Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

Una shaka kuhusu kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi hata ingawa hauna mimba? Kuchelewa ama kukosa kipindi chako cha hedhi husababishwa na sababu tofauti mbali na ujauzito. Sababu maarufu zikiwa kama vile mabadiliko ya homoni mwilini ama matatizo sugu ya kiafya.

Mbali na sababu hizi mbili, wakati mwingine ambapo ni sawa kwa mwanamke kushuhudia kipindi cha hedhi kisicho cha kawaida, ni anapo anza kupata vipindi vya hedhi, ama umri wa ugumba unapo anza. Kwa kawaida mzunguko wa kipindi cha hedhi huwa siku 28, kwa wengine ikiwa kati ya siku 21 hadi 35. Ukikosa kushuhudia kipindi chako cha hedhi, huenda ikawa ni kufuatia mambo haya.

Sababu kuu za kuchelewa kwa kipindi cha hedhi

kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi

  • Fikira nyingi

Kuwa na mawazo mengi kunaweza athiri homoni zako, kubadili utendaji kazi wako wa kila siku na hata kuathiri sehemu ya ubongo inayo husika na kudhibiti kipindi chako cha hedhi. Baada ya kipindi cha wakati, mawazo mengi yanaweza sababisha magonjwa ama kupoteza uzito kwa kasi na kuathiri kipindi chako cha hedhi.

Ikiwa una shaka kuwa fikira nyingi zina athiri hedhi yako, jaribu kuongeza mazoezi katika shughuli zako za kila siku.

  • Uzani mdogo wa mwili

Wanawake wanao tatizika kula huenda waka shuhudia kukosa hedhi. Ikiwa una tatizo hili, ni vyema kupata matibabu ili uweze kuongeza kilo kwa njia inayofaa na yenye afya na ili kipindi chako kirudi kiwe cha kawaida.

  •  Mbinu za kupanga uzazi

kuchelewa kwa kipindi cha hedhi

Kuna aina tofauti za mbinu za kupanga uzazi. Zilizo na homoni huenda zika sababisha mabadiliko mengi mwilini kama vile kuchelewa ama kukosa kushuhudia kipindi chako cha hedhi. Na hata baada ya kuacha kutumia mbinu hiyo, huenda ikachukua muda zaidi ya miezi mitano ili vipindi vyako viwe sawa kama mbeleni.

  •  Uzito mwingi wa mwili

Kuwa na uzito mwingi wa mwili kunaweza sababisha mabadiliko katika viwango vya homoni mwilini. Ikiwa una tatizika na uzito mwingi wa mwili, ni vyema kufanya mazoezi na kubadili lishe yako kwani huenda ikawa ndiyo sababu kuu inayo athiri kuchelewa kwa hedhi yako.

  •  Maradhi sugu

Magonjwa kama vile kisukari huenda yaka athiri vipindi vya hedhi vya mwanadada. Mabadiliko katika viwango vya sukari kwenye damu kume husishwa na mabadiliko ya homoni na mwishowe kuathiri vipindi vyako vya hedhi.

Soma PiaNjia Bora Zaidi Za Kudhibiti Uzalishaji Kwa Mama Anaye Nyonyesha

Written by

Risper Nyakio