Orodha Ya Vidhibiti Uzalishaji Vilivyo Salama Unapo Nyonyesha

Orodha Ya Vidhibiti Uzalishaji Vilivyo Salama Unapo Nyonyesha

Hongera kwa kujifungua mtoto na kuitwa mama! Katika kipindi hiki unapo nyonyesha, huenda ukawa hauko tayari kupata mimba tena. Ni mbinu zipi za kudhibiti uzalishaji zilizo bora kwa mama anaye nyonyesha?

Una dirisha ya kufanya uamuzi wa aina utakayo pendelea. Madaktari wengi wanawashauri kina mama kujitenga na ngono kwa wiki za kwanza sita hadi wanapo kaguliwa ama kufanyiwa vipimo. Baada ya wiki sita, utakuwa na anuwai nyingi za kuamua kutoka.

Mbinu za kudhibiti uzalishaji kwa mama anaye nyonyesha

  • Tembe za kudhibiti uzalishaji

Orodha Ya Vidhibiti Uzalishaji Vilivyo Salama Unapo Nyonyesha

Kuna habari kuwa, huenda zingine zika punguza utoaji wako wa maziwa ya mama na kufanya iwe vigumu kwa mtoto kupata kiwango cha maziwa kinacho mfaa. Kuna baadhi ya homoni ambazo huenda zikawa na athari hiyo, ila sio zote.

Je, una fahamu aina gani ya tembe za kudhibiti uzalishaji?

Kuna aina mbili kuu:

  • Za kipekee zilizo na progestin ama maarufu kama mini-pill
  • Za kuchanganya zilizo na estrogen na progestin

Mara kwa mara, estrogen huenda ika athiri utoaji wa maziwa. Kwa hivyo unapo mjulisha daktari kuwa unamnyonyesha mtoto, nafasi kubwa ni kuwa ata kushauri kutumia mini-pill, haita athiri utoaji maziwa wako.

Daktari akiona kuwa tembe za kuchanganya zinakufaa zaidi ikilinganishwa na mini-pill, ata ngoja hadi wiki 5 ili akuandikie tembe hizo.

Sababu nyingine kwa nini mama anapaswa kungoja wiki chache kabla ya kuanza kutumia vidhibiti uzalishaji ni kuwepo kwa damu iliyo ganda.

  • IUDs

Intrauterine device kwa kifupi IUD ni mojawapo ya mbinu za kudhibiti uzalishaji ya muda mrefu. Wiki sita baada ya kujifungua, daktari wako ata iingiza kwenye uterasi yako unapo mtembelea kuangalia maendeleo.

Kuna aina mbili za IUD; ya copper na iliyo na homoni ya progestin. Na zote ni salama kwa mama anaye nyonyesha kwani, ya copper haina homoni zozote kwa hivyo utoaji maziwa wako hauta athiriwa. Nyengine iliyo na homoni ya progestin ziko katika viwango vidogo, kwa hivyo hakuna mabadiliko makuu.

  • Implants na sindano

Hizi ni mbinu za kudhibiti uzalishaji zenye homoni, sio za kudumu sana ikilinganishwa na tembe ya kila siku lakini hauchukui kila siku kama tembe.

Implants. Katika mbinu hii, daktari anaingiza chombo sawa na kijiti kwenye upande wa juu wa mkono wako. Mbinu hii ina homoni ya progestin na hai athiri utoaji wako wa maziwa ya mama.

Pete ya uke. Pete hii ina ingizwa ndani ya uke wako na kubaki huko kwa wiki tatu kisha kubadilishwa. Pete hii ina homoni za progestin na estrogen. Uta shauriwa kungoja hadi baada ya wiki sita ili kuanza kuitumia.

Sindano. Daktari wako anaweza kudunga sindano baada ya kila miezi mitatu. Na huwa na viwango vya juu vya progestin.

Mbinu zingine za kudhibiti uzalishaji

Mbinu hizi ni salama kwa mama anaye nyonyesha na hazina homoni zozote. Kama vile:

Diaphragm. Daktari wako atakuweka mbinu hii wiki sita baada ya kujifungua. Ili kuupa mwili wakati tosha wa kupona na kurudi kawaida. Huenda ukahitaji saizi mpya baada ya kujifungua.

kudhibiti uzalishaji kwa mama aliye jifungua

Kondomu. Zina tumika na mwanamme, ni rahisi kutumia na zina dhibiti kupata mimba zinapo tumika vizuri.

Kofia ya kizazi (Cervical cap). Kifaa hiki kinafunika kizazi cha mwanamke. Ikiwa hii ndiyo mbinu uliyo kuwa unatumia kabla ya kupata mtoto, mwulize daktari wako akushauri ikiwa utaendelea kuitumia ama utabadilisha.

Chanzo: NHS

Soma PiaPunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kutumia Mitindo Hii Ya Ngono

Written by

Risper Nyakio