Wakati 5 Unapo Paswa Kufanya Kipimo Cha Mimba

Wakati 5 Unapo Paswa Kufanya Kipimo Cha Mimba

Kukosa kupata kipindi chako cha hedhi kwa zaidi ya mwezi mmoja ni baadhi ya ishara kuu kuwa unapaswa kufanya kipimo cha mimba.

Kipimo cha mimba huwa na matokeo sahihi kinapo fanyika wiki moja baada ya mwanamke kukosa kipindi chake cha hedhi. Kufuatia teknolojia zinazo zidi kuimarika, kuna uwezekano wa mwanamke kufanya kipimo na kupata matokeo siku 14 baada ya tendo lake la ndoa bila kinga. Ikiwa una shaka kuwa huenda ukawa na mimba, tuna kudokezea wakati muhimu unapo stahili kufanya kipimo cha mimba.

Wakati wa kufanya kipimo cha mimba

kufanya kipimo cha mimba

  1. Unapo kosa kipindi chako cha hedhi

Wanawake wengi huwa na mzunguko wa hedhi wa siku 28, na usipo kuwa makini na siku hizi, huenda ikawa ni vigumu kwako kufahamu ikiwa umechelewa ama umepata kipindi chako siku inayofaa. Ikiwa imekuwa zaidi ya mwezi mzima bila kupata kipindi chako, hakikisha kuwa unachukua kipimo cha mimba.

Kuna sababu tofauti ambazo huenda zikafanya kipindi chako kichelewa bila kuwa mjamzito. Kama vile kukwazwa kimawazo, kubadili lishe yako, kuchukua lishe duni, kubadili hali ya anga ama kufanya mazoezi kwa sana.

2. Unahisi kuumwa na tumbo

home remedies for leg cramps

Yai lililo rutubishwa linapo jipandikiza kwenye mirija ya uterasi, utahisi uchungu sawa na wa vipindi vya hedhi. Katika siku za kwanza za ujauzito, huenda ukahisi aina ya uchungu tumboni na kudhania kuwa unakaribia kupata hedhi. Ila, hauta shuhudia kipindi chako. Unapokuwa na shaka, ni vyema kufanya kipimo cha mimba.

3. Kuumwa na matiti

Punde tu unapo tunga mimba, mwili huanza kutoa homoni za estrogen na progesterone ili kuutayarisha mwili kuegemeza mtoto. Matiti ya mama yata anza kuongezeka kwa saizi, kuwa laini na kuuma.

Ishara hii ni sawa na mwanamke anapo karibia kupata kipindi chake cha kila mwezi kwani matiti huhisi kuuma. Usipo kuwa na uhakika kuhusu hali yako, ni vyema kuchukua kipimo kudhihirisha hali yako ya mimba.

4. Una hisi mabadiliko mwilini

Huenda uka hisi kuwa mwili wako una ishara zisizo za kawaida. Kama vile kuhisi kichefu chefu, kuchukia chakula ulicho kipenda huku matamanio ya chakula kingine yakizidi, uchovu na kuumwa na mgongo.

Wakati 5 Unapo Paswa Kufanya Kipimo Cha Mimba

5. Kufeli kwa mbinu ya kudhibiti uzalishaji

Mbinu nyingi za kudhibiti uzalishaji hazina uhakika wa asilimia 100 kulinda dhidi ya kutotunga mimba. Kuna kiwango kidogo cha mwanamke kupata mimba hata anapo tumia mbinu tofauti za kudhibiti uzalishaji.

Ukihisi kuwa una shaka mbinu uliyo tumia kujikinga dhidi ya magonjwa na kupata mimba, ili feli, ni vyema kufanya kipimo.

Hitimisho

Wanawake wanao jihusisha katika tendo la ndoa bila kujikinga huwa na nafasi ya kupata mimba kila mwezi. Unapokuwa makini na mwili wako, utagundua ishara za kipekee za kukuashiria kuwa unapaswa kuchukua kipimo cha mimba.

Unapokosa kupata kipindi chako, hakikisha kuwa unchukua kipimo cha mimba kubainisha hali yako. Unaweza tembelea kituo cha afya ama kujifanyia kipimo hiki nyumbani.

Soma Pia: Kwa Nini Kupima Mimba Mapema Sana Hakushauriwi?

Written by

Risper Nyakio