Kuchungwaa Ngozi Na Mimba: Kuna Athari Zipi Kwa Mtoto Aliye Tumboni Mwa Mama

Kuchungwaa Ngozi Na Mimba: Kuna Athari Zipi Kwa Mtoto Aliye Tumboni Mwa Mama

Huenda kueusha ngozi yako unapokuwa na mimba ikawa sio wazo la busara.

Kuchungwaa ngozi kunaweza athiri mtoto aliye tumboni mwa mamake? Uhusiano kati ya kuchungwaa ngozi na mimba ni upi? Unashangaa iwapo kueusha ngozi unapokuwa na mimba kuna athari? Soma zaidi upate kufahamu jinsi kueusha ngozi ukiwa na mimba kunaweza athiri mtoto aliye tumboni mwa mama.

Kuchungwaa ngozi na mimba: Kueusha ngozi ni kufanya nini?

Skin Bleaching And Pregnancy

Image of pregnant woman touching her belly with hands; Shutterstock

Kueusha ngozi ama kuichungwaa kuna maana sawa. Kulingana na NHS, kueusha ngozi ni utaratibu wa kimapambo ambao watu hufanya ili kueusha ngozi zao na kufanya waonekana weupe.

World Health Organisation iligundua kuwa asilimia 77 ya wanawake wa Nigeria wanatumia bidhaa za kuchungwaa ngozi.

Watu wengi wanakumbatia kuchungwaa ngozi wanapo taka kuimarisha kuonekana kwa alama za kuzaliwa ama alama nyeusi kama vile melasma. Kwa ujumla, watu wanao eusha ngozi hufanya hivyo ili kugeuza ngozi zao.

Kuchungwaa ngozi hufanya kazi kivipi?

Bleaching And Pregnancy

Kulingana na NHS, kuchungwaa ngozi hupunguza kiwango cha melanin kwenye ngozi na kupunguza utoaji wa melanin. Melanin ni hali ya ngozi ya kuwa na rangi nyeusi. Inasaidia kulinda ngozi kutokana na miale hatari ya jua.

Kwa kutumia bidhaa za kuchungwaa ngozi kila mara, ngozi inakuwa nyeusi na kupunguza melanin.

Kuchungwaa Ngozi na Mimba: Hiari za kuchungwaa ngozi zilizoko ni kama zipi?

kuchungwaa ngozi na mimba

Watu wanao amua kuchungwaa ngozi wanapaswa kufikiria kwa kina kabla ya kuamua mbinu watakayo tumia. Hata kama mbinu iliyo maarufu zaidi ya kuchungwaa ngozi inahusisha utumiaji wa krimu za kuchungwaa ngozi ama mafuta ya kuchungwaa na mbinu zingine zilizoko.

Hizi ni kama vile:

 • Tembe za kemikali
 • Krimu za kuchungwaa ngozi
 • Matibabu ya laser
 • Tembe ama sindano za glutathione

kuchungwaa ngozi na mimba

Tembe za kemikali za kuchungwaa ngozi 

Tembe za kemikali za kuchungwaa ngozi hufanya kazi vitofauti ikilinganishwa na tembe za kawaida. Huu sio utaratibu wa kutoa seli mpya tu na kuacha ngozi freshi na iliyo changa zaidi. Tembe za kemikali za kuchungwaa ngozi unapokuwa na mimba huwa na viungo vinavyo punguza utoaji wa melanin vinaongezwa kwa kemikali. Matokeo yake ni ngozi isiyo ng’aa.

Kuchungwaa ngozi kwa kutumia sitima ama laser

Sitima inatumika kutoa ngozi iliyo haribika. Sehemu ya juu ya ngozi inapotolewa, joto kutoka kwa laser inasaidia kuboresha utoaji wa seli mpya za ngozi.

Sindano na Tembe za Glutathione 

Nyakati za hivi punde, glutathione imekuwa maarufu sana kwa kuchungwaa ngozi. Watu wengi wanazichukua zikiwa pamoja ili kupata matokeo ya mbio. Masomo haya yalikuwa na nia ya kujua iwapo ina uwezo wa kuchungwaa ngozi.

Walakini, kuna watu wanao fanya uamuzi wa kutumia sindano za glutathione ili kupata matokeo ya mbio ikilinganishwa na tembe. Hii inaweza kuwa hatari iwapo una mimba ama la.

Kuchungwaa ngozi na mimba: Krimu za kuchungwaa

Unaweza pata tembe ama krimu za kuchungwaa kutoka maduka tofauti pahali popote. Kiungo kilicho maarufu zaidi ni hydroquinone. Baadhi ya krimu hizi huwa na mercury na steroids ambazo ni hatari sana. Bidhaa za kutunza ngozi zinazo kuwa na mercury, steroids na hydroquinone zimepigwa marufuku katika sehemu nyingi duniani, ila baadhi ya hizi bado ziko kwa soko na madukani.

Je, kuchungwaa kunaweza athiri mtoto aliye tumboni – athari za kuchungwaa ngozi

 • Kuchungwaa hufanya ngozi iwe nyembamba na kupunguza uwezo wake wa kupanuke, yenye maana kuwa unapo jichungwaa ukiwa na mimba, ngozi kwenye sehemu ya tumbo huenda ikaanza kupasuka.
 • Mercury, ni mojawapo ya viungo vya krimu nyingi na inayo sababisha saratani.
 • Kuchungwaa hutoa rangi nyeusi ama melanin kwenye ngozi yako na kutoa ulinzi wa asili wa ngozi dhidi ya saratani ya ngozi.
 • Ochronosis ni tatizo ya linalo tokana na kuchungwaa ngozi.
 • Sindano ama tembe za glutathione sio salama unapokuwa na mimba ama ukinyonyesha.
 • Kulingana na NHS, krimu za kuchungwaa zinaweza sababisha matatizo ya maini, neva na figo.
 • Viungo vinavyo tumika kwa krimu za kuchungwaa zinaweza sababisha changamoto kwenye watoto na hii ndiyo sababu kwa nini sindano ama tembe za kuchungwaa sio wazo bora.

Unapaswa kuichungwaa ngozi yako ukiwa na mimba?

Unacho fanya na ngozi yako ni uamuzi wako bila shaka. Ila, huenda ikakubidi kuwacha kuichungwaa ngozi yako unapokuwa na mimba. Mimba huja na matatizo mengi ya ngozi, na huenda ukapata majaribio ya kuficha mimba yako ama matatizo ya ngozi kwa kuichungwaa ngozi. Walakini, unapaswa kuangalia athari hasi za kuchungwaa unapokuwa na mimba kabla ya kufanya uamuzi.

Kumbukumbu: NHS

World Health Organisation (WHO)

Immune Health Science 

BBC News Pidgin

Soma pia: Excessive sleep during pregnancy- Is it normal?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio