Vidokezo Muhimu Vya Kudumisha Urembo Katika Ujauzito!

Vidokezo Muhimu Vya Kudumisha Urembo Katika Ujauzito!

Mama mwenye mimba anahitaji kupumzika kwa masaa zaidi. Kwani mwili wake unachoka kutokana na shinikizo la tumbo kubwa.

Mimba ni kipindi cha maisha kama vipindi vingine na katika wakati huu, mama anapaswa kuzidi kupendeza. Na kuvunja shingo kila anapo pita. Huu sio wakati wa kuvalia mavazi yanayo ficha tumbo lako linalo zidi kuwa kubwa kila uchao. La hasha! Huu ni wakati wa kuzidi kujipodoa, kurembeka na kung'ara. Kuna vidokezo ambavyo mama mjamzito anaweza fuatwa vya kudumisha urembo katika ujauzito.

Kudumisha Urembo Katika Ujauzito

kudumisha urembo katika ujauzito

 

  1. Valia mavazi ya kupendeza

Mavazi ya mama hubadilika kwa sana anapokuwa mjamzito. Ila sio kusema kuwa anapaswa kukoma kuvutia katika kipindi hiki. Kuna aina tofauti ya mavazi ya kupendeza ambayo mama mwenye mimba anaweza valia anapokuwa katika safari yake ya ujauzito. Ili azidi kupendeza na kuonyesha umbo lake hadi pale atakapo jifungua. Ni vyema tutupilie mbali wazo la kuvalia mavazi marefu yanayo ficha tumbo la kupendeza linalo beba kitita cha mapenzi unacho kitarajia kwa miezi tisa.

2. Lishe bora

Vidokezo Muhimu Vya Kudumisha Urembo Katika Ujauzito!

Umuhimu wa mlo bora katika ujauzito hauwezi sizitizwa vya kutosha. Tupilia mbali vitafunio vyenye sukari na ufuta mwingi unapokuwa na mimba. Huu ni wakati wa kuhakikisha kuwa mwili wako unapata virutubisho bora na tosha. Kula lishe yenye afya kuna saidia mama kwa kupunguza matatizo ya ngozi.

3. Kunywa maji kwa wingi

Maji ni muhimu sana katika kutoa sumu mwilini. Unapokunywa maji tosha ukiwa mjamzito, unatoa taka mwilini na una imarisha ubora wa ngozi yako. Na sio kwa mama tu, mbali kwa mtoto anaye kua tumboni mwako. Una shauriwa kunywa angalau glasi nane ama lita 2 za maji kila siku.

4. Pata usingizi wa kutosha

Mama mwenye mimba anahitaji kupumzika kwa masaa zaidi. Kwani mwili wake unachoka kutokana na shinikizo ambalo tumbo linalo zidi kukua linawekelea kwenye miguu na viungo vingine. Ni vyema kwa mama kupata angalau masaa manane ya kulala kila siku, na pia kuhakikisha ana lala kwa upande na wala sio kwa tumbo ama mgongo.

5. Kufanya mazoezi

Ikiwa ulikuwa unafanya mazoezi sana kabla ya kupata mimba, huu sio wakati wa kukoma. Zidi kufanya mazoezi, ila hakikisha kuwa ni mazoezi mepesi. Ni vyema kufanya mazoezi na mtaalum wa mazoezi ili akushauri mazoezi bora katika wakati huu ambayo hayatakuwa na athari hasi kwa mimba yako.

Mabadiliko ya homoni mwilini katika kipindi cha ujauzito huenda yaka athari uso wako. Na ukaanza kushuhudia kuwepo kwa upele kwenye uso wako. Kuna bidhaa ambazo unaweza kutumia kurekebisha hali hii.

Kumbuka kufurahia kipindi hiki maishani mwako. Na ufanye uwezavyo kuhakikisha kuwa una starehe, punguza mawazo mengi na ujiandae kadri uwezavyo kumkaribisha mwanao.

Soma pia:Mwongozo Wa Wiki Ya 33 Ya Ujauzito: Yote Unayo Paswa Kujua

 

Written by

Risper Nyakio