Jinsi Ya Kufurahia Mapenzi Baada Ya Kujifungua Kupitia Upasuaji Wa C-section

Jinsi Ya Kufurahia Mapenzi Baada Ya Kujifungua Kupitia Upasuaji Wa C-section

Kufanya mapenzi baada ya kujifungua kupitia upasuaji wa c-section sio jambo rahisi. Mama anapaswa kuwa mpole na mwili wake hadi apone.

Ikiwa wewe ni miongoni mwa wamama walio barikiwa na watoto wao kupitia upasuaji wa c-section na bado unazidi kupona, kurudia shughuli za kitandani sio fikira uliyo nayo katika wakati huu. Hata hivyo, huenda bado ukashangaa wakati ambapo itakuwa salama kwako kuanza kufanya mapenzi. Watu wengi hufikiri kuwa kujifungua kupitia upasuaji kuna maana kuwa hautakuwa na matatizo mengi kuanza kufanya mapenzi baada ya c-section. Ila huu sio ukweli, sawa na mama wanao jifungua kupitia njia asili ya uke, wote wana tatizika na kushuhudia matatizo ya kimapenzi.

Lini salama kuanza kufanya mapenzi baada ya c-section?

kufanya mapenzi baada ya c-section

Hakuna wakati dhabiti wa kungoja kabla ya kurudia matendo yenu ya kitandani. Ila, wanawake wengi hungoja angalau wiki 4 ama 6 kabla ya kurejelea matendo ya wanandoa. Kuna uwezekano kuwa walio pitia upasuaji hawatavuja damu sana, lakini itachukua muda wa angalau wiki 6 kwa kizazi chako kufungana. Kumbuka kuwa kipindi kila mwanamke anacho ngoja ni tofauti.

Mambo ya kutarajia unapo pona na kufanya mapenzi baada ya upasuaji

Uponaji baada ya upasuaji wa c-section

Baada ya kujifungua, utabaki hospitalini siku mbili hadi nne ili upone vyema. Na kuvuja damu kupitia kwa uke kutashuhudiwa kwa wanawake wote huku uterasi ikirejelea saizi yake ya kawaida. Na itachukua muda wa wiki sita na kwa kizazi chako kufungana tena. Baada ya kujifungua, epuka kufanya mapenzi hadi mwili wako upone. Wanawake wengi walio pitia upasuaji wanaweza rejelea kufanya mapenzi baada ya kukubalishwa na daktari baada ya wiki sita.

Kuwa na starehe

Nyuzi baada ya upasuaji zitatolewa baada ya wiki moja. Na kidonda kuzidi kupona kwa muda hadi wiki sita. Sehemu uliyo pasuliwa huenda ikawa na uchungu kwa hivyo ni vyema kujitenga na vitendo vyovyote vya kingono kuepuka kushinikiza sehemu hiyo zaidi. Kumbuka kuwa mapenzi sio ya kifizikia tu, mbali hisia na kiakili. Kwa hivyo, hakikisha una wasiliana na mchumba wako na kumwambia shaka zako.

kufanya mapenzi baada ya c-section

Kudhibiti uzalishaji

Unapo enda kukaguliwa baada ya wiki 6, hakikisha kuwa mna jadili mbinu za kudhibiti uzalishaji na utumie mbinu itakayo kufaa zaidi. Kuepuka kupata mimba ingine kabla ya mwili wako kupona.

Wakati wa kurudi hospitalini

Zungumza na daktari wako ikiwa una hisi uchungu zaidi, ama kuvuja damu baada ya upasuaji wa c-section. Kidonda chako kinapo funguka, ama kuvimba. Huenda ukawa na maambukizi.

Hitimisho

Inapo fika kwa kufanya mapenzi baada ya upasuaji wa c-section, chukua muda wako kupona na kuwa mwangalifu kwa mwili wako. Hakuna mbio za kurejelea matendo ya wanandoa. Utahitaji wakati kuzoea kufanya mapenzi baada ya kupona.

Mkikabiliana na matatizo yoyote, hakikisha kuwa mna mjuza daktari wenu ili awasaidie.

Soma PiaVidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Written by

Risper Nyakio