Kufanya tendo la ndoa kila siku kwa wanandoa walio funga pingu za maisha tu, ama walio ingia katika uhusiano ni jambo la kawaida. Mapenzi yamenoga na mnataka kuwa pamoja wakati wote. Kwa hivyo kufanya mapenzi ni jambo asili na la kufurahia kwa walio katika ndoa.
Lakini japo wakati unavyo zidi kusonga, ndivyo hisia zinavyo zidi kudidimia. Kazi inapatiwa kipau mbele. Kisha mnapata watoto, wanao stahili wakati mwingi. Mara nyingi wata sitiza juhudi zenu za kuwa na wakati wa kipekee kitandani. Uchovu wa kazi na kufanya kazi za nyumbani zinafanya iwe vigumu kuwa na nguvu tosha za kujihusisha katika kufanya mapenzi.
Baadhi ya wakati, hili ni sawa na kungoja wikendi. Lakini kuto fanya mapenzi huenda kukawa na athari hasi kwa uhusiano wenu. Tazama athari chanya za kufanya tendo la ndoa kila siku katika ndoa.
Mambo yanayo fanyika akilini na mwilini mwako unapo fanya mapenzi kila siku

- Kuimarisha ujasiri wako
Kufanya mapenzi na mchumba wako na kujaribu mitindo mipya na tofauti kuta kusaidia kuimarisha ujasiri wako. Kuna uwezekano wa wanawake kuhisi aibu baada ya kujifungua na kuhofia jinsi miili yao ilivyo. Ila, unapo zoea kufanya mapenzi mwili wako ukiwa hivyo, unapata ujasiri.
2. Kuboresha uhusiano kati ya wanandoa
Tendo la ndoa ni kitendo kinacho stahili wanandoa wawe makini. Kuelewa mwili wa mwingine na anacho taka, mambo yanayo mfanya asisimuke na kuwa tayari kufanya kitendo hicho. Mazungumzo ni muhimu sana. Na mnapo zidi kuzungumza na kuelewana zaidi, uhusiano wenu unakuwa bora zaidi. Kufanya kitendo hiki kila siku kuta fanya uhusiano wenu uwe bora zaidi.
3. Kuwa na ndoa bora

Kuwa na ndoa bora kuna tegemea vitu vingi tofauti. Kufanya mapenzi kila siku kunawafanya wanandoa wahisi kuwa wana umoja zaidi. Baada ya kitendo wanapata wakati wa kuzungumza na kujadili masuala waliyo nayo.
Wataalum wa mambo ya mapenzi na ndoa wana washauri wanandoa wanao jipata wakiwa na tofauti nyingi na kuto sikizana, kuanza kufanya mapenzi mara kwa mara. Kutenga wakati tosha wa kuwa pamoja, mbali na wanapo kuwa nyumbani waki wachunga watoto ama kufanya majukumu ya kinyumbani.
Mbali na kuboresha uhusiano kati yao, kufanya tendo la ndoa kila siku kwa wanandoa kunasaidia kupunguza mawazo mengi na kukuwezesha kulala vyema zaidi.
Soma Pia: Wanandoa Wenye Furaha Huongeza Uzito Pamoja Kulingana Na Sayansi