Jinsi Ya Kuwa Na Utangamano Wa Karibu Zaidi Na Watoto Wako

Jinsi Ya Kuwa Na Utangamano Wa Karibu Zaidi Na Watoto Wako

Boresha utangamano na watoto wako kwa kufuata sharti hili la dakika tatu kila siku!

Unapofikiria kuhusu mambo ya kuhimiza utangamano kati ya mtoto na mzazi, huenda ukafikiria kuhusu masaa mengi ya kucheza pamoja ama kula lishe pamoja na watoto wako. Bila shaka kutengeneza utangamano kati ya mtoto na mzazi ni muhimu katika viwango tofauti: mapenzi, usalama na mazungumzo ni chache kati ya utangamano unao tengenezwa.

Na hata kama kucheza pamoja na wakati wa lishe ni muhimu, wana saikolojia wanasema kuwa utangamano kati ya mzazi na mtoto kunaweza fanyika katika muda mfupi kama dakika tatu. Je, umesikia kuhusu sharti la dakika tatu?

utangamano kati ya mzazi na mtoto

Sharti la dakika tatu kulingana na wana saikolojia

Kama wazazi, mara kwa mara tuna kazi nyingi, haijalishi ama ni kuwatunza watoto wetu ama kutafuta pesa. Mara nyingi, yote haya mawili... na mengine mengi.

Ikiwa tunafanya kazi, tuna muda mdogo sana wa kuwa na watoto wetu. Tunapo pata wakati wa kuwa nao, akili zetu ziko hapo kweli? Kuna kitu tunacho kosa kweli?

Huenda kukawa nalo - na huenda ikawa sehemu muhimu zaidi ya siku yako.

Kulingana na mwana saikolojia Nataliya Sirotich, mkuu wa Kituo cha Kazi na Watoto na Vijana, kuna sharti la dakika 3 muhimu ambazo sio wazazi wengi hufanya na watoto wao.

Sharti hilo la dakika 3 linasema kuwa unapo rudi nyumbani, uwe makini na mtoto wako kwa angalau dakika 3. Na unapaswa kufanya hivi bila kukosa, kila siku.

Ni jambo rahisi ila lenye manufaa na linalo saidia kuboresha uhusiano wa familia. Kwa kufuata sharti hili, Sirotich anasema kuwa mtoto ana fahamu jinsi ya kuhisi salama na wazazi wake. Imani ya mtoto huenda ikaendelea kuongeza hadi wanapokuwa vijana wa makamu.

Mama na baba, hili huenda likatumika iwapo umetoka nje ya nyumba kufanya majukumu kwa mfano ya kazi mtaa mwingine.

Mambo ya kufanya ya kuboresha utangamano kati ya mzazi na mtoto: Jinsi ya dhibiti dakika hizi 3 vizuri

Sio kutumia dakika tatu tu na mtoto wako. Kuna baadhi ya vitu muhimu vya kufahamu kwanza.

1. Hakikisha kuwa mnaangaliana kwa urefu sawa

Unapo tumia dakika hizi tatu na mtoto wako, hakikisha kuwa mko kuwa mnaangaliana kwa urefu sawa. Ikiwa mtoto wako ni mfupi, unaweza chuchumaa ama mkae kwenye kiti ili mtoshane.

Pia mnaweza kaa kwenye sakafu pamoja, kuangaliana kwa macho ni muhimu.

2. Angazia sharti hili unapo mchukua mtoto wako kutoka shuleni

Hii ni muhimu sana unapo wachukua kutoka shuleni hasa katika darasa la chekechea. Imekuwa wakati mrefu tangu muonane nao, kwa hivyo mbona usitumie dakika tatu nao: wakumbatie na uwaulize kwa upole jinsi siku yao ilivyokuwa shuleni na walicho fanya.

Usipuuze umuhimu wa kuwa na mazungumzo machache hapa kwa sababu mtoto wako huenda akahisi kana kwamba hasikizwi usipo wapa masikio yako. Mazungumzo mnayo kuwa nayo hapa ni muhimu sana kwao.

Mtoto wako mchanga ana furaha sana na ana hamu ya kukuelezea anacho fikiria na kilicho akilini mwake anapo kuona, kulingana na Sirotich. Wewe ndiye rafiki yake mkubwa!

