Kila wakati mwanamke anapofanya mapenzi kuna uwezekano wa kubeba mimba. Iwapo mtu hayuko tayari kushika mimba huweza kutumia kinga. Kunazo njia za kuepuka kutunga mimba kiasili baada ya ngono.
Kuepuka Kutunga Mimba Kiasili Baada Ya Ngono

Wanandoa wengi hukadiria kuwa na watoto ila kwa mpango. Kwa hii sababu, wengi huzuia mimba zisizotarajiwa kwa kutumia dawa za kupanga uzazi ambazo mara nyingi huwa na madhara kwa mwili. Hili husababisha wengi kutafuta njia za kiasili ambazo zinaweza kuzuia ujauzito. Lakini hakuna njia yoyote ambayo ina ufanisi wa asilimia 100. Hivyo ni busara kujikinga ipasavyo.
Kuna njia ambazo huwiana moja kwa moja na mwili na utafiti wa kisayansi. Kujiepusha na mapenzi katika hivi vipindi huzuia ujauzito. Kama vile:
- Kufanya mapenzi kwenye kipindi kisicho cha rutuba. Unaweza kuepuka siku zako za rutuba ambazo hutokea wiki mbili kabla ya kipindi cha hedhi
- Kutumia njia ya kuchomoa uume wakati wa kufanya mapenzi
- Kuzingatia joto lako la mwilini. Ongezeko la joto mwilini huweza kuashiria kipindi cha rutuba. Unaweza kufuatilia joto lako la mwili baada ya siku zako za hedhi kufika kikomo. Wakati wa kupevuka kwa yai joto la mwilini huweza kuongezeka na kufikia kilele siku yai litakapopevuka
- Tazama ute unaotoka ukeni . Kwa kawaida mwanamke hutoa ute kutoka ukeni . Lakini hubadilika kwa rangi na mtiririko wakati yai linapevuka
Njia Asili Za Kuzuia Kutunga Mimba
Hizi njia hujulikana kufanya kazi lakini hakuna utafiti wa kisayansi kudhibitisha ufanisi wake:
- Papai: Wengi huamini ikiwa utafanya mapenzi bila kinga, kula papai mara mbili kwa siku kwa siku tatu au nne zinazofuatia kunaweza punguza uwezekano wako wa kubeba mimba
- Tangawizi: Hii huaminika kuchochea kipindi cha hedhi na kuzuia ujauzito. Kuweka tangawizi kwenye maji yaliyochemka kwa dakika tano kisha kuyakunywa mara mbili kwa siku

- Parachichi: Hii hujulikana kuzuia mimba kwa njia ya kiasili. Gramu 100 za parachichi zilizokaushwa huchemshwa kwenye maji na kuongeza kijiko kimoja cha asili
- Mtini uliokaushwa: Hizi husaidia katika mzungumko wa damu. Hakuna utafiti unaoonyesha kuwa kula mtini husaidia kuzuia ujauzito
- Mdalasini : Hiki ni kiungo kinachotumika kwenye vyakula. Lakini hujulikana kuchochea uterasi na kusababisha kutoka kwa mimba
- Kitimiri : Pia hujulikana kama njia mwafaka ya kuzuia ujauzito
- Mwarobaini : Kudunga tumbo la uzazi kwa kutumia mafuata ya mwarobaini huweza kuua mbegu za kiume. Na kula tembe za mwarobaini hupunguza uwezo wa mwanamume wakufanya mapenzi

- Nanasi : Hukisiwa kuwa nanasi ina uwezo wa kuzuia mimba. Kula nanasi mbichi kila siku kwa siku mbili hadi tatu baada ya kufanya mapenzi huzuia ujauzito
- Buckwheat : Hii hujulikana kuzuia kujipandikiza kwa yai kwenye tumbo la uzazi.
- Kiazi kikuu mwitu: Kula mara mbili kwa siku kwa mwezi mmoja huaminika kufanya kazi kuzuia kubeba mimba
Unapotumia njia yoyote ile kuepuka kutunga mimba kiasili baada ya ngono, ni vizuri kufahamu kuwa ni vyema kuzungumza na daktari wako. Hii ni iwapo unatafuta njia mwafaka ya kuzuia mimba kwa muda mrefu. Njia ama vyakula vilivyotajwa hapa juu havina ufanisi wa asilimia 100 ama kutokuwa na madhara. Vingine vina madhara yanayochukua muda kugunduliwa.
Soma Pia: Sifa Za Hedhi Baada Ya Mimba Kutoka Ikilinganishwa Na Hedhi Ya Kawaida