Njia Bora Zaidi Za Kudhibiti Uzalishaji Kwa Mama Anaye Nyonyesha

Njia Bora Zaidi Za Kudhibiti Uzalishaji Kwa Mama Anaye Nyonyesha

Hongera kwa kujifungua kitita chako cha mapenzi! Bila shaka wakati huu, hauko tayari kuwa mjamzito tena. Kwa hivyo, ni njia zipi za kudhibiti uzalishaji kwa mama aliye jifungua zinazo shauriwa.

Njia za kudhibiti uzalishaji kwa mama aliye jifungua

Umetoka hospitalini tu na huenda bado una uchovu baada ya kujifungua na hauna nguvu za kuanza kufikiria kuhusu mbinu utakazo tumia kudhibiti uzalishaji. Madaktari wengi wana washauri wamama walio jifungua tu, kuto fanya ngono hadi baada ya kuangaliwa baada ya wiki 6. Kwa hivyo, katika kipindi hiki, hautakuwa na shaka ya kutumia mbinu yoyote ile ya uzalishaji. Pia, mwili wako bado hauja pona.

Kuna aina nyingi za mbinu za kudhibiti uzalishaji.

Tembe

kudhibiti uzalishaji kwa mama aliye jifungua

Tembe za kudhibiti uzalishaji huwa na homoni ambazo zinaweza uathiri mwili wako hasa katika kipindi hiki unapo nyonyesha. Huenda baadhi ya tembe zika punguza utoaji wako wa maziwa na kufanya iwe vigumu kwako kunyonyesha mtoto wako.

Kuna aina mbili za tembe za kudhibiti uzalishaji. Zilizo na progestin peke yake ama zilizo changanywa, progestin na estrogen. Zilizo na estrogen zita athiri kiwango cha maziwa ya mama unacho toa. Kwa hivyo kwa wanawake wanao nyonyesha, huenda progestin ikawa bora kwao kwani haiathiri maziwa.

IUDs

kutoa IUD

Ukitaka njia ya kudhibiti uzalishaji ya muda mrefu isiyo ya kudumu daima, IUD ni wazo bora kwako. Kuna aina mbili za intrauterine device, iliyo na kichocheo za progestin na ya copper. Daktari wako ata iingiza kwenye uterasi yako, punde tu baada ya kujifungua ama baada ya wiki 6. Madaktari wengi wana shauri uwekwe baada ya wiki 6 unapo enda kukaguliwa kwani kuiweka punde tu baada ya kujifungua, huenda ikasukumwa nje na mwili wako.

Sindano

Kuna aina ya sindano za miezi mitatu zinazo tumika kudhibiti uzalishaji. Sindano hizi huwa na kichocheo cha progestin.

Implants

Hizi huwa bora kwa wanao lenga kudhibiti uzalishaji kwa hadi miaka mitatu. Aina hii ya kudhibiti uzalishaji kwa mama aliye jifungua hakuna athari kwa maziwa yake kwani ina homoni ya progestin peke yake.

Kondomu

kudhibiti uzalishaji kwa mama aliye jifungua

Ni rahisi kutumia na zinapo tumika inavyo paswa, zina saidia kuepusha uwezekano wa kupata mimba. Ni salama kwa mama kwani hazina homoni zozote zile.

Soma Pia:Mimba Ya Bahati Mbaya Ama Usiyo Tarajia: Huenda Likakufanyikia

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio