Ikiwa wewe ni kama mimi, kila unapowaona wanandoa wanaopendana walio katika miaka yao ya uzeeni, unavutiwa na mapenzi yao. Katika kila kitu, wamekuwa pamoja kwa miaka hiyo yote na wangali wanakuza utangamano wao na wakaweza kudumisha ndoa yenye furaha. Zungumza kuhusu mapenzi ya undani…bila shaka yanaweza kuonekana.
Mapenzi na ndoa hata yanapo egemezwa na hisia nyingi, yanategemea kazi nyingi na kujitolea. Ni kuhusu kujiahidi kwa mtu mwingine na kufanya kila kitu uwezacho kuwaonyesha jinsi unavyo jitolea. Siri ni nini? Wanandoa wanawezaje kudumu hivyo vyote? Kulingana na utafiti, kuna siri 5 za kudumisha ndoa yenye furaha kwa maisha yako yote.
Siri za kudumisha ndoa yenye furaha

- Mawasiliano
Bila shaka, hii sio mara ya kwanza unapo yasikia haya. Mawasiliano ndiyo nguzo ya ndoa yenye mafanikio. Wakati ambapo ni jambo linalo semwa mara kwa mara, utafiti ulidhibitisha kuwa huu ndiyo ushauri uliokuwa maarufu zaidi. Huku kuna maanisha kuzungumza kuhusu mambo yote muhimu na madogo maishani na mchumba wako. Na sio kuzungumza tu, unahitaji kuwasikiliza pia na kusoma jinsi ya kuzungumza bila fiche. Waeleze hisia na mawazo yako na utakuwa kwa njia inayofaa.
2. Mweke mchumba wako mbele ya watoto wako
Kabla ya kuwapata watoto, ni rahisi kumpa mchumba wako kipau mbele. Baada ya kuwapata watoto, huenda ikawa na ugumu kidogo. Baada ya kazi, watoto, na mchumba, inaweza kuwa vigumu kwako kupatia vitu vyote kipau mbele. Kilicho muhimu ni kuwa wakati inapofaa, unamweka mchumba wako kabla ya mengine yote. Usipo, uko katika hatari ya kukuza utengano ambao utaathiri ndoa yenu baadaye. Kumbuka kuwa uhusiano wa muda mrefu wenye mafanikio na afya una athiri watoto wenu pakubwa.
Image : Shutterstock
3. Msiwe na vita mkiwa na njaa
Huu ndiyo ushauri wa kusisimua zaidi. Lakini una chanzo. Watu huwa na hasira wanapokuwa na njaa na vita vidogo huanzisha matatizo makubwa baadaye. Usikubalishe njaa ikuongoze. Nyamaza hadi baada ya kula kisha umweleze mchumba wako kinacho kusumbua.
4. Kuwa tayari kubadilika
Bila shaka hakuna anaye stahili kubadilika ili kumpendeza mchumba wake, lakini hilo halimaanishi kuwa huwezi imarisha tabia zisizo pendeza. Kuwa tayari kukua kama mtu binafasi kwa njia zitakazo wanufaisha nyote. Ni njia bora ya kushinda matatizo katika ndoa.
5. Jitunze
Kupata mtu unayetaka kuwa naye maishani mwako mwote sio jukumu lako kukutunza. Usitupilie vitu ulivyofanya hapo awali kuitunza afya na urembo wako kama kufanya mazoezi na kuvalia mavazi ya kupendeza. Hakikisha kuwa wakati wote unajitunza na kujipamba inavyofaa. Ni muhimu katika kudumisha ndoa yenye furaha.
Soma Pia: Aina Tofauti Za Kupanga Uzazi Na Umuhimu Wake Kwa Jamii Na Wanandoa