Je, Ni Salama Kuchukua Antibiotics Katika Mimba?

Je, Ni Salama Kuchukua Antibiotics Katika Mimba?

Wanao hitajika kuchukua antibiotics katika mimba hawawezi tumia penicillin kwa sababu ya mzio wanapatiwa antibiotics za macrolide badala yake.

Kulingana na The Independent, somo jipya lime vumbua aina fulani ya antibiotic inayo tumika badala ya penicillin kuhusika na aina ya matatizo ya kuzaliwa zinapo chukulia katika trimesta ya kwanza ya mimba. Wanao hitajika kuchukua antibiotics katika mimba hawawezi tumia penicillin kwa sababu ya mzio wanapatiwa antibiotics za macrolide badala yake. Lakini sasa wataalum wameonya inapaswa kutumiwa kwa tahadhari, hasa katika hatua za kwanza za mimba.

Kuchukua antibiotics katika mimba

best vitamin to take for weight loss

Matibabu mengi yako katika kikundi hiki cha antibiotics, yanayo tumika kutibu maambukizi yanayo sababishwa na bakteria. Antibiotics ni muhimu kwa kuua bakteria ama kuzikomesha kuongezeka.

Hali kama vile bacterial vaginosis hufanyika kwa wanawake walio na mimba na zinaweza hitaji matibabu kutumia dawa za antibiotics. Zinapo achwa bila kutibiwa, hali hii inaweza sababisha matatizo kama vile uchungu wa uzazi usio komaa ama maambukizi kwenye uterasi.

Walakini, sio antibiotics zote ambazo ni salama kama zinazo julikana kama macrolides. Na karibu theluthi moja ya wanawake huandikiwa antibiotics katika hatua moja ya ujauzito wao, huku moja kati ya 10 ya dawa hizi zikiwa macrolides.

Kulingana na somo lililo fanyika katika Chuo Kikuu cha London, kuna uhusiano kati ya kuchukua antibiotics za macrolide na matatizo ya kuzaliwa. Watoto 186 walio zaliwa kati ya watoto 8,632 walio zaliwa kwa wanawake walio chukua macrolides katika miezi ya kwanza mitatu ya ujauzito wao walikuwa na matatizo ya kuzaliwa. Wanawake waliochukua penicilin, kati ya watoto 95,973 walio zaliwa, 1,666 walikuwa na matatizo ya kuzaliwa.

Walakini, baada ya kuangalia sababu zote, somo hilo liligundua kuwa visa 28 vya matatizo ya kuzaliwa katika watoto 1,000, mama zao walikuwa wanachukua macrolides. Wakati ambapo wanawake walio chukua penicillin walikuwa na visa 18 vya changamoto za kuzaliwa katika watoto 1,000.

Je, antibiotics ni salama katika mimba: ni zipi zilizo salama?

kupata mimba baada ya kudhibiti uzalishaji

Kuna dawa nyingi zilizoko kwenye kikundi cha antibiotics. Kwa hivyo ni karibu vigumu kuweka kila moja kwenye kikundi hasa. Walakini tume tengeneza orodha yenye antibiotics zinazo julikana kuwa salama na zisizo salama katika ujauzito.

Zilizo salama

 • Amoxicillin
 • Clindamycin
 • Ampicillin
 • Erythromycin
 • Augmentin
 • Cefaclor
 • Penicillin
 • Cephalexin

Zisizo salama

 • Macrolides
 • Bactrim
 • Metronidazole
 • Ciprofloxacin
 • Sulfonamides
 • Doxycycline
 • Quinolones
 • Furadantin
 • Tetracycline
 • Macrobid
 • Macrodantin
 • Septra
 • Minocycline

Vidokezo unapo mtembelea daktari wako

 • Mwambie daktari wako kuhusu dawa zozote unazo chukua kabla ya kukuandikia zingine. Ikiwezekana, zibebe unapo enda hospitalini
 • Chukua dawa hizo kama unavyo elezewa na daktari wako
 • Epuka kuongeza, kupunguza ama kuto maliza dawa ulizo pewa
 • Ukimaliza kuchukua dawa kisha uhisi kuwa hali yako bado haiko sawa, hakikisha kuwa unamjulisha daktari wako.

Hizi ni hatua za kuhakikisha kuwa mtoto wako anabaki salama katika mimba.

Makala haya yameandikwa kuhimiza watu kufahamu zaidi kuhusu antibiotics na hatari zake katika ujauzito. Sio mbadala wa matibabu ya daktari wako. Wasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua dawa zozote katika ujauzito. Na umkumbushe daktari wako wakati wote kuwa una mimba anapo kuandikia dawa zozote zile.

Soma Pia: Changamoto Za Mimba Kutokana Na Lishe Yenye Kiwango Kidogo Cha Wanga

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio