Wanandoa wajawazito mara nyingi hushangaa ikiwa ni salama kufanya mapenzi ukiwa na mimba. Kuta hatarisha maisha ya mtoto? Mimba inaweza haribika? Kuna mitindo salama ya kufanya ngono katika kipindi hiki? Hapa kuna ujumbe wote unao hitaji kujua kuhusu haya.
Je, ni salama kufanya mapenzi ukiwa na mimba?

Ngono ni tendo asili kwa wanandoa na katika ujauzito, kama mimba yako ni ya kawaida na haina hatari yoyote. Kufanya ngono katika ujauzito hakuta mwathiri mtoto kwa njia yoyote ile. Kwani amelindwa na kuta za uterasi na gunia la amniotic fluid.
Kubanwa mwanamke anapo fika kilele sio sawa na kubanwa wakati wa uchungu wa uzazi. Lakini, madaktari wengi huwa shauri wanawake kutofanya ngono katika wiki za mwisho kabla ya kujifungua. Ili kuepuka kuanza kushuhudia kubanwa kabla ya wakati. Kuna imani kuwa, manii huwa na kichocheo kinacho fanya mlango wa uke kuiva na mwanamke kuanza kushuhudia kubanwa kwa uchungu wa uzazi. Huku madaktari wengine wakiamini kuwa hizi ni imani tu zisizo kuwa na msingi.
Kuna nyakati ambazo sio salama kwa mama kufanya mapenzi katika mimba kama vile:
- Una hatari ya kupoteza mimba ama una historia ya kupoteza mimba
- Uko katika hatari ya kujifungua kabla ya wakati
- Una shuhudia kuvuja damu kutoka kwa uke, ama kuumwa na tumbo bila chanzo chake kujulikana
- Gunia lako la amniotic fluid lina vuja
- Mlango wako wa uke umefunguka mapema katika ujauzito
- Una mimba ya mtoto zaidi ya mmoja
Tendo la wanandoa katika ujauzito

Kila mwanamke hushuhudia jambo tofauti na mwingine katika ujauzito. Hisia za hamu ya tendo hili katika kipindi hiki pia hutofautiana. Kwa wengine, hamu ya tendo la wanandoa hupungua ama kuisha, huku wengine wakishuhudia ongezeko la hamu la kitendo hiki. Haya yote ni sawa kwani vichocheo hubadilika mwilini, na huenda wanawake wengine waka hisi kuwa hawana ujasiri na miili yao katika ujauzito.
Ni vyema wanandoa kuwa na mazungumzo wazi kuhusu tendo la kimapenzi na hisia zao. Hakikisha kuwa mitindo mnayo tumia mnapokuwa wajawazito ina starehesha mama na hashinikizi mgongo ama tumbo yake.
Ikiwa hauna uhakika kuhusu historia ya kingono ya mpenzi wako, hakikisha kuwa mnatumia kondumu ili kujilinda dhidi ya maambukizi ya kingono na ukimwi.
Chanzo: healthline
Soma Pia: Mambo Ya Kufanya Mapenzi Yanapo Isha Katika Ndoa