Utafiti: Sababu 11 Kwa Nini Wanawake Hutatizika Kufika Kilele Wanapo Fanya Mapenzi

Utafiti: Sababu 11 Kwa Nini Wanawake Hutatizika Kufika Kilele Wanapo Fanya Mapenzi

Hata kama kufika kilele katika ngono sio kitu cha kipekee cha kuangazia katika ngono, kuikosa ni suala linalo paswa kuangaziwa ili mpate maisha ya kingono na ndoa inayo tosheleza.

Wakati ambapo kufika kilele katika ngono sio dhibitisho la ngono ya kusisimua, hakuna kukana kuwa ni muhimu. Kufika kilele huboresha kutosheka kingono. Pia kumedhihirishwa kuwa na manufaa ya kiafya. Kuna boresha afya ya uke, kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo, kusawazisha usingizi, kukusaidia kupunguza uzito wa mwili na kupunguza uchungu. Kwa hivyo ukigundua kuwa unatatizika kufika kilele katika ngono, huenda ukawa una kosa kupata manufaa ya kiafya na kutoshelezwa kingono. Hata kama kuna baadhi ya sababu kwa nini wanawake wanaweza kosa kufika kilele.Tuangazie yanaweza kuwa nini.

Sababu Maarufu Zaidi Kwa Nini Wanawake Hawafiki Kilele

kuto fika kilele katika ngono

Habari mpya zilizo chapishwa kwenye makala ya Marital Sex & Therapy ziliangalia sababu kwa nini wanawake hufikiria kufika kilele katika ngono ni changamoto kwao.

Kati ya wanawake 452 walio husika kwa utafiti walio kuwa na matatizo ya kufika kilele, wali orodhesha sababu maarufu zaidi wanafikiria ni vigumu kwao.

Watafiti walifika aje kwa sababu hizi 11? Kwanza waliangalia wanawake 913 wenye umri zaidi ya miaka 18. Kwa nambari hii, 452 walionyesha kutatizika zaidi katika kufika kilele. Asilimia 45 ya wanawake hawa walikuwa na matatizo ya kufika kilele katika nusu ya vipindi vyao vya ngono. Asilimia 30 walipata kuwa vigumu kufika kilele kila mara walipo fanya mapenzi.

Kisha, watafiti walichukua sababu tofauti  -umri, wanakotoka, mtindo wa maisha, hali ya kuwa na mpenzi, historia ya afya, kufika kilele  -na kukadiria "kiwango cha dhiki" kinacho husishwa na matatizo ya kufika kilele.

Waliwapatia wanawake vikundi vifuatavyo vya kuchagua kutoka:

 1. Mapenzi na mchumba wako haya nisisimui
 2. Mapenzi nami hayaonekani kumsisimua mchumba wangu
 3. Si furahii kufanya mapenzi na mchumba wangu
 4. Mchumba wangu haonekani kufurahia kufanya mapenzi nami
 5. Sija tayarishwa vya kutosha wakati wa ngono
 6. Sina uowevu wa kutosha wakati wa kufanya mapenzi
 7. Na hisi uchungu nikifanya mapenzi
 8. Tuna harakisha ngono, kuto pata wakati wa kutosha
 9. Nina waza kwa kina kuhusu mwili wako na fizikia yangu
 10. Matibabu na hali fulani inani dhibiti kufika kilele
 11. Na hisi ni vigumu kufika kilele kwa sababu ya kufilisika kimawazo na wasiwasi

Asilimia 58 ya wanawake wali jibu kuwa na wasiwasi na mawazo mengi kuwa sababu kuu kwa nini hawawezi fika kilele

kuto fika kilele katika ngono

Hapa kuna sababu zingine kuu:

 • asilimia 48 walisema kuwa kukosa kuamshwa kingono ilikuwa sababu iliyo kisiwa
 • asilimia 40 walisema kuwa kutopata wakati tosha kuliwa dhibiti
 • asilimia 28 waliripoti hisia kuhusu miili yao
 • asilimia 25 walisema uchungu na kuto kuwa na starehe kulisababisha
 • asilimia 24 waliripoti kutokuwa na uowevu tosha kwa uke
 • na asilimia 17 peke yake ili laumu hali za kiafya

Daktari Grant Brenner aliandika kuwa mhusika anaweza shuhudia zaidi za sababu moja. Kwa mfano, wanawake wanaweza kuwa na fikira nyingi na wasiwasi kwa sababu ya kuto tayarishwa vya kutosha kabla ya ngono.

Wamama wanapaswa kukabiliana vipi na tatizo hili la kuto fika kilele?

Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 50 ya wanawake kamwe hawafiki kilele katika ngono. Ni muhimu kujua kuwa hakuna kitu kibaya nawe. Kutoweza kufika kilele haikufanyi kutokuwa mwanamke vya kutosha.

Kulingana na sababu zilizo tajwa hapo awali, ni dhahiri kuwa vyanzo vina husika na mawazo na hisia kuhusu ngono.

Sio siri kuwa kiwango cha kutosheka cha mwanamke katika ngono kina husika kwa karibu na hisia. Somo katika mwaka wa 2007 lilisema kuwa kutosheka kwa mwanamme katika ngono kunafuatia hisia zake.

Daktari Brenner ali shauri haya ili kuimarisha:

 • Kuboresha mitindo ya ngono
 • Kuimarisha mazungumzo kati yenu
 • Kumhimiza na kumwegemeza mchumba wako hasa asiye upenda mwili wake
 • Kuimarisha ubora wa uhusiano, kwa kumsikiliza mchumba wako
 • Ikiwa kuna matatizo ya kiafya yanayo sababisha, wanandoa wanapaswa kuzungumza na wataalum wa afya.

Hata kama kufika kilele katika ngono sio kitu cha kipekee cha kuangazia katika ngono, kuikosa ni suala linalo paswa kuangaziwa ili mpate maisha ya kingono na ndoa inayo tosheleza.

Vyanzo: Healthline, Psychology TodayNCBI

Soma Pia:Baadhi Ya Sababu Za Kupata Tathmini Za Ngono Mara Kwa Mara Katika Ndoa Yako

 

Written by

Risper Nyakio