Kufanya Mapenzi Baada Ya Kupata Watoto: Jinsi Ya Kuendeleza Hamu Kati Yenu

Sababu kwa nini kufanya mapenzi baada ya kupata watoto hupunguka na jinsi ya kuregesha utangamano asili ulio kuwa kati ya wanandoa.
Kupata watoto hubadilisha mambo mengi, ikiwemo maisha yenu ya kimapenzi. Wazazi wengi wanafahamu kuwa kufanya ngono mara chache zaidi ni sehemu ya maisha mapya na mtoto. Lakini ungetarajia kuwa baada ya watoto kukua mambo yangebadilika na wazazi kuanza kufanya mapenzi kama hapo awali, ila, la. Kulingana na utafiti, wanandoa walio na watoto wenye umri mkubwa hufanya ndoa mara chache zaidi ikilinganishwa na walio na watoto wachanga. Mbona kufanya mapenzi baada ya kupata watoto kuna badilika?
Ukweli Kuhusu Kufanya Mapenzi Baada Ya Kupata Watoto
Ngono baada ya kujifungua haina ladha sana
Watu wengi huamini kuwa uchungu wa ngono baada ya watoto huwa kiwewe baada ya kujifungua. Na huenda ikawa, ila, mara nyingi huwa kufuatia viwango vya chini vya estrogen vinavyo athiri uwezo wa kupanuka wa tishu za uke.
Kuna sababu nzuri kwa nini huna hamu ya mapenzi baada ya kujifungua
Kukosa usingizi, mabadiliko kati yako na mchumba wako na huenda hata ukawa na hisia hasi kuhusu mwili wako mpya. Hizi zote sio fikira za kukupatia hamu ya kufanya mapenzi. Ikiwa una nyonyesha, itakuwa ngumu zaidi. Kwani unatoa kichocheo cha oxytocin kinacho kufanya umpende mwanao na kushusha viwango vyako vya hamu ya mapenzi.
Mapenzi ni muhimu sana sasa
Ikiwa hamfanyi mapenzi, mtaanza kuhisi kana kwamba nyinyi ni mandugu, na sio jambo nzuri. Kuhisi kuwa hamna utangamano huenda kuka sababisha chuki kati yenu. Anzeni kwa kugusana kwa njia ya kimapenzi na mabusu na mtie juhudi kurejesha maisha yenu ya kimapenzi baada ya kupata watoto.
Utahitaji mapenzi tena
Sawa na vile utakavyo lala tena, kuanza kuenda kuburudika na marafiki wako tena na hata kuwa na mawazo ya kujifungua tena, uta hisi hamu ya kufanya mapenzi tena. Jipe wakati wa kupona na wa kuzoea majukumu yako mapya. Mwelezee mchumba wako kinaga ubaga na ukumbuke kuwa kuna baadhi ya wakati ambapo hautakuwa na hamu. Lakini utafurahi kuwa uliyafanya baadaye. Kadri na vile ambavyo unaweza dhania, kupata watoto zaidi sio sawa na kuto fanya mapenzi vya kutosha.
Jinsi ya kuboresha maisha yenu ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua
Msingoje usiku
Mojawapo ya sababu kwa nini kufanya mapenzi huwa ngumu baada ya watoto ni kwa sababu wazazi hungoja usiku kama kawaida yao. La, mna muda mwingi mchana na asubuhi.
Kuoga pamoja
Kuoga pamoja wakati wa mchana kunawasaidia kuhisi mna utangamano. Kwa hivyo ikiwa watoto hawaja amka asubuhi, ingieni bafu mkoge pamoja.
Tenga wakati wenu
Kwa wazazi walio na watoto wenye umri mkubwa, kukosa usiri wenu na kukosa wakati tosha wa kuwa pamoja huwa maarufu. Hakikisheni kuwa mnatenga wakati wakuwa peke yenu.
Chanzo: Parents