Kwa Nini Vyakula Unavyo Vipenda Vinakufanya Kuhisi Kutapika Ukiwa Na Mimba?

Kwa Nini Vyakula Unavyo Vipenda Vinakufanya Kuhisi Kutapika Ukiwa Na Mimba?

Ni vyema kuhakikisha kuwa hauchukii chakula fulani kisha kukosa virutubisho fulani mwilini. Ikiwa una kosa virutubisho fulani usipo kula chukula kama vile samaki, unaweza nunua supplements.

Kipindi ambacho mwanamke huwa na mimba huwa mojawapo ya vipindi vya kufurahisha zaidi na kumjaza na matamanio ya kuitwa mama. Ila, kipindi hiki huja na changamoto zake. Kama vile hamu ya kula vyakula vingi huku ukichukia vyakula ulivyo vipenda hapo awali. Huku ukitamani kula vitu kama vile vibanzi na tikiti maji, huenda ukachukia vyakula ulivyo penda kuvila sana hapo awali. Ikiwa ulipenda kuanzia siku yako na kahawa hapo awali, kila siku kabla ya kufanya kazi zako, nafasi kubwa ni kuwa harufu ya kahawa itakufanya uhisi kutapika. Kipi kinacho sababisha kuchukia vyakula katika mimba?

Sababu Za Kuchukia Vyakula Katika Mimba

 

kuchukia vyakula katika mimba

Ni jambo maarufu kwa wamama walio na mimba kuchukia moja wapo ama zaidi ya vyakula walivyo vipenda hapo awali. Kila mama huwa tofauti na chakula ambacho mama mmoja atapenda huenda mwingine akakichukia. Kuna uwezekano mkubwa wa kuchukia vyakula kama vile nyama, mayai, na pilipili kwa chakula.

Ikiwa unashuhudia kuchukia chakula huku katika mimba, huenda ukawa una shuhudia ugonjwa wa asubuhi, kichefu chefu ama hata kutapika. Na sio wakati wa asubuhi tu, hata siku nzima. Utashuhudia mambo haya sana sana katika trimesta ya kwanza. Kuwa tayari kwani unaweza shuhudia haya miezi yote tisa hadi pale utakapo jifungua. Chanzo cha matamanio ya chakula katika mimba na kichefu chefu bado hakija dhihirika. Lakini kulingana na wataalum, huenda ikawa ni kufuatia mabadiliko ya homoni ya HCG (human chorionic gonadotrophin) mwilini katika kipindi hiki cha ujauzito.

Kulingana na Anjali Kaimal ambaye ni mkurugenzi mkuu wa matibabu ya mama na fetusi katika hospitali kuu ya Massachusetts huko Boston, viwango vya HCG mwilini huwa vingi zaidi katika trimesta ya kwanza, kisha vinaanza kudidimia. Wanawake wajawazito huwa na ongezeko la uwezo wao wa kunusa na kuonja. Kitu chochote chenye harufu kali huenda kikawafanya wahisi kutapika. Wanawake wengine hushindwa kula kabisa. Huku pia kuna husishwa na mabadiliko ya homoni mwilini.

faida za scent leaf unapokuwa na mimba

Mambo muhimu ya kukumbuka

Kuna imani kuwa, hisia za kuchukia chakula fulani huwa mara nyingi kwa chakula ambacho huenda kikam haribikia mama ama kumwumiza mtoto. Kuchukia vyakula katika mimba ni nadra kuwa na athari hasi kwa mama ama mtoto, hata kama huenda mama akachukia chakula chenye virutubisho muhimu mwilini. Ni vyema kuhakikisha kuwa hauchukii chakula fulani kisha kukosa virutubisho fulani mwilini. Ikiwa una kosa virutubisho fulani usipo kula chukula kama vile samaki, unaweza nunua supplements.

Unapo zidiwa na kichefu chefu ama kukosa hamu ya kula vyakula muhimu na ambazo hazina supplements, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako. Ili kuhakikisha kuwa mtoto hakosi virutubisho muhimu mwilini. Kumbuka kuwa, ukuaji wa mtoto wako unategemea chakula unacho kila katika kipindi hiki.

Soma Pia: Ishara 7 Katika Mimba Zinazo Ashiria Kuwa Kuna Hatari

Written by

Risper Nyakio