Hizi Ndizo Sababu Kwa Nini Unaongeza Uzito Hata Baada Ya kufanya Mazoezi

Hizi Ndizo Sababu Kwa Nini Unaongeza Uzito Hata Baada Ya kufanya Mazoezi

Kufanya mazoezi na kuongeza uzito ni mojawapo ya mambo yanayo tia wasiwasi zaidi. Hasa unapo kazana kupunguza uzito. Tazama chanzo cha jambo hili.

Una ratiba yako ya kufanya mazoezi ama unjiunga na darasa la kufanya mazoezi karibu nawe ili kuanzisha safari yako ya kutimiza malengo yako ya kupunguza uzito. Siku zinapita kwenye chumba cha mazoezi, na ungali huoni matokeo yoyote, ila, huenda ukawa unaongeza uzito zaidi. Hapa kuna baadhi ya sababu kwa nini unashuhudia kufanya mazoezi na kuongeza uzito.

Sababu Zinazo Sababisha Mtu Kufanya Mazoezi Na Kuongeza Uzito

kufanya mazoezi na kuongeza uzito

Je, umekuwa ukifanya mazoezi na kula chakula bora, lakini unapo simama kwenye uzani, inasema umeongeza uzito zaidi? Bila shaka, hauko peke yako.

Kufanya mazoezi ni vigumu ya kutosha,  bila hisia zinazo endana na kusimama kwenye uzani na kupata kuwa nambari zinaenda tofauti na unavyo kusudia. Hali hii ni ya kutia wasiwasi na kuvunja moyo.

Unajaribu kufikiria unacho kifanya vibaya. Usitie wasiwasi! Mabadiliko haya kwenye uzani haya maanishi kuwa unafanya chochote isivyo faa. Kuna baadhi ya sababu kwa nini unazidi kuongeza uzito ukifanya mazoezi.

Haupaswi kushtuka kufuatia uzito unaozidi kuongezeka unapozidi kuishi maisha  bora, kwa kula unavyo paswa na kufanya mazoezi.

Tazama sababu zinazo sababisha hili

kufanya mazoezi na kuongeza uzito

  1. Maji kubaki mwilini

Hii ni mojawapo ya sababu kwa nini uzito wako unazidi kuongezeka. Wakati tu ulipo dhani kuwa kunywa maji ni vizuri kwa afya yako, manufaa yake yanakuwa tofauti na ulivyo dhani. Maji huwa asilimia 65-90 ya uzito wa mtu, na tofauti ya kiwango cha maji mwilini mwa binadamu huenda kikasababisha uzito kwenda juu  mara kwa mara.

2. Kuongeza misuli

Bila shaka, tunafahamu kuwa unapo fanya mazoezi, unaongeza misuli. Unapo badilisha mwili wako ulivyo na kufanya mazoezi kwa kuongeza misuli iliyo mizito zaidi na kupunguza ufuta mwilini mwako. Uzani wako huenda ukaongezeka, wakati ambapo ufuta wa mwili wako utapunguka. Mabadiliko haya huenda yaka fanyika baada ya wiki na miezi sio masaa ama siku.

3. Jinsi mwili wako unavyo itikia

Jinsi mwili wako unavyo itikia ama kubadilika baada ya mazoezi huenda ikawa kuongeza uzito.

Kuanza kufanya mazoezi hakumaanishi kuwa mwili wako wakati wote utaanza kuonyesha mabadiliko kwa kasi. Mazoezi sio rahisi kwa mwili hasa ikiwa hapo awali haukuwa unafanya chochote na huenda mwili uka itikia kwa kuongeza uzito. Baadhi ya wakati, mwili wako unahitaji muda ubadilike. Usiwe makini sana na uzani.

Soma PiaUjauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

Written by

Risper Nyakio