Kufanya Tendo La Ndoa Kila Siku Kuna Manufaa Gani Kwa Afya Yako?

Kufanya Tendo La Ndoa Kila Siku Kuna Manufaa Gani Kwa Afya Yako?

Kufanya mapenzi kila siku katika ndoa kuna boresha uhusiano wenu na kufanya utangamano wenu uwe bora zaidi.

Kufanya mapenzi kila siku sio jambo nadra kwa walio funga pingu za maisha hivi karibuni ama wanandoa katika siku za mapema za uhusiano wao. Hawatosheleki kuwa pamoja wakati wote. Kwa hivyo tendo la ndoa ni jambo asili linalo tosheleza.

Lakini muda unapo pita, hisia za kufanya ngono wakati wote zinapungua. Kazi huingilia ufanyaji ngono wenu. Kisha mnapata watoto, na majukumu yenu yana badilika. Ama wakati mwingine mmechoka sana kufanya ngono baada ya siku mrefu ya kufanya kazi.

Baadhi ya wakati, hii ni sawa na mnaweza pata wakati wenu wikendi ama likizo. Lakini wakati mwingine, huenda ikawa vigumu kwa ndoa yako mnapokosa wakati wenu wa kipekee na kufanya mapenzi na mchumba wako.

Kwa hivyo, mwandishi wa Umarekani na mama wa watoto watatu Brittany Gibbons aliamua kufanya majaribio kwa kufanya ngono na bwana yake kila usiku kwa mwaka mzima.

Na haya ndiyo alisoma kutokana na hilo.

kufanya mapenzi kila siku

Mambo 3 yanayo fanyika mwilini mwako na akilini baada ya kufanya mapenzi kila siku

  1. Kuboresha ujasiri wako

Unapo fanya kitu kwa muda mrefu, kinakuwa na uzoefu. Lakini hutaki kufanya mapenzi kuanze kukosa ladha. Kwa hivyo lazima utie juhudi ili kufanya ngono kuwe na ladha. Baada ya wakati, ujasiri wako utaongezeka.

Brittany anaeleza kuwa baada ya mtoto wake wa tatu, hakuhisi starehe kuwa uchi. "Nilizima sitima wakati wa tendo la ndoa, nikaficha tumbo na chuchu kwa mavazi mepesi, na kungoja mume wangu atoke chumbani kabla ya kutoka kwenye bafu hadi kwenye chumba cha kuvalia," alisema.

Baada ya kuzungumza na rafiki yake, aliamua kufanya tendo la ndoa kila siku kwa mwaka ili kujilazimisha kupenda mwili wake mpya. Na akazoea hisia za kuwa uchi na kuguswa na bwana yake baada ya miezi michache katika jaribio lake. Hakujipata akijificha tena.

2. Unaanza kutazamia tendo hilo

kufanya mapenzi kila siku

Mama, huenda ukaweza kuelewa Brittany anacho sema kuhusu kuto kuwa na starehe na mwili wake. Wanawake wengi huhisi wana hofu kuhusu wanavyo kaa. Na kuathiri maisha yao ya kingono. Lakini unapofanya mapenzi kila siku, utaanza kutazamia kufanya tendo hilo.

3. Kubadilisha uhusiano wenu

Kufanya tendo la ndoa kila siku kutabadilisha jinsi uhusiano wenu ulivyo. Baada ya miezi michache ya kufanya mapenzi na mume wake kila siku, Brittany alisema kuwa uhusiano huo wa kila mara ulianza kuonekana nje ya chumba cha kulala.

"Tuna mapenzi zaidi kama wanandoa, kugusana mikono tunapo pitana, kumbusiana zaidi baada ya kazi na sio peck tu. Uhusiano wetu una nguvu zaidi na ndoa yetu inafuzu."

Wanandoa wanapaswa kufanya mapenzi kila siku wanapo hisi kuwa wameanza kutengana.

Chanzo: News.com.au

Soma PiaJinsi Ya Kuanzisha Tendo La Ndoa Na Mumeo Ili Kuibua Cheche Katika Ndoa Yenu

Written by

Risper Nyakio