Muundo wa familia umebadilika sana. Sasa hivi, ni kawaida kuona wazazi wawili wanaofanya kazi ikilinganishwa na zamani ambapo mume alikuwa anafanya kazi na bibi kubaki nyumbani. Hasa nchini Kenya ambapo gharama ya maisha inazidi kuenda juu kila uchao. Ni vigumu kwa nyumba kufanisi na mlezi mmoja. Kwa wanandoa, wazazi na walioleka hivi majuzi, lazima uende kazini pamoja na mchumba wako kila asubuhi. Hapa kuna vidokezo vya kufanya ndoa yako ifuzu, dhidi ya kuwa na kazi nyingi.
Kufanya Ndoa Ifuzu Dhidi Ya Kufanya Kazi
- Tumia wikendi vizuri

Watu wanaofanya kazi sana huchukua wikendi kama muda wao wa kupumzika. Ni wakati ambapo mtu anaweza kuwa na siku mbili za kupumzika bila kukatizwa. Siku za wiki humkwaza mtu na huenda ukafanya kazi mpaka usiku wa maanani ama kubeba kazi nyumbani. Wikendi ni muda ambapo wanandoa wanaweza kupata nafasi ya kuwa pamoja. Kwenda kwenye bahari, kula nje pamoja ama kutazama runinga kwa pamoja. Wazo ni kuwa na wakati na mchumba wako, kuzungumza naye na kumsikiliza pia.
2. Usilete kazi ya ofisini nyumbani
Ni muhimu kuheshimu nyumbani na wakati wa familia. Kazi ya ofisini haipaswi kubebwa nyumbani. Tengeneza muda wa kufanya kazi zako za ofisini bila kuzifanyia nyumbani. Unapofika nyumbani, huo ni wakati wa familia na kupumzika baada ya muda mrefu. Kufanya kazi za ofisini nyumbani kuna chukua muda ambao ungekuwa na mchumba wako, na watoto mkizungumza kuhusu siku zenu zilivyokuwa.
3. Gawana kazi ya nyumbani

Watu wawili wanapoishi pamoja na wote wanafanya kazi siku nzima, nani anayefanya kazi za kinyumbani? Ili kuepuka vita vya kinyumbani vya mara kwa mara na kutokubaliana kuhusu kugawana kazi za kinyumbani ni vyema kugawana kazi hizi. Isiwe ni vita kuhusu anayefanya kazi rahisi na anayefanya kazi ngumu. Badala yake, gawaneni kwa usawa. Unaposhindwa kufanya kazi zako, mweleze mchumba wako muda kabla.
4. Tenga wakati wa kuwa pamoja
Hata ikiwa siku za wiki zina kazi nyingi, ni vyema kwa wanandoa kutenga muda katika siku hasa ya wiki kuwa na wakati wao wa kipekee. Ni muhimu kwa wanandoa kukumbuka kuwa walikuwa na maisha na uhusiano kabla ya kupata watoto. Kwa hivyo wasikubali kuwa na watoto kufanye mkose muda wenu wa kipekee.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Sababu 5 Kwa Nini Wanandoa Huachana