Kumbuka: Fuata wanacho kwambia kwa kuuliza maswali hasa kuhusu wanacho kuambia. Usiwahi wapuuza.

3. Unacho hitajika kutowahi fanya

Haupaswi kupuuza kuwa makini kwa watoto wako kwa dakika tatu baada ya kipindi kirefu bila ya kuwaona. Usipo watazamia watoto wako muda wako, huenda wakaanza kupuuza umuhimu wa wanacho kipitia kila siku.

 Huenda wakadhani kuwa hauna hamu ya kujua kuwahusu na katika siku za usoni, huenda wakakua na kujiwekea vitu na kukosa kukwambia chochote.

3. Bila shaka usichukue maana ya juu

Sharti la dakika 3 lina maana ya kufanya juhudi zaidi za kuwa na wakati angalau dakika tatu na kuwa makini kwa mtoto wako, ili wakueleza mambo muhimu zaidi punde tu wanapo kuona.

utangamano kati ya mzazi na mtotoMatendo ya kuboresha utangamano kati ya mzazi na mtoto

Kuna vitu vingine ambavyo unaweza fanya ili kuwa na wakati zaidi na utangamano wa karibu na mtoto wako kulingana na wana saikolojia.

1. Fanya vitu mnavyo pendelea nyote

Jambo la muhimu hapa ni kuwajulisha kuwa una hamu ya kuwa na wakati pamoja nao na kufanya mambo kwa pamoja. Huenda likawa jambo rahisi kama kucheza mchezo ama kutengeneza vitu!

Katika wakati huu, kuwa makini kwao na kuwa nao. Vitu vingine vyote vinaweza ngoja.

2. Kuwajulisha watoto wako kuwa wanaweza kuongelesha wakati wote na kukuamini

Mama na baba, ni muhimu kuwasikiza watoto kwa makini mnapo kuwa mkizungumza nao.

Mbali na kusikiza wanacho kuambia tu, mtoto wako anahitaji kujua kuwa umeelewa anacho kwambia vizuri. Huku kuta kunufaisha vipi kwa muda mrefu ujao?

Watakua wakielewa umuhimu wako kama chombo cha amri na mahali penye mapenzi na kuegemezwa. Pia unaweza kuwa na uhakika kuwa watakuja kwako iwapo wana kitu chochote cha kusema. Cha zaidi, unaweza tarajia kuwa tabia hii itaendelea hadi wawe vijana.

sifa za mwanamme mwema

3. Kuwa mkweli, usilazimishe kicheko

Baadhi ya wakati, huenda ukakosa kuelewa kitu chochote ambacho mtoto wako anakuambia.

Katika jaribio lako la kumwitikia mtoto wako inavyo faa, jambo muhimu ni kuwa mkweli wakati wote. Watoto wana maarifa zaidi ya unavyo dhani. Na baadhi yao huweza wakajua unapo jilazimisha.

Kumbuka: Pitia mazungumzo mliyo kuwa nayo, kwani yana mhakikishia kuwa umesikiza na ukaelewa alicho kisema.

Athari za kumpuuza mtoto wako

Haimaanishi kuwa usipo zingatia sharti la dakika tatu, kuwa unampuuza mtoto wako. Lakini kuto zingatia sharti hili huenda kukaonekana kwa njia zingine mtoto wako anapo zidi kukomaa.

  • Kukuza tabia ya kujifungia - huenda mtoto wako aka jikunja kwa sehemu yake
  • Unaonekana kuto kuwa nao wanapo kuhitaji na wanapo zeeka zaidi, watapata sababu chache za kuongea nawe
  • Huenda wakawa hawana hamu ya kukujuza kuhusu mambo muhimu yanayo tokea maishani mwao

Manufaa ya kuwasikiza watoto wako kwa makini wanapo kuongelesha yana dumu. Jambo muhimu ni kufanya hivi wakati wote na kuwaonyesha watoto wako kuwa uko nao katika kila hatua ya maisha yao.

Chanzo: ZepthaAmerican Psychological Association

Soma pia: Vidokezo Vya Kuwa Mama Mwema Kwa Watoto Wako: Sifa 5 Za Mama Mwema

Written by

Risper Nyakio