Yote Unayo Hitajika Kufahamu Kuhusu Hali Ya Blighted Ovum

Yote Unayo Hitajika Kufahamu Kuhusu Hali Ya Blighted Ovum

Hali ya blighted ovum inaweza mfanya mwanamke mwenye mimba kukata tamaa kwa sababu hakuna fetusi inayo kua kwenye uterasi.

Hali Ya Blighted Ovum- Mimba Ila "Isio Mimba"

Huenda ukawa ulisoma kuhusu ushahidi wa Anne Marianne katika makala ya Kufanikiwa Kujifungua Mtoto Baada Ya Blighted Ovum. Kulingana na Shirika la Kuharibika kwa mimba, hali ya blighted ovum ama mimba ya anaembryonic yote huwa hali ambapo seli za kuumba fetusi hukoma kukua. Ila katika wakati huo huo, sac ama mfuko wa mimba mahali ambapo fetusi iko, itaendelea kukua.

Hali ya blighted ovum na kinacho sababisha hali hii

Mwanamke mwenye mimba huenda akakosa kujua kuwa anashuhudia hali hii kwa sababu tumbo hubaki imeongezeka saizi kana kwamba ana mimba. Mwanamke ataendelea kudhihirisha ishara za mimba kama vile kuhisi kutapika, kuhisi kizungu zungu na ugonjwa wa asubuhi.

Hali hii mara nyingi hudhibitika katika umri wa wiki 8 hadi 13 kupitia kwa utaratibu wa ultrasounda.

Kinacho sababisha hali hii

Kuhusu vyanzo vya hali hii, wataalum husema kuwa kuna sababu nyingi. Kwanza, manii kukosa kuwa bora na seli za mayai ama ugawaji mbaya wa seli huenda ukasababisha hali hii. Mwili wa mwanamke mwenye mimba huenda ukadhibitisha hii kama hali isiyo ya kawaida na kukomesha utaratibu wa mimba na kufanya fetusi kukosa kukua zaidi.

Pili,  maambukizi ya TORCH (TOxoplasm, Rubella, Cytomegalovirus / CMV na  Herpes) huenda ikasababisha hali hii ya blighted ovum. Virusi, bakteria ama vimelea vinavyo sababisha maambukizi ya TORCH huenda yakaingia mwili wa mama mwenye mimba kupitia kwa nyama ambayo haija pikwa vizuri ama iliyo na sumu kama vile uchafu wa paka (Toxoplasm), kuwasiliana na wagonjwa (rubella), kuwekwa damu ama kuwasiliana kingono (CMV na herpes), usafi mdogo wa chakula.

Tatu, ACA (anticardiolipin) inayo sababisha antiphospholipid syndrome ama kushikana kwa damu pia kumedhihirika kusababisha hali hii. ACA syndrome inasababisha mfumo wa kinga kufikiria kuwa seli za protini za kawaida kana kwamba ni 'adui' na kuziweka pamoja zinakuwa nyembamba.

Iwapo mwanamke mwenye mimba ana shuhudia ACA, mishipa ya damu inayo enda kwenye fetusi ina shikana na chakula cha fetusi kinaweza kosa kufika. Na kuziba ukuaji wa fetusi.

Njia bora ya kujua iwapo mama ana hali hii ni kupitia kwa utaratibu wa kipimo cha ultrasound katika trimesta ya kwanza ya mimba.

blighted ovum

Jinsi ya kuepuka hali hii?

Sasa hivi, hakuna njia dhabiti ya kuepuka hali hii. Ila haupaswi kufa moyo kwa sababu mama walio pitia hali hii ya blighted ovum bado wana nafasi ya kupata mimba na kujifungua kwa njia ya kawaida. (Kama bi. Anne baada ya kuugua hali hii mara mbili).

Unahitajika tu kungoja hadi vipindi vitatu vya hedhi ilikufanya ngono ama kutunga. Iwapo una historia ya kimatibabu inayo husishwa na TORCH, ni wazo bora kupata chanjo ya anti-rubella.

Hakikisha kuwa wakati wote wewe ni msafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na kuosha matunda na mboga zako vyema. Wakati wote valia glavu iwapo unataka kusafisha gari yako.

Pia, kuna ushauri kuwa mama hawapati mimba punde tu baada ya kuwa na hali hii. Usipuuze hali hii. Angalia mzunguko wa damu yako mara kwa mara. Wanawake wenye mimba wanapaswa kufanya kipimo mara mbili kwa wiki hadi fetusi inapo kuwa miezi 7 kuhakikisha kuwa inakua ipasavyo. Kuangalia viwango vya ACA na vipimo vya maabara pia kunahitaji kufanyika angalau mara moja kwa wiki sita.

Kwa bahati mbaya, hakuna njia ya kuongeza ubora wa manii ama mayai yaliyo mabaya kwa sababu ubora wake unadhibitika mtu anapo zaliwa. Kuboresha mitindo ya maisha yako na kuepuka fikira nyingi ni mojawapo ya njia zinazo shauriwa ili kuongeza ubora wa manii ama mayai ili ubora usipunguke zaidi.

Kumbukumbu: Nova Tabloid, American Pregnancy Association, Mayo Clinic, Kompas. com, the Miscarriage Association

Soma pia: What is ectopic pregnancy?

Written by

Risper Nyakio