Vidokezo Salama Vya Kuepuka Kuambukizwa Homa Ya Korona

Vidokezo Salama Vya Kuepuka Kuambukizwa Homa Ya Korona

Katika bara la Afrika, sisi wote tunapaswa kuwa mbele katika kuepuka kupata virusi hivi vya korona.

Na visa vingi vinavyo endelea kuripotiwa kila siku vya homa ya korona inayo sambaa kwa urahisi na kuadhiri sehemu tofauti nchini; limekuwa jambo la lazima kwa wanafamilia na watu binafsi kuchukua hatua za mapema kuepuka kuendeleza kusambaa kwa virusi hivi. Hii ndio sababu tume tengeneza vidokezo kukusaidia kuepuka kuambukizwa homa ya korona.

Kutoka chanzo chake kwenye soko la chakula mkoa wa Wuhan, Uchina, mwezi wa kumi na mbili mwaka uliopita wa 2019; hadi kwa nchi zilizo mbali kama Umerikani na Ufilipino, virusi hivi vimeathiri ma elfu ya watu, na vifo vinavyo endelea kuongezeka zaidi ya 4,000.

Ugonjwa huu unatoka na kuambukizwa na virusi vya SARS-CoV-2. Mwezi uliopita, Shirika la Afya Duniani lilipatia virusi hivi jina la COVID-19, inayo maanisha ugonjwa wa homa ya korona ugonjwa wa 19. Hata na wasiwasi unaoshuhudiwa baada ya habari za virusi hivi kusambaa, ni vigumu kwako kuugua SARS-CoV-2; isipokuwa pale unapo patana na mtu aliye dhibitika kuwa na virusi hivi.

Soma zaidi upate maarifa jinsi ya kujiepusha kupata virusi hivi; na jinsi ya kuepuka kusambaza virusi hivi iwapo uko nazo tayari.

Kuepuka Kuambukizwa Homa Ya Korona Ili Usiugue

preventing coronavirus infection

Umesikia kuwa unapaswa kunawa mikono yako kwa kutumia sabuni mara kwa mara. Ila, kuna njia unayo paswa kunawa mikono yako vyema. Na hiyo ni kunawa kwa kutumia sabuni kwa hadi sekunde 20. Sekunde 20 ni refu kiasi gani? Muda mrefu kadri inavyo chukua kuimba "ABCs."

Angalia vidokezo zaidi vya kujikinga tulivyo orodhesha:

 • Usiguse uso wako, mapua ama mdomo na mikono michafu.
 • Usitoke nje iwapo unahisi kana kwamba we ni mgonjwa ama una dalili za homa ama mafua.
 • Kaa angalau fiti 3 mbali na mtu anaye chemua ama kukohoa.
 • Funika mdomo wako kwa kutumia upande wa ndani wa kiwiko chako unapo chemua ama kukohoa.
 • Tupa mbali tishu baada ya kutumia.
 • Clean any objects you touch a lot. Use disinfectants on objects like phones, computers, utensils, dishware, and doorknobs.
 • Safisha vifaa unavyo gusa sana. Tumia disinfectants kwa vifaa kama vile simu, kompyuta, vyombo, ama

Virusi hivi vinapokuwa ndani ya watu, virusi vya korona vinasambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kupitia matone ya mfumo wa kupumua. Hili ni jina la kimafundi la vitu vilivyo na unyevu nyevu vinavyo sambaa kwa hewa unapokohoa ama kuchemua. Virusi hivi vinakaa kwenye matone na unaweza vipumua kwenye mfumo wako wa kupumua (mafua na koo ya pumzi); ambapo virusi hivi vinaweza sababisha maambukizo.

Huenda ukawa umesikia kuwa virusi hivi vya korona vinakaribiana na homa ya kawaida ama mafua ya msimu, ila vinasababisha vifo. Madaktari wanasoma mambo mapya kuhusu virusi hivi kila siku. Kwa umbali huu, tunafahamu kuwa COVID-19 huenda hapo mwanzoni ikakosa kuwa na dalili zozote. Unaweza beba virusi hivi hadi kwa siku 2 ama wiki 2 kabla ya kuona dalili zake.

Baadhi ya dalili za kawaida zinazo husishwa na COVID-19 ni kama vile:

 • Upungufu wa kupumua
 • Kuwa na kikohozi kinacho zidi kuongezeka kila wakati
 • Kiwango cha joto nyingi kinacho zidi kuongezeka

Orodha kamilifu ya dalili hizi bado ina fanyiwa utafiti zaidi.

