Mama anapokuwa na mimba, lengo lake kuu ni kuwa na afya na kumchunga mwanawe anayekua kwenye uterasi. Kufanya mazoezi katika ujauzito ni mojawapo ya mambo makuu ya kufanya ili kuhakikisha kuwa mtoto ana afya bora. Mazoezi katika ujauzito yanasaidia katika:

- Kumpa mwanamke mjamzito nishati
- Kupunguza hatari ya magonjwa ya kimoyo
- Kuponya maumivu ya mgongo
- Kudhibiti uzito wa mama na mwanawe
- Kupunguza uvimbe mwilini katika mimba
- Kuboresha ubora wa usingizi
- Kuboresha mzunguko wa damu mwilini
Kufanya mazoezi mama anapokuwa na ujauzito humpa mtoto chanzo chenye afya maishani mwake.
Vidokezo vya kuwasaidia wanawake wenye mimba katika mazoezi

- Kibali kutoka kwa daktari wako
Kulingana na afya ya mama, daktari wake atakushauri mazoezi bora na unayopaswa kujitenga nayo. Kufanya aina fulani ya mazoezi katika wakati usiofaa huenda kukasababisha matatizo ya kiafya. Kabla ya kuanza kufanya mazoezi katika mimba, ni vyema kwa mama kuwasiliana na daktari wake.
2. Epuka mazoezi
Iwapo kabla ya kutunga mimba mama alikuwa mchezaji mashuhuri, katika michezo kama vile kadanda ama mpira wa vikapu. Wakati wa mimba ni nyeti na ni wakati wa kulinda kiumbe kinachokua tumboni mwa mama. Mama anapaswa kujiepusha na michezo na mazoezi yanayohusisha kuruka na kugeuka kwa kasi.
3. Usifanye mazoezi kwa muda mrefu
Mazoezi ni bora, ila mama anapofanya mazoezi zaidi ama kwa muda mrefu, anahatarisha maisha ya mtoto. Pumzika unapochoka na usifanye mazoezi kwa muda mrefu.
4. Kuwa na uthabiti
Kufanya mazoezi kwa dakika 15 mara nne ama tani kwa siku ni bora kuliko kufanya mazoezi ya masaa matatu mara moja kwa mwezi. Mwili unahitaji mazoezi kwa mara thabiti.
5. Kujitayarisha kwa mazoezi
Fanya mazoezi ya kabla ama warm up kabla ya kuanza mazoezi yako. Ili kuepuka kuumwa na mbavu ama maumivu kwenye misuli.
Hitimisho
Mazoezi ya wastani ni muhimu kwa wanawake wajawazito, lakini lazima wachague mazoezi yaliyo salama kwao na yaliyopitishwa na madaktari wao. Mazoezi pia yanapaswa kuwa rahisi na yasiyo shinikiza tumbo. Hivi ni baadhi ya vidokezo muhimu kuangazia katika kufanya mazoezi katika ujauzito kwa mama mjamzito.
Soma Pia: Kunyonyesha Mtoto Mdogo: Manufaa Kwa Mtoto Na Mama