Jinsi Kufikiria Sana Kutakavyo Haribu Uhusiano Wako

Jinsi Kufikiria Sana Kutakavyo Haribu Uhusiano Wako

Kupenda kwa dhati na kwa kweli kiasili hufanya watu wengi wawe na imani na wachumba wao bila wasiwasi na kuwaacha katika hatari ya kuvunjwa moyo na masikitiko. Hili linapo tendeka, kinacho fuata, kwa baadhi ya watu ni kuwa wao huingia kwa uhusiano mwingine wakiwa na maumivu kutoka kwa uhusiano wa hapo awali na kuwa na matatizo ya kuwaamini wachumba wao, na bila shaka uwoga mwingi wa kuvunjwa moyo tena.

Jinsi Kufikiria Sana Katika Uhusiano Wako Kuna Haribu Utangamano Wenu

kupata ngono nzuri

Kwa mtu ambaye alivunjwa moyo bila tahadhari ama hata kuona ishara zozote za uchungu huu ujao, kila tendo la wachumba wao wapya lita fikiriwa kwa kina na mara kwa mara kufikiria kwa njia isiyo faa.

Wanaume kama hawa hushangaa kama mwanamme mwingine aliye tajiri zaidi haja anza kufuata wachumba wao. Ikiwa hawajui mahali hasa alipo, tuhuma zao huongezeka na wao huanza kuwapigia mara kwa mara wakiwa na shaka kuwa wanaweza wachwa wakati wowote.

Huenda mwanamme huyo akawa amenyamaza tu. Wanawake katika kundi hili huanza kutia shaka na kuanza kushangaa anacho panga. Atamalizana na mimi? Je, amepata mtu mwingine?

Kuwa na hisia nyeti na kuwa makini kwa mchumba wako ni jambo asili hadi kwa kiwango ambapo watu huanza kuonyesha tabia kama kufikiria zaidi kuhusu kila tendo, kutahini mambo zaidi ama kujaribu kung'amua maana ya kila kitu ambacho mchumba wako anafanya, bila shaka kuna tatizo.

Ili kukumbana na tatizo hili, mazungumzo yana baki kuwa jibu kuu.

Badala ya kujaribu kusoma mawazo ya mchumba wako ama kuanza kudadisi matendo yake, mbona usikae nao na uwe na mazungumzo wazi? Mara nyingi, tatizo huenda likawa liko mawazoni mwako. Baada ya kufikiria sana kuhusu mambo yasiyo kuwepo.

Ni vyema kutia juhudi maishani na kuboresha kujiamini kwako kifizikia, kihisia na kiakili. Pia, epuka kujilinganisha na watu wengine ama kulinganisha uhusiano wenu na uhusiano ulivyo kuwa nao na wachumba wako wa hapo awali.

Haisaidii mtu yeyote unapo kwamilia maumivu ya kiroho ya hapo awali. Badala yake, jaribu kuwa na mazungumzo na mchumba wako kuona jinsi mnavyo weza kubadili nyanja tofauti. Pumzika, kwani kufikiria sana katika uhusiano kuna haribu uhusiano wenu.

Soma Pia: Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Written by

Risper Nyakio