Kuepuka Maambukizo ya Homa ya Korona Kwa Watu Wengine Unapokuwa na Virusi Hivi

covid-19

Kuna orodha ya mambo muhimu unayo paswa kufanya iwapo unashuku kuwa una virusi hivi vya COVID-19. Utahitaji utunzi wa kimatibabu, ila kwanza utahitaji kujipeleka kwa mamlaka ya nchi ya afya ili uweze kupimwa. Wakati kati ya kujishuku na kufanyiwa vipimo, kaa umejitenga nyumbani mwako. Inajulikana kama kuji karantini na ina maana kuwa unakaa nyumbani na kuepuka umati wa watu ama kupatana na watu wengi. Epuka kupatana kwa uma na unapokohoa ama kuchemua, fanya hivi kwenye sehemu ya ndani ya kiwiko chako. Matone yana ambukiza virusi hivi. Kwa kufuata usafi mwema wa mfumo wa kupumua, unalinda watu walio karibu na wewe kutokana na virusi hivi kama vile homa, mafua na COVID-19.

Kaa nyumbani iwapo hauhisi vyema. Iwapo una joto jingi, kukohoa ama matatizo ya kupumua, mwone daktari upate matibabu. Fuata maagizo unayopatiwa na mamlaka ya afya yaliyo karibu nawe.

Mamlaka ya nchi na mitaa watakuwa na ujumbe ulio afikiana kitarehe kuhusu hali ilivyo kwenye eneo lako. Kupiga simu kabla ya kufika huko kutamsaidia mtunzaji wako wa afya kukuelekeza kwa kituo mwafaka cha afya. Huku kutakulinda na kukusaidia kuepuka kuambukizwa homa ya korona na maambukizo mengine.

Ongea na daktari wako bila kukawia iwapo unafikiria kuwa una virusi hivi vya COVID-19 ama umeona dalili zake. Daktari wako ataongea na maafisa wa mitaa wa afya ya umma ili kukupatia mwelekezo iwapo vipimo vinahitajika.

Fundi wa maabara ataoa sampuli ya damu kwa kutumia sindano ama atumie swab ya pamba kutoa sampuli ya mate ama uchafu wa mfumo wako wa kupumua kutoka kwa mapua ama nyuma ya koo lako.

Sampuli hii inaenda kwa kituo cha vipimo ili kuhakikisha kuwepo kwa nyenzo za virusi ama antibodies zinazo guswa na virusi hivi.

Jinsi ya Kuepuka Covid-19: Matibabu Na Matatizo yake

preventing coronavirus infection

Kwa sasa, hakuna matibabu ya kipekee yaliyo kubalika ya COVID-19 na hamna tiba ya maambukizo haya, ingawa matibabu na chanjo kwa sasa zinafanyiwa utafiti. Badala yake, matibabu yanazingatia kuthibiti dalili kwani virusi hivi vinakawia kuonekana.

Virusi vingine vya homa ya korona kama SARS na MERS vina chanjo na matibabu. Baadhi ya matibabu ya virusi hivi sawa ni kama vile:

 • Madawa ya antiviral ama retroviral
 • Usaidizi wa kupumua, kama vile uingizaji wa hewa wa kimitambo (mechanical ventilation)
 • Steroids kupunguza kufura kwa mapafu
 • Utoaji wa plasma za damu

Hali tata zaidi ya maambukizo ya SARS-CoV-2 ni aina ya pneumonia: riway ya 2019 ya corona-infected pneumonia (NCIP).

Matokeo kutoka kwa somo la 2020 la watu 138 walio lazwa hospitali katika mkoa wa Wuhan, Uchina, na NCIP walipata kuwa asilimia 26 ya hawa waliolazwa hospitalini walikuwa na visa vilivyo zidi na walihitaji kutibiwa kwenye utunzi wa dharura (ICU).

Karibu asilimia 4.3 ya watu walioko kwenye vyumba vya walio lemewa (ICU) walikufa kwa sababu ya aina hii ya pneumonia. Umbali huu NCIP ni tatizo la kipekee ambalo limehusishwa na homa ya korona ya 2019. Watafiti wameona matatizo yafuatayo katika watu walio pata virusi hivi vya COVID-19.

 • Matatizo ya kupumua (respiratory distress syndrome- ARDS)
 • Mpigo wa moyo usio wa kawaida (arrhymia)
 • Mshtuko wa cardiovascular
 • Uchungu mwingi wa misuli (myalgia)
 • Uchovu
 • Kuharibika kwa moyo (heart damage) ama mshtuko wa moyo

CDC Healthline WHO

Originally written by AyeeSha

Translated by Risper Nyakio

Soma pia: NCDC May Ban Large Gatherings To Prevent The Spread Of COVID-19 (Coronavirus)

Written by

Risper Nyakio