Je, nitajuaje iwapo ananithamini? Anataka uhusiano wa kweli ama ananichezea kisha aniwache baada ya miezi michache? Kuna wanaume wanaokuwa katika uhusiano na wanawake kwa muda mrefu bila kuwa na mipango ya kimaisha nao. Kufahamu ikiwa mwanamme anakuthamini katika uhusiano ama la kutakusaidia kuondoka kwenye uhusiano usio na maana. Na kuepuka kuvunjwa moyo baada ya kuwekeza hisia zako.
Kufahamu iwapo mwanamme anakuthamini katika uhusiano

1.Hazungumzi usipozungumza
Mazungumzo ni muhimu katika uhusiano wowote na hasa kwa mwanamme anayeogopa kukupoteza, atakuwa na jitihada za kuzungumza nawe. Itakuwa sehemu ya siku yake. Ikiwa mpenzi wako hafanyi hivi, na hazungumzi usipomwongelesha, huenda kukawa na shida.
2. Hapangi dates
Ikiwa mwanamme anakupenda, atapanga dates apate kukujua zaidi na kuwa na wakati nawe. Lakini iwapo mpenzi wako hana muda wako na wala hatii juhudi kukuona, anakuzungumzia anapotaka kufanya mapenzi nawe, bila shaka hakupendi na hana mipango ya kimaisha nawe.
3. Haoni wivu
Kuna uwezekano wa mwanamme anayekupenda na mliye katika uhusiano naye kutosikia wivu? Hata wanaume wengine wanapokutazama ama kutaka kuzungumza nawe. Unapokuwa na mpenzi, ataona wivu hata watu wengine wanapokusalimia na atatafuta sababu ya kukukasirikia na kukumbusha kuwa anakupenda na hapendi wengine wanapokuangalia. Hata kama hawezi fanya jambo lolote kuwafanya wengine wasikuangalie.
Ikiwa mpenzi wako haoni wivu hata unapoenda nje na kuchelewa, huenda anataka wakati mzuri tu.

4. Hakuiti mchumba wake
Mwanamme anapokupenda atakuwa na uhakika anachotaka nawe. Kama kuzungumza na kukuuliza iwapo ungependa kuwa mchumba wake. Lakini asipokuuliza swahili hili na kuwacha mambo yaendelee bila mpango, nafasi kubwa ni kuwa hakupendi kama unavyofikiria.
5. Hakuonyeshani kwa marafiki zake
Kuna mitandao mingi ya kijamii ambayo wapenzi wanatumia kuonyeshana mapenzi yake. Huenda asikuweke kwenye mitandao yote. Lakini iwapo hakuonyeshani hata kwa mtandao mmoja, na kila unapomwuliza anasema kuwa anapenda kuweka mapenzi siri, huenda ikawa kuna vitu anaficha.
Asipojaribu kuonekana nawe kwa marafiki zake ama kuenda kwenye sherehe za kijamii na kikazi na wewe, nafasi kubwa ni kuwa hakupendi kama unavyompenda.
Kuangalia matendo ya mwanamme katika uhusiano wa kimapenzi kutakusaidia kufahamu iwapo mwanamme anakuthamini katika uhusiano ama la. Pia, msipokuwa na shauku sawa na kinachowaleta pamoja ni kitendo cha mapenzi, bila shaka hakuthamini katika uhusiano na haoni maisha marefu nawe.
Soma Pia: Mambo 6 Hasi Katika Ndoa Ambayo Wanawake Hufanya Yanayo Haribu Uhusiano Wao