Matunda 8 Ya Kula Unapo Nyonyesha Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama

Matunda 8 Ya Kula Unapo Nyonyesha Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama

Parachichi zina wingi wa asidi ya folic, vitamini C, E na potassium zinazo msaidia mtoto wako kukua na kuendelea inavyo faa. Tunda hili linakusaidia kusawazisha viwango vyako vya kolesteroli na kisukari.

Unapokuwa ukinyonyesha, lishe yako huwa muhimu sana katika kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata virutubisho tosha. Ni bora zaidi kama unaweza kula vyakula vinavyo boresha utoaji wa maziwa ya mama(vyakula kama hivi vina fahamika kama galactagogues), ama kuboresha ubora. Hata kama huenda ukahitajika kujitenga na nambari ya vitu, kitu pekee ambacho unaweza kula ni vitamu tamu. Ikiwa unapenda kula matunda, angalia orodha yetu ya matunda matamu ambayo yana manufaa kwa wamama wanao nyonyesha.

Matunda 6 ya kula unapo nyonyesha kuboresha utoaji wa maziwa ya mama

1.Papai za kijani

Naam, sio papai tu. Papai za kijani ni mojawapo ya matunda bora zaidi ambayo unaweza kula unapo nyonyesha hata kama sio bora kwako ukiwa na mimba.

Ikiwa unashangaa papai la kijani ni lipi? Ni papai la kawaida ambalo halija iva bado. Ni agenti inayo kusaidia na kunyonyesha kwa kuboresha utoaji wa homoni ya oxytocin na hivyo kuongeza maziwa yako. Papai la kijani pia huwa na uwingi wa vitamini muhimu kama vile vitamini A, B,C na E.

2. Parachichi

kuboresha utoaji wa maziwa ya mama

Tunda hili kuu lina faida nyingi na mojawapo ya faida hizi ni kusaidia na maziwa ya mama. Lina wingi wa omega-3 fatty acids, omega-6, omega 9 na litakusaidia kutoa maziwa yenye virutubisho vingi ya mtoto wako.

Parachichi zina wingi wa asidi ya folic, vitamini C, E na potassium zinazo msaidia mtoto wako kukua na kuendelea inavyo faa. Tunda hili linakusaidia kusawazisha viwango vyako vya kolesteroli na kisukari.

3. Strawberries

Matunda haya hayana ladha tu, mbali yana virutubisho vingi ambavyo mtoto wako mchanga atahitaji katika ukuaji. Tunda hili lina iron nyingi na vitamini C, kalisi, potassium na magnesium. Pia lina kiwango cha juu cha maji kinacho kusaidia kuwa na maji tosha unapo mnyonyesha mtoto.

4. Mandizi

matunda salama kwa mjamzito

Ni vigumu kuto kula mandizi. Yana ladha na pia vitamini na madini muhimu. Ni tunda linalokuwa na kalori nyingi na litakusaidia kupunguza kuhisi njaa unapokuwa ukinyonyesha na linakusaidia na viwango vyako vya asidi ya folic.

5. Blueberries

Yana fahamika sana kwa kuwa antioxidant. Wakati ambapo kiwango kinacho pita kwa mtoto wako hakijulikani, inafahamika kuwa antioxidants humfikia mtoto wako kupitia kwa maziwa ya mama. Pia yana vitamini, madini kama vitamini A na K, kalisi na potassium.

Ila, ni vyema kudhibiti viwango vya matunda haya kwani yanaweza sababisha mtoto kuwa na gesi.

6. Maembe

Maembe yana antioxidants nyingi na vitamini K. Fiber na potassium iliyoko kwenye matunda haya pia inasaidia mama anaye nyonyesha kuongeza virutubisho mwilini.

Kwa sasa kwani unafahamu matunda unayo hitaji unapo nyonyesha. Ni vyema kupata maarifa kuhusu matunda unayo paswa kuepuka ukinyonyesha.

Matunda ya kuepuka unapo nyonyesha:

1. Machungwa, kiwi, nanasi, ndimu, limau na grapefruit

Matunda yaliyo na kiwango cha juu cha citric acid ambayo inaweza sumbua mwendo wa tumbo wa mtoto na mfumo wake wa kummeng'enya chakula. Hata watu wazima wanashindwa na viwango vya juu vya citric acid, mbona mtoto asilemewe?

2. Prunes na cherries

Matunda haya yana shauriwa wakati wowote unapo taabika kwenda msalani. Kula viwango vikubwa vya matunda haya kunaweza athiri mfumo wa kummeng'enya chakula wa mtoto wako. Na kukufanya ukimbie msalani kila mara, sio nzuri kwako kwa sababu unahitaji kuwa na maji tosha mwilini unapo nyonyesha.

Ni matumaini yetu kuwa orodha yetu ya matunda ya kuboresha utoaji wa maziwa ya mama na matunda ya kuepuka unapo nyonyesha imekusaidia!

Vyanzo: WebMD

Livestrong

Soma piaLishe Ya Ujauzito: Ratiba Ya Chakula Cha Ujauzito Cha Nigeria

Written by

Risper Nyakio