Kuna imani nyingi zinazozingira kufanya mapenzi kupata mimba. Katika makala haya, tunaangazia imani hizo na mambo ambayo wanandoa wanapaswa kufahamu.
Kufanya mapenzi kupata mimba
- Wakati bora kushika mimba

Wakati bora kushika mimba ni katika kipindi cha rutuba. Kupevuka kwa yai hufanyika mara moja kwa mwezi. Siku mbili kabla na siku mbili baada ya siku hii, mwanamke huwa na nafasi za juu kushika mimba. Mbegu za kiume zina uwezo wa kuwa hai kwa kipindi cha siku tano, huku yai likidumu kati ya masaa 12 hadi 24.
2. Jinsi ya kufahamu siku ya kupevuka kwa yai
Vipindi vya mzunguko wa hedhi hubadilika na kufanya iwe vigumu kufahamu siku hasa kama siku ya kupevuka kwa yai kila mwezi. Kuna apps zinazo saidia kujua siku ya kupevuka kwa yai. Kuangalia ishara za kabla ya kupevuka kwa yai kunasaidia kufahamu siku za hatari zenye nafasi ya juu ya kushika mimba.
3. Mara za kufanya mapenzi ili kushika mimba
Kufanya mapenzi mara nyingi kunaongeza nafasi za kupata mimba. Hakuna mara za kupindukia inapofika kwa kufanya ngono kushika mimba. Jambo muhimu ni kuzingatia siku za hatari ama siku chache kabla na baada ya kupevuka kwa yai.
4. Kufanya mapenzi kila siku ni vibaya?

Tumekubaliana kuwa mnaweza kufanya mapenzi mara nyingi mtakavyo. Hata hivyo, kufanya mapenzi ni tendo linalopaswa kuwa la furaha. Msihisi kana kwamba mnafanya kazi ama jukumu la lazima. La hasha, jambo la mapenzi kati ya wapenzi linapaswa kuwa tendo lenye furaha na la kuboresha utangamano.
5. Kuna wakati spesheli wa kufanya mapenzi mchana?
Usingizi umedhihirishwa kusaidia kuongeza ubora wa manii. Kwa hivyo ikiwa mnashangaa wakati bora wa kufanya mapenzi kupata mimba, asubuhi ndiyo wakati bora kwenu. Kabla ya kuenda kazini ama kuanza siku, chukueni fursa hiyo kufanya wapendanao wafanyavyo kuongeza nafasi zenu za kupata mimba kirahisi.
6. Inachukua muda upi kushika mimba?
Kutunga mimba hufanyika siku sita baada ya ngono, yai linaporutubishwa na manii kutoka kwa mwanamme. Yai linarutubishwa kwenye mirija ya ovari kisha linasafiri hadi kwenye uterasi ya mama linapojipandikiza na ujauzito kuanza.
7. Matatizo kushika mimba

Kabla ya kukata tamaa baada ya kujaribu kwa miezi mitatu bila kufanikiwa, kumbuka kuwa, inachukua hadi miezi sita kutunga mimba. Ikiwa hauna matatizo yoyote ya kiafya, usife moyo, jipe hadi mwaka mmoja.
8. Kuongeza nafasi za kushika mimba
Wanandoa wanaweza kupuuza afya yao wanaposhughulika na kutunga mimba. Afya bora inachangia pakubwa katika kushika mimba kwa urahisi. Zingatia mitindo yenye afya ya maisha kama kufanya mazoezi, kupunguza ulevi, kaffeini na kula chakula chenye afya.
9. Wakati wa kumwona daktari
Ikiwa baada ya mwaka mmoja wa kujaribu kushika mimba hamjafanikiwa, ni wakati wa kuzungumza na mtaalum wa masuala ya uzalishaji.
Kufuatia teknolojia katika nyanja ya kiafya, kuna njia tofauti ambazo wanandoa wanaweza kutumia kupata mtoto.
Soma Pia: Jinsi Ya Kushika Mimba Kwa Kasi Kwa Muda Chini Ya Miezi Miwili