumo wa uzazi, inafanya iwe vigumu kwa mwanamke kupevusha yai anapotakikana. Pombe ina athiri nafasi za wanandoa kushika mimba kwa kasi. Mwanamke anapaswa akome kutumia vileo miezi 3 hadi 6 kabla ya kuanza juhudi za kutunga mimba. Vileo kwa wanaume vinapunguza idadi na ubora wa manii anayotoa.
Kutumia vileo baada ya kutunga mimba kuna athiri ukuaji wa fetusi na mtoto huenda akazaliwa akiwa na uzani wa chini wa mwili ama akiwa na matatizo ya kimaumbile.
3. Uzito wa mwili wenye afya

Mwanamke anapokuwa na uzito wa kupindukia ama uzito wa chini wa mwili, mara nyingi, atatizika kushika mimba. Viwango vya homoni mwilini haviko sawa na kumfanya kupata hedhi isiyo ya kawaida. Ili kuboresha uwezo wa kutunga mimba kwa kasi na kwa urahisi, ni vyema kwa mwanamke kuhakikisha kuwa ana uzito unaomfaa kulingana na urefu wake. Hata hivyo, wanawake walio na uzani wa chini ama wa kupindukia bado hutunga mimba kwa nafasi sawa na walio na uzani wa wastani.
4. Chukua vitamini za kabla ya kujifungua

Vitamini za prenatal ni muhimu katika kujifungua mtoto mwenye afya. Mama anaweza anza kutumia vitamini hizi kabla na kutunga mimba na kuendelea anaposhika mimba. Zinasaidia fetusi kupata mahitaji na kuboresha ukuaji wake.
5. Punguza mawazo

Ni vigumu kujitenga na mawazo mengi kadri unavyozidi kukua. Masomo, familia, kazi na gharama ya maisha zinawafanya watu kuwa na mawazo tele. Kusombwa na mawazo hufanya iwe vigumu kwa mama kushika mimba kwa urahisi. Ni vyema kwa mama kutafuta njia za kupunguza mawazo haya. Kwa kufanya mazoezi, kusikiza muziki, kuzungumza na mtaalum ama hata kujaribu meditation.
Mbali na kuzingatia vidokezo hivi vya kuboresha mfumo wa uzazi wa mwanamke, ni muhimu kwa mwanamke kuhakikisha kuwa anachukua maji tosha kwa siku. Kuwasiliana na mtaalum wa mambo ya uzazi, kufahamu mzunguko wake wa hedhi na siku anapokuwa na nafasi zaidi za kutunga mimba na kujikakamua na kitendo cha wanandoa.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Ishara 4 Zinazodhihirisha Kuwa Mama Ana Ujauzito Wenye Afya