Ulezi sio jukumu rahisi. Mara nyingi, huenda mzazi akahisi kuwa amechoka kihisia, kiakili na kifizikia kufuatia ulezi. Mzazi anapofanya hivi, mara nyingi atajipata akijitenga na watoto wake na marafiki wa karibu. Mzazi anaye tatizika na hali ya kuchoka katika ulezi huenda akasahau vitu, kupuuza majukumu yake ama kufilisika kimawazo.
Mzazi anapokuwa na shaka nyingi kuhusu kutekeleza mahitaji ya watoto wake, huenda akapata tatizo hili. Hasa kufuatia janga la Covid-19 ambapo watu wengi wamesimamishwa makazi zao, huku wengine wakipata mapato yaliyo punguka na hayatoshi kukimu mahitaji yao. Ni kawaida kwa mzazi kuwa na shaka na wasiwasi kuhusu karo ya shule na chakula cha familia yake.
Ishara za kuchoka katika ulezi

- Uchovu, kuhisi hauna nguvu kila wakati
- Kujitenga na watu wengine
- Kuumwa na kichwa wakati wote
- Kukosa motisha
- Kukasirika ovyo
- Kuhisi kana kwamba uko peke yako duniani
Wazazi wanaohisi uchovu huenda wakajipata wakitumia mihadarati na vileo, ili kujituliza akili.
Jinsi ya kukabiliana na tatizo hili
Matatizo mengi hupunguka na kusuluhishwa kwa mazungumzo. Kuzungumza na mchumba wako ni hatua ya kwanza kubwa. Kuwa wazi katika mazungumzo yako na umweleze unachokipitia. Usiwe na hofu kuwa ataona kana kwamba hufurahii kuwa mzazi. Nafasi kubwa ni kuwa utasikiliza na kukusaidia na baadhi ya majukumu ya nyumbani.
Kutopata usingizi na mapumziko tosha huwa na athari hasi kwa afya. Hata kama una kazi inayochukua masaa mengi na kisha kuwa na majukumu zaidi ya kinyumbani, ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata wakati tosha wa kupumzika. Kulala kwa masaa manane kwa siku kunaimarisha afya yako ya kiakili.

Mazoezi husaidia katika kupunguza mawazo mengi, kwa hivyo kufanya mazoezi kwa dakika chache kila siku kutapunguza hisia za uchovu kwa walezi.
- Kuwa na marafiki wa kukuegemeza
Kuwa katika vikundi vya wazazi ni njia bora ya kuwa miongoni mwa watu walio na majukumu sawa nawewe. Kuzungumza nao kuhusu matatizo unayoyapitia kutakusaidia kuhisi kuwa una sikilizwa na maoni yako ni muhimu.
Kuwa mzazi ni hatua moja ya maisha na wala sio jukumu la kipekee. Ni kwa hivyo ni vyema kwa wazazi kuzidi kufanya mambo waliyopendelea kufanya hapo awali na kujitunza. Kumbuka kuwa mzazi asiye jitunza itakuwa vigumu kwake kutunza watoto na familia yake. Hakikisha unajipenda kwanza na kuitunza afya yako ya kihisia, kiakili na kifizikia.
Soma Pia: Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?