Kudhibiti hasira kwa wazazi ni muhimu. Kukasirika na kuwa na hasira ni jambo la kawaida kwa binadamu. Ni vigumu kwa wazazi kutokasirika wanapokuwa na watoto wanaofanya wanachotaka mara kwa mara. Lakini kutodhibiti hasira kwa wazazi kunaweza kuwa na athari hasi kwa mtoto. Wazazi wanaweza kutumia mbinu hizi kudhibiti hasira yao.
Vyanzo vya hasira

Mwili unapogundua kuwa kuna hatari, hutoa mwitikio huu. Mtu anapokasirika, mwili hutoa kichocheo cha adrenaline, misuli yake kujikaza zaidi, mpigo wa moyo na shinikizo la damu kwa usawa kuongezeka. Kuna baadhi ya watu wanaokasirika kwa urahisi sana, wengine walizaliwa hivi, huku wengine wakitatizika na hali ya kimatibabu.
Vyanzo vya kukasirika ni kama vile kuhisi kuwa hawadhaminiwi, kuwa na shaka nyingi, kukumbuka mambo magumu yaliyokutendekea hapo awali. Pia, sio watu wengi wanaojua jinsi ya kujieleza wanapokuwa na hasira. Wazazi walio na watoto wachanga hukasirika mara kwa mara wanapofanya mambo wasiyofaa kufanya, kukataa kula chakula na kadhalika. Kuhisi kuwa mchumba wako hakusaidii ni chanzo kingine cha wazazi kukasirika ovyo. Masuala ya uhusiano na ya kifedha huzua hasira pia.
Jinsi hasira ya wazazi inavyoathiri watoto

Ni muhimu sana kwa wazazi kujua jinsi ya kudhibiti hasira zao wanapokuwa na watoto wachanga. Kukasirika na kutumia maneno makali mbele ya watoto wao huwa na athari hasi katika ukuaji wa kiakili wa mtoto na katika siku zao za usoni.
Kwa kawaida, mtoto anapomwona mzazi wake amekasirika, hujilaumu. Kutumia maneno yenye makali kwa mtoto humfanya ahisi kuwa hadhaminiwi ama yeye ni mtu mbaya.
Huenda mtoto akashindwa kucheza na marafiki zake, kusikiliza darasani, kunyamaza na kujitenga na watu ama kutatizika kulala.
Mzazi anapokuwa na hasira, sio jambo la busara kumuadhibu mtoto wake. Badala yake, anapaswa kuchukua muda kutulia kisha kuzungumza na mtoto.
Kudhibiti hisia zako
Unapogundua kuwa umekasirika mbele ya mtoto wako, epuka kutumia lugha yenye makali ama kumchapa, badala yake:
- Ondoka kutoka chumbani
- Tembea kwa dakika chake utulie
- Nenda kwenye chumba cha kulala
- Mwambie mtoto aende akacheze na watoto wengine
Unapogundua kuwa ni vigumu kwako kudhibiti hasira yako, zungumza na mtaalum.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kudhibiti Hasira Kama Mzazi: Mwongozo Kwa Wazazi Wote