Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kueusha Ngozi Ya Mtoto Wako

Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kueusha Ngozi Ya Mtoto Wako

Njia salama na zenye afya za kueusha ngozi yako.

Watoto bila shaka ni warembo kweli kweli. Hakuna vitu virembo zaidi kuliko watoto, haijalishi rangi ya ngozi yao. Nyeusi, nyeupe ama ya hudhurungi; haijalishi rangi ambayo mtoto alizaliwa nayo, haibadilishi chochote. Kinacho jalisha kwa mzazi ni wema wa mtoto, afya, ukuaji na maendeleo yake. Wamama wapya wako tayari kujaribu mambo mapya kwa watoto wao. Wakati ambao jambo hili huenda likawa la kusisimua, lazima iwe salama pia. Kwa utaratibu, tume orodhesha baadhi ya matibabu ya kinyumbani ya kueusha ngozi ya mtoto wako. Tuna taka uwe na uwezo wa kufanya hivi bila kusababisha kukosa starehe kwa ngozi yako. Ngozi ya mtoto wako ni nyeti sana na huenda ikapata maambukizo. Kutoka wakati watoto wanapo zaliwa, iwapo unaweza watunza vyema, ni njia bora ya kuwapa zawadi ya ngozi ya kupendeza maishani mwao mote. Je, ungependa kujua zaidi kuhusu vidokezo hivi vya kuifanya ngozi ya mtoto wako ing'ae?

Tazama Matibabu Haya ya Kinyumbani Ya Kueusha Ngozi Ya Mtoto Wako:

Masi Ya Kawaida Ya Mafuta Moto

home remedies for baby skin whitening

Masi za mafuta moto mafuta ya oliveama mafuta ya nazi ni bora zaidi kwa ngozi yako.

Ukitumia viganja vyako, pasha moto mafuta na uyasugue kwenye ngozi ya mtoto wako kwa upole. Mafuta haya yana julikana ku ipa ngozi unyevu, kulinda na kuboresha ngozi ya mtoto wako. Zina ipa unyevu mwingi na kuilinda ngozi na seli za mtoto. Zina sawasisha mafuta kwenye seli za ngozi na kuiwacha ngozi iking'aa na kuwa nyeupe. Mafuta ya nazi ni hiari njema ya kujaribu kama mafuta ya masi. Ina boresha ngozi ya mtoto wako na kuifanya ing'ae. Ni mojawapo ya njia ya kueusha mtoto wako.

Mlishe mtoto wako matunda

kueusha ngozi ya mtoto wako

Hakuna kitu kama kumlisha mtoto wako matunda freshi ili apate ngozi inayo ng'aa. Matunda yamejazwa na virutubisho, fiber na yana saidia kusafisha mwili wa mtoto wako kutoka ndani. Huku kuna saidia kwa kuimarisha afya yote ya ngozi. Sharubati ya zabibu imedhibitika kuwa dawa bora katika kuimarisha sura ya mtoto wako. Sharubati iliyo tolewa kwa zabibu asili inasafisha ngozi ya juu na kuicha ikiwa laini na inayo ng'aa. Pia unaweza tumia matunda mengine kama vile tufaha kueusha ngozi ya mtoto wako.

Matibabu Ya Nyumbani Ya Kuesha Ngozi Ya Mtoto Wako

kueusha ngozi ya mtoto wako

Maski za mwili ni bora za kuimarisha ngozi ya mtoto wako na kuilinda kutokana na maambukizi. Mojawapo ya bodypacks bora zaidi za mtoto ni mchanganyiko wa maziwa na turmeric. Pia kuna nyanya, oatmeal na curd.

Maziwa ni bidhaa bora kwa kueusha ngozi ya mtoto kwani ina wingi wa Vitamini A inayo saidia kutengeneza seli mpya zenye afya. Changanya turmeric na maziwa na utumie mchanganyiko huu kwenye uso na mwili wa mtoto wako. Paka mchanganyiko huu kwenye ngozi ya mtoto wako na uiache kwa dakika 10. Kisha, kwa upole uipanguze kwa kutumia taulo safi yenye unyevu nyevu. Baada ya kupanguza mchanganyiko huo, msafishe mtoto wako bila kumpaka sabuni kwenye ngozi sehemu ambazo ulikuwa umempaka mchanganyiko huo. Ngozi itang'aa baada ya hayo. Mchanganyiko huu unasaidia kueusha ngozi ya mtoto wako na kutoa uchafu wowote.

Fanya hivyo na mchanganyiko wa nyanya, curd na oatmeal.

Maji ya mtoto ya kuoga inapaswa kuwa na joto ya kawaida

kueusha ngozi ya mtoto wako

Joto ya maji unayo yatumia kumwosha mtoto wako ni muhimu sana katika hali ya ngozi yake. Hakikisha kuwa maji hayo sio baridi sana na wala hayana joto jingi. Tumia maji yenye joto ya kawaida ambayo haitamfanya mtoto kukosa starehe. Joto jingi sana huenda ikafanya ngozi ya mtoto kukauka na kuwa nyeusi na inaweza iharibu kwani bado ni nyeti sana.

Usitumie sabuni

home remedies for baby skin whitening

Usiwai tumia sabuni inayo patikana kwenye duka kwa ngozi ya mtoto wako. Sabuni hizi hazina upole kwenye ngozi na zinaweza ikausha. Badala yake, tumia bidhaa asili za usafishaji wa ngozi kama vile gram flour, inayo boresha mguso wa ngozi. Sabuni zina ukali na zimejazwa na kemikali zinazo fanya ngozi ya mtoto wako kukauka na kuwa nyeusi. Unaweza tumia glycerin kuosha mtoto wako.

 Matibabu Ya Nyumbani Ya Kuchungwa Ngozi Ya Mtoto: Moisturizer laini

kueusha ngozi ya mtoto wako

Kutumia moisturizer ni lazima. Inasaidia maji ya mwili kubaki kwenye ngozi ya mtoto na kuiepusha kukauka. Chagua moisturizer iliyo na upole kwenye ngozi ya mtoto. Unashauriwa kupaka moisturizer kwenye mtoto wako baada ya kila masaa 4 kupata matokeo bora zaidi.

Hakikisha mtoto wako ana maji tosha mwilini

Kunywa maji kuna hakikisha anatoa vitu visivyo faa mwilini, na ni sawa kwa mtoto wako. Walakini, angalia na daktari wako kiasi kifaacho chake.

Weka tahadhari hizi akilini
  • Wakati wote, shughulikia ngozi ya mtoto wako kwa upole. Usiisugue mbio sana ama kwa nguvu.
  • Usiwache ngozi yake ikiwa na maji. Ikaushe kwa kutumia taulo iliyo safi na laini.
  • Usitumie bidhaa za watu wazima kwenye ngozi ya mtoto wako.
  • Wakati wote fanya kipimo cha bidhaa unazo taka kutumia kwenye ngozi ya mtoto wako kwa kupaka kiasi kidogo kwenye sehemu ndogo ya ngozi yake.
  • Tia akilini hali ya anga na ubadilishe utunzi wa ngozi ya mtoto wako ifaavyo.
  • Mvalishe mtoto wako nguo safi, zenye kumstarehesha na zinazo mkubalisha kupumua kuepuka kuto hisi vyema kwa ngozi yake.

Ngozi nzuri ni thibitisho ya afya yako. Mfanyie mtoto wako jambo la busara na ufuate vidokezo tulivyo angazia hapa juu kuhakikisha ana ngozi nzuri sasa na siku za usoni.

Kumbukumbu: Stylecraze.com

Soma pia: Top Melanin Popping Skincare Products For Your Family

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio